Anaandika Binamu Binanga kuhusu madai ya Katiba Mpya

Linguistic

JF-Expert Member
Mar 16, 2021
3,671
8,238
Wengi akili imeelemea kwenye kudai Katiba Mpya. Hili ni wazo jema sana. Lakini tumewaza vizuri vita tunayoipigana? Silaha tunazotumia? Tuko tayari na matokeo ya vita hii?


Nimemsikikiza wakili msomi Peter Kibatala alipofanya uchambuzi wa kishule (sio kiharakati) nimemuelewa sana

Mchakato wa katiba ulishafika hatua fulani,
Rasimu ya Jaji Warioba tayari na wengi wanaamini ni maoni ya wananchi
Bunge la katiba lilijadili (licha ya wapinzani kususia) na mwisho ilikuwa ni wananchi kuipigia kura Rasimu iliyorekebishwa na Bunge (jambo ambalo halikufanyika). Na ikumbukwe aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Katiba ndiye Rais wa sasa Samia Suluhu Hassan

Je, tuanzie wapi?

1-Mwanzo? (Maoni ya wananchi)
2-Katikati? (Rasimu ya Warioba)
3-Mwisho? (Kura za Bunge)

Kwa mujibu wa sheria Tume ya Taifa ya Uchaguzi na ile ya Zanzibar zina role kubwa kwenye kufanikisha *kuipata katiba tuitakayo. Kwa nn tusiwekeze nguvu kuitaka tume huru kwanza kabla ya katiba mpya?

Bunge la sasa la Tanzania na lile la wawakilishi ambayo majority ni CCM ni sehemu muhimu ktk mchakato huu, TUNAPITIA WAPI? Tunaimani kwamba watakataa mapendekezo yanayoweza kukiweka chama chao hatarini kisha wakubali yanayowapa favour wapinzani? Tutakuwa tume VUTA mlango ulioandikwa PUSH na tukitarajia ufunguke.

Naanza pia kuelewa kwa nn kuna watu wanashauri kuwe na mchakato wa maridhiano kuhusu katiba kati ya makundi mbalimbali. Wanasiasa wawe sehemu muhimu ya mjadala huu ila wasiutawale mjadala huu, maana ni katiba ya wananchi inayotafutwa!

TUCHAGUE VITA YA KUPIGANA
TUCHAGUE SILAHA ZA KUTUMIA

Hizi ni akili zangu na huwa najivunia nazo, sishikiwi akili.

But I stand to be corrected!
 
Mkuu umeandika vema lakin suala la kupata tume huru kwa katiba hii ya sasa ni vigumu! Sabab kwa katiba ya sasa anayehusika kuteua watendaji wote wa tume ni Rais ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM, Je unategemea tutaje tume huru hapo?? Mie nadhani tupate kwanza katiba itakayomuondoa mwenyekiti wa chama cha siasa kuwa muundaji wa tume inayoshindanisha chama chake na vyhama vingine, Kwa msingi huo hapa ni katiba kwanza, then tume huru!
 
Msingi wa utawala wo wote ni katiba! Katiba ndiyo itaweka mwongozo na dira ya Taifa. Hivyo tuanze na katiba vingine vyote vitafuata.
 
Back
Top Bottom