Polisi wilayani Bariadi mkoani hapa inamshikilia mwanamke mkazi wa kijiji cha Mwamabu wilayani humo kwa tuhuma za kumnyonga mtoto wake wa kumzaa ili aolewe.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Diwani Athumani, alisema ofisini kwake jana kuwa, Tabu Maimatha mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu ameuawa kikatili kwa kunyongwa na mama yake mzazi, akishirikiana na mpenzi wake, Kijiji Nyamagu ambaye alitoroka baada ya mauaji hayo.
Alimtaja mwanamke huyo kuwa ni Limi Limbu (22) mkazi wa kijiji cha Mwamabu kata ya Bumera na kwamba tukio hilo lilitokea juzi saa saba za mchana kijijini hapo baada ya Limi kurubuniwa na mpenzi wake Nyamagu, kuwa wakimuua mtoto wake wataoana.
Baada ya kukamatwa, Limi alikiri mbele ya polisi kuwa alishirikiana na mpenzi wake huyo kumwua mtoto wake, ili waishi kwa amani na waoane na kuanza maisha mapya katika ndoa yao.
Inadaiwa Limi baada ya kukubaliana na mpenzi wake huyo walifanya kitendo hicho cha kikatili ili kuondokana na bughudha ya mtoto huyo wa nje ya ndoa na hivyo wazae watoto wao wa ndani ya ndoa.
Kweli ulee mimba kwa miezi 9, umzae mtoto, uishi nae mwaka na nusu ukutane tu na lijamaa likushawishi uue mwanao nawe ukubali tu!!! VERY CRUEL, EVIL, STUPID AND CRIMINAL!!!
Nimeshasikia case kama hizi saaan. Na si Tz tu hata nje ya nchi. Sielewi kama wahusika hasa yule ambaye mtoto ni wake wanakuwa kwenye akili timamu au vichaa.
shetani kamzidi akili kiasi cha kujikuta akimtumukia bila ya kujijua.
Naye anastaili adhabu hiyo hiyo iwe fundisho kwa wale wote wazaao na kuua.
Bora amtelekeze na sio kuua. Kapoteza kiongozi mzuri wa kesho. Balaa na zimwandame maisha yake yote na mungu amnyike mtoto maisha yake yote.