Ana miaka 30 ana watoto watatu nje ya ndoa

Nazjaz

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
7,684
8,832
Huyu ndiye mwanaume nimpendae, tatizo ana watoto watatu na hajaoa, na pia anasumbuliwa sana na wanawake wake wa zamani na wanawake wengi wanamtongoza kwenye simu na kila tutokapo out.

Je, nifanyeje ili atulie na awe wangu peke yangu? Na niwafanye nini wanaomtongoza usiku na mchana?
 
mhhhhhh mda ngumu kwa ushauri wangu huyu mwanaume hakufai na hataweza kutiliana ww ameshazoea kula nje na tena sii mwangalifu hatumii condom.unajitafutia headache bure.
 
Kama kutulia basi atatulia mwenyewe. Usikae ukajidanganya eti kuna ambalo waweza kufanya ili atulie na awe wako peke yako.

Kuhusu wanaomtongoza, hakuna la zaidi utakaloweza kufanya. Mwenye uwezo wa kuzuia hilo ni huyo mwanaume na nadhani anajua nini cha kufanya ili hao wanaomtongoza waache.
 
Tatizo liko kwa mtongozwaji anayekubali na sio watongozaji. Hawa usigombane nao. Hao watoto watatu anawalea yeye au wako kwa mama zao? Ana uwezo gani wa kuwapatia matunzo hao pamoja na "family to be? Hapa napaona pagumu kidogo. Unaweza kumdhibiti huyo mwanamume kwa mashauri ya busara lakini kwanza jishauri tena na tena kabla hujaingia kichwa kichwa.
 
Huyu ndiye mwanaume nimpendae, tatizo ana watoto watatu na hajaoa, na pia anasumbuliwa sana na wanawake wake wa zamani na wanawake wengi wanamtongoza kwenye simu na kila tutokapo out. Je nifanyeje ili atulie na awe wangu peke yangu? Na niwafanye nini wanaomtongoza usiku na mchana?
am sorry ila mungu hukupa wa kufanana naye.
 
We jitume tu acha kuangalia ana nani na nani anamfata, ni jukumu lako kumfanya kipofu na kiziwi kila apigiwapo simu na kufwatwa na wasichana. muonyenye upendo, ummjali, usiwe unamuuliza maswali ya kumuudhi, mpikie vizuri kama una nafasi, mahaba mazito mpe nakuaminia mtoto NazJaz
 
duu! Hii ss kal! Utamzuiaje actongozwe? C ajizuie mwnyewe? M2 co mbuz useme utamfnga kmba! Km haja2lia, haja2lia 2 hta ufanyeje! Kupnda kaz kwel, kwel!
 
ndio maana huwa nakuwa siwezi kushauri juu ya uhusiano kati ya watu wawili ....eti niseme huyu sio wako?!!! huwa siwezi maana wanawake ni watu watata sana...anaweza kujiweka kwa mtu yaani hadi ukashangaa..ukijidai kumwambia ....jibu huwa moja tu....mindi your b'ness!!!




 
Naona usipoangalia utajiingiza kwenye foleni ya kuwa mmoja wa wake zake wengi. Unanikumbusha ndugu yangu aliyefikisha umri wa miaka sitini akiwa na watoto 23 aliowazaa na wanawake mbalimbali. Hujivuna kuwataja na kusema ana timu 2 za mpira wa miguu.
 
Huyu atakuwa kabila lililosifiwa sana kwenye thread moja hivi, hongera ila acha wasiwasi umependwa wewe hayo mengine hayakuhusu
 
Back
Top Bottom