The Donchop
JF-Expert Member
- Jan 10, 2014
- 294
- 378
Habarini wadau wa humu,
Mwenzenu nina shida na ninakuja kwenu nikiwa na matumaini ya kupata ushauri mzuri na unaojenga. Mimi ni mwanamke mwenye miaka 28.
Nina mpenzi ambaye tuko mbioni kutambulishana. Mwenzangu ana mtoto mdogo ambaye alimpata kabla hatujakutana naye.
Mara ya kwanza aliponiambia hilo swala, sikuliweka maanani. Lakini kwa kipindi ambacho tunataka kuwa kitu kimoja, nimeanza kupata mashaka. Mtoto ni mdogo na wala sijawahi hata kukutana naye.
Tatizo nina hofu. Hofu hiyo inatokana na siku nilipokutana na mama mkwe ambaye aliniuliza juu ya kuwa na mume mwenye mtoto.
Mimi nikamjibu kirahisi kuwa ni sawa tu, mtoto hana shida as long as alipatikana kabla hatujakutana naye. Mama mkwe alitoa mawazo yake kuwa kunapokuwa na mtoto wa nje basi familia inakuwa na shida kidogo.
Jambo la pili linalonitia hofu ni kwamba, mimi pia nina ndugu ambaye tulizaliwa kwa baba mmoja. Alilelewa nyumbani toka akiwa mdogo lakini sasa amekuwa mtu ambaye ni ugonjwa kwa familia.
Jambo la tatu ni kwamba, mwenzangu ni mtu wa kutafsiri jambo hata kama jema ataliweka kwenye ubaya. Najiuliza, tutakapoishi na huyu mtoto, chochote nitakachofanya hata kwa uzuri, mwenzangu si atatafsiri vibaya na hapo ndoa itakuwa ndoano. Na ni lazima mtoto aishi naye yeye baba.
Nampenda jamaa lakini hofu yangu ni furaha na amani kwenye ndoa.
Ushauri tafadhali.