Ana wivu sana.

DERICK2000

JF-Expert Member
Apr 8, 2012
203
35
Ananipenda sana,ila anawivu mno mpaka ananiudhi..Dawa yake ni nini wana mmu?.nataka anipende kiasi..
 
Nawe mpende sana na uwe na wivu pia kwake.

Ukitaka kusaidiwa basi jieleze vizuri watu wakuelewe maana swali lako fupi na utapata majibu mafupi pia.
 
Wivu siku zote ni mbaya na mtu mwenye wivu mara nyingi hajiamini.
 
Wivu ni kipimo cha upendo mtu akupedacho, sasa kama wewe huo wivu huutaki mwache halafu upate asiyekuwa nao ili uish kwa uhuru.
 
dadavua kidogo,
ila kwa nini ana wivu uliopitiliza?
je hajiamini?
au umeweka mazingira ya kutoaminika?
 
Mtaftie yeye small house (yaani awe na kidumu), utaona hatakuwa na time na wewe kabisaa! Bishanga anafaa kuwa kidumu manake mkewe mkali, so hatataka kukutoa KO.

Pole kwa kupendwa sana.
 
Wajinga ndo waliwao..kama unamuonyeshea live vicheche wako akuchekee tu?.

Soln:mwache akamuonee wivu mwingine.
 
Mwache .ataacha kukupenda sana na atakusahau then utakua huru.

Dah umemjibu vizuri sana, ninachoamini wivu ni ngao ya mapenzi, mara nyingi watu wenye vidumu huwa hawapendi waonewe wivu, Wivu ni kipimo cha mapenzi... Wanaume wengine bwana, eti anawivu mpaka ananikera, khaaaaaa.. !!! Kweli anakukera mtoto wa watu? Ulitaka awe anakaa kimya ili uhisi kuwa hupendwi? Mapenzi hayako hivyo, "ukiamua kuolewa usiogope kulala uchi".. Na wewe ukimpenda kikweli YEYE PEKEYAKE na wewe utakua ktk viatu vyake tu, ukimshindwa sana nikaPM namba zake..
 
We nawe. . .
Kupendwa sana hakutoi matokeo ya kutoaminiwa na kuonewa wivu kupitiliza , hilo ni tatizo na anaweza hata akawa nalo mtu asiyekupenda sana. Hivyo usijiridhishe kuwa unapendwa SANA kisa tu mwenzio haachi kuwa na hofu/shaka juu yako.

Nwy kama unampenda, ni mwaminifu, hujampa sababu ya kuamini sio mwaminifu na unapenda mahusiano yenu yaendelee msaidie kuelewa kwamba tatizo liko kwake na sio kwako wewe. Niliwahi kuandika hii huko nyuma. . . https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/210439-paranoia-2.html
. . . ITUMIE.
 
Dah umemjibu vizuri sana, ninachoamini wivu ni ngao ya mapenzi, mara nyingi watu wenye vidumu huwa hawapendi waonewe wivu, Wivu ni kipimo cha mapenzi... Wanaume wengine bwana, eti anawivu mpaka ananikera, khaaaaaa.. !!! Kweli anakukera mtoto wa watu? Ulitaka awe anakaa kimya ili uhisi kuwa hupendwi? Mapenzi hayako hivyo, "ukiamua kuolewa usiogope kulala uchi".. Na wewe ukimpenda kikweli YEYE PEKEYAKE na wewe utakua ktk viatu vyake tu, ukimshindwa sana nikaPM namba zake..

Wivu ukizidi ni KERO na laweza kuwa tatizo la kisaikolojia kwahiyo usitake watu wavumilie kero eti kuwa ndio mapenzi. Hata wasio na mapenzi ya kutosha wanaweza kuonyesha wivu kwasababu ya kupenda KUMILIKI wenzao iwe wanawapenda au hawawapendi.
 
Ananipenda sana,ila anawivu mno mpaka ananiudhi..Dawa yake ni nini wana mmu?.nataka anipende kiasi..

Kupendana huendana na ka-degree ka wivu kwa wapendanao. Ukiona watu wanasema wanapendana na hawaoneani wivu hata kidogo, ujue hapo hakuna upendo ni uzushi tu na kuzidanganya nafsi zao. Ila ukiona wivu umezidi kupita kiasi, then hilo ni tatizo. Jaribu kukaa na huyo mwenzio na mweleze kwamba ajaribu kujiamini na kukuamini ya kuwa umejitoa kwake na huna mpango wa kuwa na mwingine, so atulie tu na kurelax.
 
Wivu ukizidi ni KERO na laweza kuwa tatizo la kisaikolojia kwahiyo usitake watu wavumilie kero eti kuwa ndio mapenzi. Hata wasio na mapenzi ya kutosha wanaweza kuonyesha wivu kwasababu ya kupenda KUMILIKI wenzao iwe wanawapenda au hawawapendi.

Asante Mkuu, nimekuelewa vizuri sana
 
Wivu ukizidi ni KERO na laweza kuwa tatizo la kisaikolojia kwahiyo usitake watu wavumilie kero eti kuwa ndio mapenzi. Hata wasio na mapenzi ya kutosha wanaweza kuonyesha wivu kwasababu ya kupenda KUMILIKI wenzao iwe wanawapenda au hawawapendi.

Lizzy, Ndio maana awali nikamwambia hajaeleweka....afunguke kidogo kwasababu tafsiri ya "kupendwa sana" inaweza kuwa tofauti baina ya mtu na mtu..na pia sio sio kila kupenda sana kunatafsiriwa kama wivu. Tatizo mtoa hoja kaingia mitini ndo maana wachangiaji tunakosa muelekeo....
 
Ananipenda sana,ila anawivu mno mpaka ananiudhi..Dawa yake ni nini wana mmu?.nataka anipende kiasi..
Dawa ya mtu mwenye wivu ni kufanya vile anavyotaka ili umridhishe,tatizo linakuwa kama wewe haujampenda kihivyo lazima akunyime raha na kama hapo ndio umefika we yatimize tu na utaona sio kero bali raha ya ajabu.Ila umeniboa hapo unaposema unataka akupende kiasi ina maana wewe hauko serious na kitu kinachoitwa mapenzi bali ni wale onjaonja.
 
Back
Top Bottom