Anachofanya Lissu ni uhaini

Anachofanya Lissu ni uhaini

kwa hiyo wajibu wenu ni kushiriki kuikandamiza badala ya kusaidia njia bora. Je kwa busara ya mihilimi mitatu ndege haikuja? Bado mmesupataza shingo shame on you
Huo unaofanya ni ushabiki maandazi tu,Sikh akili zikikurudia utaelewa
 
Dawa pekee ya kumnyamazisha Lissu huko Duniani aliko ili aachane na kuituhumu serikali yake, dawa hiyo aliyenayo ni serikali yenyewe kujishughulisha na suala la Lissu ikiwa ni pamoja na ;

1.Serikali kutoa ushahidi usio na shaka wa mtu halisi aliyehusika kumshambulia Lissu

2. Serikali kuieleza Dunia walikokuwa walinzi waliokuwa zamu kulinda nyumba za serikali wakati Lissu anashambuliwa.

3. Serikali kuieleza Dunia zilikokwenda CCTV camera baada ya Lissu kushambuliwa.

Kwa nini serikali ndo inapaswa kuwa na majibu haya? Kwa sababu ndo pekee ina mamlaka ya kutoa majibu hayo na si mwingine!!! Hayo ndiyo maswali pekee ambayo Lissu amekuwa akiyauliza kila kwenye chombo cha habari cha kimataifa anachoalikwa!!
Tukio litokea Dodoma,Tanzania nchi huru.Majibu mnayatafuta BBC,CNN mtajibiwa kihuni vivyo hivyo katiba imeweka utaratibu wa kughulikia matatizo ya watu pamoja na watu kuwasiliana na serikali
 
Aliyeleta uzi naomba kasome sheria zinazomruhusu Rais kuingilia pillars zingine. Halafu kumkosoa Rais According to our constitution sio kosa kwa taarifa yako.
[emoji1] [emoji1] [emoji1]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamhuri ya muungano wa Tanzania ina katiba inayotambua Rais,Bunge na mahakama. Unapotukana mihimili hii mitatu unajunja katiba inayoweka miiko na taratibu za nchi.

Katiba inamtambua rais aliyepatikana kwa kura za wananchi, unapohamasisha Rais apingwe kila kona na kususiwa huo sio UASI.

Rais hakukwapua madaraka kama unavyotaka yakwapuliwe. Ujuwe kwa katiba hii kama utakuwa Rais kwa mkono wa wafadhili wako sawa lakini kama ni katiba hii wewe ni Muasi tayari.

Bunge ni mhimili mwingine unaoubeza ambao umekulea na kukuapisha kutii katiba na sheria za nchi pia unayo kura ya kutokuwa na imani na Rais kwa nini usitumie ushawishi kikatiba kumtoa Rais madarakani.

Kama kuna kuvunja katiba kuna mahakama ya Katiba lakini umeamuakutumia shortcut. Hukumbuki shortcut itakulazimu kuja na majeshi yako, katiba yako, wanajeshi wako, usalama wako nje ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Absolutely wewe ni Muasi
Waasi ni wale waliopanga mipango ya kumuua, kukataa kumtibu, kumnyima mishahara nk.
Muhaini mnaye kiongozi wa kirundi!
 
Jamhuri ya muungano wa Tanzania ina katiba inayotambua Rais,Bunge na mahakama. Unapotukana mihimili hii mitatu unajunja katiba inayoweka miiko na taratibu za nchi.

Katiba inamtambua rais aliyepatikana kwa kura za wananchi, unapohamasisha Rais apingwe kila kona na kususiwa huo sio UASI.

Rais hakukwapua madaraka kama unavyotaka yakwapuliwe. Ujuwe kwa katiba hii kama utakuwa Rais kwa mkono wa wafadhili wako sawa lakini kama ni katiba hii wewe ni Muasi tayari.

