figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,492
- 54,890
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla, amesema nidhamu ya Wanafunzi MBEYA DAY ni mbovu, wakati mwingine wanatoka nje ya darasa Mwalimu akiingia'. Wanaenda kuvutia bangi kule shule ya Msingi Azimio na wakifika huko wanafanya vurugu.
"Sisi kama Serikali tumezama na tunauthibitishia Umma kwamba nidhamu ya wanafunzi wa Mbeya Day katika kidato cha tatu na cha nne ni ya hali ya chini sana. Katika darasa la wanafunzi 50 inaweza ikatokea Mwalimu akafundisha watoto kumi na wengine wanatoka wanapishana na Mwalimu na hawafanyi kitu chochote. Kuna vijana ambao wamekinga ngumi wanataka kupigana na walimu na Walimu wanaona isiwe tabu.
Sasa lazima tufike mahali mimi kama Mzazi na Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama lazima nione kwamba walimu wanatimiza wajibu wao lakini na watoto wetu wawe na malezi ya kuamini kwamba Mwalimu ni mtu ambaye ni kama mzazi wake anampa Elimu, lakini muda mwingi hatukai na hawa watoto kwa Malezi Mazuri.
Kwahiyo niwahakikishie tukio hili limetokea na halitatokea tena lakini pia niwatoe hofu kwamba wanafunzi walimu wanaokuja kwenye Mafunzo waje. Na miminitaendelea kuziangalia shule zote zenye watoto wakorofi kudeal nao kuwarejesha katika nidhamu nzuri wapate malezi na walimu wale watimize wajibu wao.
Hivi karibuni Walimu wa Mafunzo katika Shule ya Mbeya Day walifukuza kazi kazi kwa kile kilichodaiwa ni Video iliyosambaa ikionesha walimu hao wakiwapa adhabu wanafunzi bila kufuata utaratibu.
Habari hiyo ya Mwanafunzi kupigwa, ipo kwenye hii thread=>MBEYA: Walimu warekodiwa Video, wakimfanyia unyama Mwanafunzi