Ana mtoto, nawezaje kuwa salama?

Ana mtoto, nawezaje kuwa salama?

Habarini wadau wa humu,mwenzenu nina shida na ninakuja kwenu nikiwa na matumaini ya kupata ushauri mzuri na unaojenga.
Mimi ni mwanamke mwenye miaka 28. Nina mpenzi ambaye tuko mbioni kutambulishana. Mwenzangu ana mtoto mdogo ambaye alimpata kabla hatujakutana naye.
Mara ya kwanza aliponiambia hilo swala, sikuliweka maanani. Lakini kwa kipindi ambacho tunataka kuwa kitu kimoja, nimeanza kupata mashaka. Mtoto ni mdogo na wala sijawahi hata kukutana naye.
Tatizo nina hofu. Hofu hiyo inatokana na siku nilipokutana na mama mkwe ambaye aliniuliza juu ya kuwa na mume mwenye mtoto. Mimi nikamjibu kirahisi kuwa ni sawa tu, mtoto hana shida as long as alipatikana kabla hatujakutana naye. Mama mkwe alitoa mawazo yake kuwa kunapokuwa na mtoto wa nje basi familia inakuwa na shida kidogo.
Jambo la pili linalonitia hofu ni kwamba, mimi pia nina ndugu ambaye tulizaliwa kwa baba mmoja. Alilelewa nyumbani toka akiwa mdogo lakini sasa amekuwa mtu ambaye ni ugonjwa kwa familia.
Jambo la tatu ni kwamba, mwenzangu ni mtu wa kutafsiri jambo hata kama jema ataliweka kwenye ubaya. Najiuliza, tutakapoishi na huyu mtoto, chochote nitakachofanya hata kwa uzuri, mwenzangu si atatafsiri vibaya na hapo ndoa itakuwa ndoano. Na ni lazima mtoto aishi naye yeye baba.
Nampenda jamaa lakini hofu yangu ni furaha na amani kwenye ndoa. Ushauri tafadhali.
Hapo hakuna shida kama unajua maana ya ndoa,ndoa inahitaji uvumilivu ambao hujawahi kukutana nao tokea uzaliwe,sasa kama umeamua na unampenda huyo mwanaume fungeni ndoa,ingawa ndoa ikishakuwa na mtoto wa nje kama hivyo nisikufiche mdogo wangu mara nyingi ina changamoto nyingi sana na hizo ambazo umeanza kuziona ni baadhi tu.
 
Hahaaa Atakufa kwa presha
Huyu anataka akutane na wanaume kama mimi ambae baada ya ndoa ndipo naenda kuzaa na mchepuko, kisha namleta ndani....[emoji12] [emoji12]
[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
mama mkwe yupo sahihi kabisa kuku uliza mapema maana vibinti vingi huwa vina manyanyaso au ubaguzi kwa watoto wasio kuwa wao,ni tofauti na sisi wanaume huwa tunapenda hata visivyo kuwa vyetu
 
Hahaaa Atakufa kwa presha
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Kazi ya moyo ni kusukuma dam
[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
Akina Mama wengi mnakuaga na inferiority complex juu ya watoto wa kambo,yaani mmeshajiwekea kua ukikaa na mtotot wa mwenzio lazima umtese ndio maana na wewe umeshsjiwekea tayari kichwani kuwa utashindwa kwa kua unajaua kua lazima utamtesa,sasa mtoto mdogo anakusumbua kwa lipi?
Na hii ni funzo kwa akina mama wote wa kambo,unaweza mlea mtoto asiye wako na akakukumbuka maisha yako yote,mimi ni nina jamaa yangu alilelewa na mama wa kambo na akasoma mpaka alikotaka yeye tene kwa upendo mkubwa,jamma saa hizi ni mtu mkubwa tu hapa nchini,mama yake halisi yupo ila huwa anasema wazi kuwa anampenda mama wa kambo na atamjali kuzidi hata mama yake wa kumzaa,
Napoleon Hill alikuwa ni mwandishi mhiri sana dunuani ambaye mpaka leo vitabu vyake vimewahamasisha watu wengi sana,kipaji chake kiligunduliwa na kukuzwa na mama yake wa kambo,
Sasa mtu ameshakuweka wazi mapema kabisa sasa unaogopa nini? je angekuficha kesho si ungsepa kabisa
Muache utafute asiye na mtoto,wanawake wa leo kuolewa hamuolewi kwa sababu mnajifanyaga mko sensitive sana tena u sensitivity ambao hauna tija mara nyingi
 