Bunge ni mhimili mwingine unaoubeza ambao umekulea na kukuapisha kutii katiba na sheria za nchi pia unayo kura ya kutokuwa na imani na Rais kwa nini usitumie ushawishi kikatiba kumtoa Rais madarakani.

Kama kuna kuvunja katiba kuna mahakama ya Katiba lakini umeamuakutumia shortcut. Hukumbuki shortcut itakulazimu kuja na majeshi yako, katiba yako, wanajeshi wako, usalama wako nje ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Absolutely wewe ni Muasi

Kauli kama hizi ni za WALEWALE ambao Lissu ameahidi kuwataja akiwa hai au amekufa.
Kabla hujaleta hoja yako ya kichizi hapa kwanza jiulize maswali haya:
  1. Unasemaje kuhusu WASIOJULIKANA ambao mpaka leo Serikali yako haijawakamata?
  2. Nani mhaini kati ya anayataka KUUA RAIA WASIO NA HATIA na ANAYE IELEZA DUNIA KWANINI ALIMININIWA RISASI 38 HUKU 16 ZIMWIINGIA MWILINI?
 
So sad kwa mtu ambaye amelishwa maneno na ufahamu wakati hali inaonesha. Ni sawa na mtu kuwasha air condition akiwa njombe huku anadai kuwa kuja joto sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una haki ya kutoa maoni na kusikilizwa.
Toka Lisu azungumze na Hardtalk ya BBC, hata wasio na ufahamu wanalalama na kutunga uongo ili kufurahisha mfumo.
Tafuta tafsiri ya uhaini. Naona umejaa hofu kuwa rais atapinduliwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuna anachodanganya ama ni nn

Sent using Jamii Forums mobile app
Kitu kinachowaumiza ni kwamba jamaa anaonekana kusema ukweli mwingi Rather than unafiki wa viongozi wengi kwa kigezo cha kumpa heshima ambayo hata katiba haitambui.
Na mbaya ni kwamba kuna baadhi ya fursa ndo basi tena kwa Tanzania ila nyumbu hatuoni hilo tunakazana na Lissu kurudi Home utadhani ndo huwa tunampatia huduma zake za kijamii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sheria ya Uhaini. Na.2 ya 1970 Jedwali
SURA YA SABA

UHAINI NA MAKOSA MENGINE DHIDI YA SERIKALI
39.-(1) Mtu yeyote ambaye yumo ndani ya Jamhuri ya Muungano
(a) akiwa ndani ya Jamhuri ya Muungano au popote, anamuua au anajaribu kumuua Rais; au
(b) akiwa ndani ya Jamhuri ya Muungano anaanzisha vita dhidi ya Jamhuri ya Muungano,
atakuwa na hatia ya kosa la uhaini na atawajibika kwa adhabu ya kifo.

(2) Mtu yeyote ambaye, yumo katika ndani ya Jamhuri ya Muungano, akiwa ndani ya Jamhuri ya Muungano au popote, anajenga nia kusababisha au kuwezesha kusababishwa, au anajenga nia ya kuchochea, anashawishi, shauri au kuusia mtu yeyote au kikundi cha watu kusababisha au kuwezesha kusababishwa yoyote kati ya matendo au malengo
yafuatayo, yaani:-

(a) kifo, kumlemaza au kumjeruhi, au kufungwa au kumzuia,
Rais;

(b) kumwondoa Rais madarakani isivyo halali kutoka katika
wadhifa wake wa Urais au kumwondolea ufahari, heshima na jina la Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Jamhuri ya Muungano;

(c) kupindua kwa njia zisizo halali, Serikali ya Jamhuri ya Muungano; au

(d) kutishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Bunge na Mahakama ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano,
na kubainisha nia hiyo kwa kuchapisha maandishi or machapisho au kwa kitendo chochote cha siri kinachojionyesha cha hali yoyote, atakuwa na hatia ya kosa na atawajibika kwa adhabu ya kifo.

