Nilikua kwenye mahusiano yasiyo rasmi na mwanaume mmoja ambaye sasa namuona kama mume mtarajiwa, ila kabla mahusiano yetu hayajakomaa niligundua anamfuatilia binti mmoja ambaye wanakaa karibu lakini baada ya kumuuliza alikubali na kusema alipitiwa tu ananipenda mimi.
Alimpigia simu huyo binti na kumwambia ananipenda Mimi na amsamehe kwa kumpotezea muda na Mimi binafsi nampenda sana huyu kaka na Jana tu ametoka kumwambia mama yake kuwa yupo kwenye mahusiano na Mimi na tulivyopanga na yeye mwakani tunafunga ndoa.
Naombeni ushauri wanajamvi kwani huwa naingiwa na hofu namuomba sana Mungu anisaidie nifunge ndoa na nampenda sana mwenzangu huyu