Yaani mpaka hapo hamna mapenzi tena, na mama mkwe nae ni kama hajaridhishwa nawe, ukiolewa huku unawaza kasoro za mtarajiwa we unajipeleka shimoni. Tafakari, chukua hatua
 
Sijui ni shida ya uelewa...
Swala la kuishi na mtoto wa mtu hasa mama yake naye akiwa yu hai, ni suala lenye changamoto. Ukizingatia kuwa mama naye bado anampenda mzazi mwenzake ila kutokana na sababu zisizopingika, haiwezekani wao kuoana.
Mama mkwe kwa upande wake anaona mtoto wa nje anashida na mara nyingi analeta mtafaruku ndani ya nyumba hivyo ni kheri aishi na mama yake maisha yake yote huku baba akiendelea kutekeleza majukumu yake kama kawaida.
Swala la mtoto kuteswa halipo. Ni mara yangu ya kwanza kuingia kwenye hii changamoto ya kuishi na mtoto wa nje. Nilichonacho ni hofu tu kuwa chochote nitakachofanya hakitakuwa chema kwa mtoto.
Nyie mnaokuja na maswala ya mama wa kambo anatesa, mnakariri na kukurupuka. Hamtazami upande wa pili wa shilingi. Kuwa kinachoongelewa si swala la kuteswa wala kutesana bali HOFU INAYOTOKANA NA MIMI KUWA NI MARA YA KWANZA KUISHI NA MTOTO WA KAMBO.
 
Jichunguze mwenyewe, Kama unahisi huna moyo wakulea kisicho cha tumboni mwako basi kataa kuolewa.

Vinginevyo itakusumbua na utapigwa chini tu.
 
mamamkwe wako kakupima tu aone msimamo wako juu ya huyo mtoto . Usiogope mlee vizuri kama mwanao na Mungu atakulinda, na Ndoa yako itadumu .
 
tunaom
Sijui ni shida ya uelewa...
Swala la kuishi na mtoto wa mtu hasa mama yake naye akiwa yu hai, ni suala lenye changamoto. Ukizingatia kuwa mama naye bado anampenda mzazi mwenzake ila kutokana na sababu zisizopingika, haiwezekani wao kuoana.
Mama mkwe kwa upande wake anaona mtoto wa nje anashida na mara nyingi analeta mtafaruku ndani ya nyumba hivyo ni kheri aishi na mama yake maisha yake yote huku baba akiendelea kutekeleza majukumu yake kama kawaida.
Swala la mtoto kuteswa halipo. Ni mara yangu ya kwanza kuingia kwenye hii changamoto ya kuishi na mtoto wa nje. Nilichonacho ni hofu tu kuwa chochote nitakachofanya hakitakuwa chema kwa mtoto.
Nyie mnaokuja na maswala ya mama wa kambo anatesa, mnakariri na kukurupuka. Hamtazami upande wa pili wa shilingi. Kuwa kinachoongelewa si swala la kuteswa wala kutesana bali HOFU INAYOTOKANA NA MIMI KUWA NI MARA YA KWANZA KUISHI NA MTOTO WA KAMBO.
ba mrejesho
 
Kitu chochote unachofikiria kufanya ukishaona nafsi inakataa kwa kuweka viulizo basi ACHA MARA MOJA! Hiyo ni alert umepewa na ulimwengu wa kiroho its better ustopishe hayo mahusiano haraka iwezekanavyo. Hukuumbiwa huyo mtu.
 
Back
Top Bottom