(3) Mtu yeyote ambaye, yumo katika utii wa Jamhuri ya Muungano–

(a) aliye na mshikamno na maadui wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au anawapa msaada au hifadhi ndani ya Jamhuri ya Muungano au kwingineko;

(b) anachochea, aidha ndani ya Jamhuri ya Muungano au kwingineko, mtu yeyote aivamie Jamhuri ya Muungano kwa kutumia jeshi; au

(c) anabeba silaha ndani ya Jamhuri ya Muungano kwa amri, kwa nia ya kutumia nguvu ya kuizuia, kuilazimisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano kubadilisha vigezo au ushawishi wake, au kwa nia ya kulazimisha au kuzuia au kutishia, Serikali ya Jamhuri ya Muungano,
atakuwa na hatia ya kosa la uhaini na atawajibika kwa adhabu ya kifo.
Mkuu K
Tatizo lenu kubwa nyinyi mazuzu ni kwamba huwa mnamuelewa mtu anayeandika yale yanayowapendeza machoni na mioyini mwenu. Sina muda wa kukulisha upumbavu ili nafsi yako isuuzike. Nimeweka vifungu vya sheria. Kwa utashi na upeo wako wa kikamanda ukapigwa na upofu na kubadili GIA angani kama kawaida yenu.

Some tena vifungu vya sheria vinasemaje kuhusu MHAINI hapo chini...

Sheria ya Uhaini. Na.2 ya 1970 Jedwali
SURA YA SABA

UHAINI NA MAKOSA MENGINE DHIDI YA SERIKALI
39.-(1) Mtu yeyote ambaye yumo ndani ya Jamhuri ya Muungano

(a) akiwa ndani ya Jamhuri ya Muungano au popote, anamuua au anajaribu kumuua Rais; au

(b) akiwa ndani ya Jamhuri ya Muungano anaanzisha vita dhidi ya Jamhuri ya Muungano,
atakuwa na hatia ya kosa la uhaini na atawajibika kwa adhabu ya kifo.

(2) Mtu yeyote ambaye, yumo katika ndani ya Jamhuri ya Muungano, akiwa ndani ya Jamhuri ya Muungano au popote, anajenga nia kusababisha au kuwezesha kusababishwa, au anajenga nia ya kuchochea, anashawishi, shauri au kuusia mtu yeyote au kikundi cha watu kusababisha au kuwezesha kusababishwa yoyote kati ya matendo au malengo
yafuatayo, yaani:-

(a) kifo, kumlemaza au kumjeruhi, au kufungwa au kumzuia,
Rais;

(b) kumwondoa Rais madarakani isivyo halali kutoka katika
wadhifa wake wa Urais au kumwondolea ufahari, heshima na jina la Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Jamhuri ya Muungano;

(c) kupindua kwa njia zisizo halali, Serikali ya Jamhuri ya Muungano; au
(d) kutishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Bunge na Mahakama ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano,
na kubainisha nia hiyo kwa kuchapisha maandishi or machapisho au kwa kitendo chochote cha siri kinachojionyesha cha hali yoyote, atakuwa na hatia ya kosa na atawajibika kwa adhabu ya kifo.

(3) Mtu yeyote ambaye, yumo katika utii wa Jamhuri ya Muungano–

(a) aliye na mshikamno na maadui wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au anawapa msaada au hifadhi ndani ya Jamhuri ya Muungano au kwingineko;

(b) anachochea, aidha ndani ya Jamhuri ya Muungano au kwingineko, mtu yeyote aivamie Jamhuri ya Muungano kwa kutumia jeshi; au

