Ana uraia wa nchi mbili,anataka kumiliki ardhi afungue kiwanda cha juice TZ!

Wonderful

JF-Expert Member
Apr 8, 2015
7,347
5,984
Wana bodi,

Nina ndugu yangu yupo Europe kwa muda mrefu sasa na tayari ameshachukua passport ya huko ingawa hajaukana utanzania wake.

Sasa amehamasika kuwekeza nyumbani na kwa kuanzia anataka kununua ardhi Pwani kwaajili ya kukamua matunda ya aina mbalimbali ili kupata juice.

Sasa wakati akifatilia ununuzi wa plot ndio akaambiwa haiwezekani maana yeye ameshaukana uraia ingawa si kweli kama ameukana utanzania wake.

Je hapa hili jambo likoje?

Maana hayupo tayari kuukana utanzania wala uzungu na anaendelea kutumia passport mbili.
 
Hapa tanzania hairuhusiwi kuwa na uraia wa nchi mbili, ukichukua uraia wa nchi nyingine automatic umeukana utanzania.
Duh!!
Ok thx.
Ila si sawa.
Nina rafiki yangu mkenya ana uraia wa czech republic na kenya,ni mfanya biashara wa mboga ana export.
Why Tanzania???
 
kaka, huyo ndiyo kwa kheri kwa manene machache tu.

Hadi hapo wewe muombe akupe hizo hela uendeshe viwanda yeye arudi bara Europa akaendeleze mishe za kusaka noti huko.

Ila kuwa na uraia picha kwa Tanzania hiyo sheria ilikataliwa.

Kama wadau , wengine.walivyo sema kuwa ukichukua uraia wa nchi nyingine kwa sheria ya Tanzania wewe umejifuta huu wa hapa nyumbani hata kama hujasema kwa kinywa chako.

Mfano, hapo ni bwana Manji, naye kwa sasa yuko katika hilo kundi la ndugu yako.
 
Wana bodi.
Nna ndugu yangu yupo europe kwa muda mrefu sasa na tayari ameshachukua passport ya huko ingawa hajaukana utanzania wake.
Sasa amehamasika kuwekeza nyumbani na kwa kuanzia anataka kununua ardhi Pwani kwa ajiri ya kukamua matunda ya aina mbalimbali ili kupata juice.
Sasa wakati akifatilia ununuzi wa plot ndio akaambiwa haiwezekani maana yeye ameshaukana uraia ingawa si kweli kama ameukana uTZ wake.
Jee hapa hili jambo likoje?
Maana hayupo tayari kuukana utz wala uzungu na anaendelea kutumia passport mbili.
Aje afungue kampuni yake then kampuni inunue ardhi ya kujenga hiko kiwanda.

Aongee na TIC anaweza kupewa enep bure,awe na mtaji $500,000!
 
Aje afungue kampuni yake then kampuni inunue ardhi ya kujenga hiko kiwanda.

Aongee na TIC anaweza kupewa enep bure,awe na mtaji $500,000!

Mkuu na mimi ningemshauri hivyo hivyo. Ila wakati anafanya usajili wa kampuni hiyo ni lazima miongoni mwa wanahisa awepo Mtanzania.

Mkuu Wonderful unaweza kuni-pm kwa ushauri zaidi.

Kaka ...
 
Aongee na TIC anaweza kupewa enep bure,awe na mtaji $500,000!


Hapana, mtu ambae sio raia wa Tanzania hawezi KUPEWA ardhi.

Sheria inayokataza wageni kupewa ardhi haisemi ukiwa na ma trilioni kadhaa tuta suspend sheria, hapana. Ardhi Tanzania anapewa MTANZANIA mwenye ma trilioni na mwenye hela sifuri and anybody in between.
 
Hapana, mtu ambae sio raia wa Tanzania hawezi KUPEWA ardhi.

Sheria inayokataza wageni kupewa ardhi haisemi ukiwa na ma trilioni kadhaa tuta suspend sheria, hapana. Ardhi Tanzania anapewa MTANZANIA mwenye ma trilioni na mwenye hela sifuri and anybody in between.
Usibishe kitu ambacho hujui. Akifungua kampuni inakuwa imesajiliwa tz kwahio ni kampuni ya kitanzania hivyo inaweza kufanya chochote.
 
Ukishachukua Hati ya kusafiria ya nchi nyingine hapo ni dhahiri na moja kwa moja umeukana uraia wako wa Tanzania. Haya ni makosa ambayo ndugu zetu wengi wanaoishi Ughaibuni wameyafanya na inawagharimu pindi wanapohitaji kurudi nyumbani na kununua ardhi au hata kufanya mambo ya kimaendeleo n.k.
 
Duh!!
Ok thx.
Ila si sawa.
Nina rafiki yangu mkenya ana uraia wa czech republic na kenya,ni mfanya biashara wa mboga ana export.
Why Tanzania???
Tanzania hairuhusu dual Citizenship.Ila nchi kama Kenya inaruhusu.Yaani unaweza ukawa raia wa Kenya then ukawa raia wa nchi nyingine ,kwa Tanzania hatuna hiyo sheria.Cha kufanya kama wewe ni muaminifu ungenunua hiyo ardhi kwa majina yako usimamie hicho kiwanda then mgawane faida.Au jamaa aingie kama foreign ivestor.Fuatilieni taratibu sehemu husika naamini zipo vizuri tuu ila muachane na mambo ya siasa kabisa kama itawezekana.
 
Awe na kampuni atapewa derivative right of occupancy na TIC. NI PM
 
Usibishe kitu ambacho hujui. Akifungua kampuni inakuwa imesajiliwa tz kwahio ni kampuni ya kitanzania hivyo inaweza kufanya chochote.

Ridiculous, ingekuwa hivyo Wakenya wangekuwa wanasajili kampuni halafu wanamiliki ardhi.

Unanambia mimi ndio sijui?

Hujui chochote!

Foreign owned company iliyosajiliwa Tanzania ikiomba kutumia ardhi Kamishna wa Ardhi anampa TITLE DEED Mkurugenzi Mkuu wa TIC, kwenye sehemu ya mmiliki inajazwa TIC. Mwekezaji anapewa DERIVATIVE RIGHTS.

Ndio maana wekezaji wanalalamika kwamba wakienda benki kuomba mikopo na derivative right title deed mabenki mengi yanakataa kwa sababu TIC ndio mmiliki wa title mwisho wa siku.

Unanambia nisibishe kitu ambacho sikijui, wewe unajuaje kwamba wewe unajua mimi sijui? We vipi wewe?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom