Amuua mkewe kwa kumchoma kisu mbarali, mbeya

Amuua mkewe kwa kumchoma kisu mbarali, mbeya

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,335
MWANAMKE mkazi wa kijiji cha Mahango kata ya Madibila wilayani Mbarali mkoani Mbeya aliyefahamika kwa jina la Jitihada Mamga(20) ameuawa kwa kuchomwa kisu na mumewe aliyefahamika kwa jina Gervas Kadaga(25) ambaye pia ni mkazi wa kijijini

[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Gervas Kadaga(25) anaetuhumiwa kumuua mkewe akiwa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"] Mama mkubwa wa Gervas aliyejitambulisha kwa jina la Martha Lugenge alisema kuwa vijana hawa walikutana Madibila kila mmoja akiwa katika shughuli zake ndipo walipoamua kuishi pamoja.

MWANAMKE mkazi wa kijiji cha Mahango kata ya Madibila wilayani Mbarali mkoani Mbeya aliyefahamika kwa jina la Jitihada Mamga(20) ameuawa kwa kuchomwa kisu na mumewe aliyefahamika kwa jina Gervas Kadaga(25) ambaye pia ni mkazi wa kijijini hapo.

Tukio hilo limetokea Novemba 21 majira ya saa 1:00 jioni baada ya kutokea ugomvi baina ya wapenzi hao ambapo marehemu alikutwa na majeraha tisa ya kisu katika sehemu mbalimbali za mwili wake.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Bw. Diwani Athumani alisema kuwa marehemu alifia nyumbani kwake ambapo mtuhumiwa ambaye amelazwa katika hospitali ya Rufaa Mbeya naye amejeruhiwa kwa kuchomwa na kisu tumboni.

Hata hivyo Kamanda Athumani alisema kuwa hadi sasa hakijafahamika chanzo halisi cha ugomvi huo ambapo Jeshi la Polisi linaendelea kufanya uchunguzi wa tukio hilo huku mtuhumiwa akiwa amewekwa chini ya ulinzi wa polisi katika hospitali ya rufaa ya Mbeya alikolazwa.

Akizungumza katika hospitali ya rufaa alikolazwa mama mkubwa wa Gervas aliyejitambulisha kwa jina la Martha Lugenge alisema kuwa vijana hawa walikutana Madibila kila mmoja akiwa katika shughuli zake ndipo walipoamua kuishi pamoja.

Alisema yeye alipewa taarifa za tukio hilo siku inayofuata na kwamba alipofika alikuta ndugu wa marehemu wameuchukua mwili wa mtoto wao kwa ajili ya taratibu za mazishi na kwamba hajui chanzo cha ugomvi uliosababisha wapigane visu.

Mama huyo alisema kuwa vijana hao hawajawahi kupata mtoto na kwamba hawajaanza kuishi pamoja muda mrefu; ''Wote ni watoto, kwani wameanza kuishi muda mrefu? wamekutana kila mmoja akiwa katika kazi zake, ndipo walipoanza kuishi kama mke na mume,''alisema

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
makubwa!!!! Jamani sijui dunia inaenda wapi? R.I.P Jitahada
 
Mmmh, ukihisi umemkosea mpenzi wako hiyo siku hakikisha na wewe umeweka silaha za kutosha kwa ajili ya vita ya mapenzi, la sivyo sepa kabisaaaaaa uokoe roho yako, mapenzi ya sikuhizi ni vita yaani silaha mkononi.

R.i.p marehemu
 
Ugomvi wa kawaida hauwezi kufikia hatua ya kuuana. Ukiona hivyo ujue ni wivu wa mapenzi au kuibiana hela! Na wadada wa siku hizi mnavyopenda hela! Uko tayari kuondoka na mwathirika ili mradi kakuahidi pesa! Loh!
 
hahahaaa....... Kwahiyo hela ni bora kuliko afya sio?

Ujue nini, unaweza kuona ugomvi ni wa kawaida kwako ila usijue mwenzio nae anauchukuliaje, hujui kikomo cha hasira zake.
so, kinga ni bora kuliko tiba, ukihisi umeliboronga JIPANGE!!!!!!
 
Aah hizi hasira jaman...poleni wafiwa..!
 
Mmmh, ukihisi umemkosea mpenzi wako hiyo siku hakikisha na wewe umeweka silaha za kutosha kwa ajili ya vita ya mapenzi, la sivyo sepa kabisaaaaaa uokoe roho yako, mapenzi ya sikuhizi ni vita yaani silaha mkononi.

R.i.p marehemu

tatizo hata ukiandaa silaha hujui atakuvizia wakati gani,
 
Huyu mama anashangaza kusema wote ni watoto. Kweli dunia imebadilika watu wamekosa kabisa uvumilivu.
 
zamani tulikuwa tunasikia mwaka wa chakula, wa njaa, surua sasa mwaka 2013 wa vifo vya mapenzi
 
Mmmh, ukihisi umemkosea mpenzi wako hiyo siku hakikisha na wewe umeweka silaha za kutosha kwa ajili ya vita ya mapenzi, la sivyo sepa kabisaaaaaa uokoe roho yako, mapenzi ya sikuhizi ni vita yaani silaha mkononi.

R.i.p marehemu

unaweza kuwa na silaha mkononi usifanikiwe kutumia ukikosea jitangulize kituo cha police
 
Uwiiii hebu uishe haraka huu mwaka labda utakaokuja utakuwa na stori tamu tamu!
 
ukatili wa kijinsia ukomeshwe,kama mdada amekukwaza mwambie mama njia hiyo nenda kwenu ukapumzike,sasa hapo mkono wa sheria una msubili
 
Mmmh, ukihisi umemkosea mpenzi wako hiyo siku hakikisha na wewe umeweka silaha za kutosha kwa ajili ya vita ya mapenzi, la sivyo sepa kabisaaaaaa uokoe roho yako, mapenzi ya sikuhizi ni vita yaani silaha mkononi.

R.i.p marehemu

Duuuu!!!!!yaani kila kukicha afadhali ya jana
 
Back
Top Bottom