(c) anabeba silaha ndani ya Jamhuri ya Muungano kwa amri, kwa nia ya kutumia nguvu ya kuizuia, kuilazimisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano kubadilisha vigezo au ushawishi wake, au kwa nia ya kulazimisha au kuzuia au kutishia, Serikali ya Jamhuri ya Muungano,
atakuwa na hatia ya kosa la uhaini na atawajibika kwa adhabu ya kifo.
Mkuu Katiba haisomwi kama kitabu cha riwaya au gazeti mkuu, kila sentensi na kila neno katika Katiba au Sheria yoyote imebeba maana specific kisheria. Kimsingi tafsiri ya kila kifungu cha sheria haitokani na namna mtumiaji anavyoitafsiri, bali inatokana na 'Legal Agreement' kulingana na muktadha wa sheria hiyo inapotungwa. Na ndio maana sheria inaposhindwa kukidhi mahitaji kunafanyika amendment, hailazimishwi kufit katika mazingira ambayo siyo yake.
Hakuna hata sehemu moja ambayo Tundu Lisu amewahi kufikiria au kutamka au kuyaomba mataifa ya nje kusaidia kumtoa rais madarakani aidha kwa kuchochea vita, au kwa kumuondolea rais fahali yake, au kumwondolea rais ukuu wa nchi wala ukuu wa serikali. Anachokifanya Tundu Lisu siku zote ni kupinga na kukosoa vitendo vinavyokiuka haki na vinavyovunja sheria. Rais wetu anapenda ukweli, na anapenda watu wakweli, sasa kumwambia ukweli kwamba hiki umekosea na madhala yake yatakuwa hivi na vile kama alivyotahadhalisha tangu mwanzo suala la ndege kuzuiliwa kwasababu ya mikataba tuliyosaini ya kimataifa, uhaini uko wapi hapo?. Ameiambia dunia imsusie, hajaiomba imtoe madarakani kwa namna yoyote ile. Ndio maana nimetangulia kukwambia sheria haisomwi kama gazeti mkuu, kila neno linatoa tafsiri husika kisheria na Tundu Lisu anajua namna ya kutumia maneno kisheria. Na ndio maana hakuna mtu yoyote aliyemfungulia ama anayeweza kumfungulia mashtaka Tundu Lisu mahakamani kwa kosa la "uhaini", sana sana wataishia kusema uchochezi, na kutoa vitisho vingi ambavyo havina msingi wowote. Na kama huamini, jaribu kwenda mahakamani hata sasa hivi kamfungulie Lisu mashtaka ya kosa la Uhaini halafu njoo utupe report mkuu kesi itakapofikia. Ikumbukwe kwamba chombo chenye dhamana ya kutafsiri sheria ni mahakama peke yake, na hata ikitokea Tundu Lisu atakutwa na hatia hiyo ya uhaini, mahakama yenye dhamana ya kutoa 'death sentences", na wala siyo chombo kingine chochote. Ndiyo maana wenye akili wanajiuliza, ukisema kilichompata Lisu september 27, 2017 ndio malipo ya uhaini inamaana tunaitangazia dunia kuwa mahakama ndiyo iliyotoa agizo la mbunge huyu kumiminiwa risasi ikiwa ni kama hukumu kwa uhaini wake? Mimi siamini hivyo, maana hakukuwahi kuwa na kesi yoyote aliyoshitakiwa Lisu kwa kosa la Uhaini, haipo. Hivyo kuhusisha shambulio lile na adhabu ya uhaini ni kuzidi kulichafua taifa, maana katika utawala wa sheria hata inapotokea mtu akahukumiwa kifo kuna utaratibu uliowekwa kisheria. Hivyo sidhani kama ni busara kulitazama jambo hili kwa jicho hilo.
 
tangu lini kukosoa serikali ni uhaini?
Kamuulize shangazi yenu Fatma kwa nini jina lake halikupendekezwa katika wagombea wa nafasi ya Urais wa TLS awamu Ijayo!? Ndio utapata jibu kamili. Kuna tofauti kubwa sana kati ya kuikosoa serikali na kuikosoa kwa kutumia lugha za Matusi, kejeli, kebehi, kejeli na utovu wa nidhamu.
 
Back
Top Bottom