Amos Makalla una sababu ya msingi ya kuendelea kuwa RC Mkoa wa Dar es Salaam?

Yaani tunashindwa kuchunguza na kujua Panya road ni akina nani na wanatokea wapi ili tuchukue hatua?.

Yaani kitengo cha CID jeshi la polisi, na hata task force fulani ya TISS wanashindwa kufanya intelejensia for a week na kukamata wote pamoja na kukata mzizi kabisa?

Yaani vitoto vidogo ndio vinasumbua mijitu tuliyoisomesha kwa hela nyingi nje na ndani na kuwapa majukumu ya kutulinda na kututumikia huku wengine tukifanya kazi kwa bidii kulipa kodi na kujenga nchi halafu yenyewe inakuwa mipumbavu tu.
Hzo sio kazi TISS. Yaan TISS waache kuhangaika na ishu kubwa za usalama wa nchi wahangaike na panya road. Polis ambao ndio walinzi wa mali na raia wanafanya kazi gani?
 
Hao Panya road hapo Kawe huwa wanawakaba hadi askari wa JWTZ. Siku moja askari wamekabwa kesho yake mchana wakaja askari kama 100 wakawa wanapiga kila MTU wanayemuona mitaa hiyo...yaani jamaa miguvu mingi akili kisoda, utapigaje kila MTU njiani tens mchana!!??
 
Hzo sio kazi TISS. Yaan TISS waache kuhangaika na ishu kubwa za usalama wa nchi wahangaike na panya road. Polis ambao ndio walinzi wa mali na raia wanafanya kazi gani?
Usalama wa nchi maana yake nini? Wenye nchi/wananchi wanakatwa mapanga hapo kuna usalama? Vyombo vya ulinzi na usalama huwa vinashea taarifa.
 
Hzo sio kazi TISS. Yaan TISS waache kuhangaika na ishu kubwa za usalama wa nchi wahangaike na panya road. Polis ambao ndio walinzi wa mali na raia wanafanya kazi gani?

Nchi ni ipi? Ishu kubwa ni zipi katika Nchi?
Dar es salaam sio sehemu ya Nchi?

Utofauti wa Polisi na TISS ni upi linapokuja suala la usalama wa wananchi??
 
Juzi kati kulikuwa na tukio Kinyerezi, jana kulikuwa na tukio Kawe na mtu mmoja aliuwawa, leo usiku huko Dovya Temeke watu wamekatwa mapanga mengi sana.

Mhe. Makala una sababu gani ya msingi kuendelea kuwa RC na Mkuu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa mkoa wa Dar es Salaam?
Kwahiyo unataka Makalla ndiyo apambane na vibaka kwa mokno wake? Migwmbo si mnao mitaanj kwenu?
 
Naandika uzi huu kwa masikitiko makubwa.

Mhe. Amos Makala ukiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es salaam.

Huu Mkoa ni kitovu cha biashara kwenye nchi hii, huu mkoa ndio una image kubwa ya nchi kibiashara, wageni zaidi ya 90% wako Dar es salaam.

Pamoja na mambo yote hayo mkoa huu ghafla umegeuka kuwa sio salama kabisa watu wanakatwa mapanga kila siku, hawa vijana wa Panyaroad wanavamia maeneo mbalimbali ya mkoa huu na kuua, kujeruhi, kuiba na kuharibu mali ambazo wananchi wamezitafuta kwa tabu.

Juzi kati kulikuwa na tukio Kinyerezi, jana kulikuwa na tukio Kawe na mtu mmoja aliuwawa, leo usiku huko Dovya Temeke watu wamekatwa mapanga mengi sana.

Mhe. Makala una sababu gani ya msingi kuendelea kuwa RC na Mkuu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa mkoa wa Dar es Salaam?

Unaamka asubuhi unaenda ofisini kwa gari la watanzania, unawekewa mafuta, unalipwa vizuri, unapewa dereva, una PS una jeshi la Polisi, una JWTZ, una TISS, Fire, Magereza, immigration n.k ivi kweli umefeli Mheshimiwa?

Hawa vijana ni mpaka wamuue mwanao wa kumzaa ndio utajua kuna tatizo?

Mpaka wamuu mkeo ndio utajua kuna tatizo mkoani kwako?

Mheshimiwa Makala acha kuongea maneno marahisi, ingia kazini, tumia vyombo ulivyokabidhiwa watu katika mkoa huu hawana amani na wewe upo.

Kama unaona umefeli resign Mzee aje mtu mwingine hapa.

Nadhani huu mkoa upewe RC sawa na wale wenye sifa za ziada waliopo mikoa ya mipakani kama Mtwara, Kigoma n.k

Nawasilisha.
Arudi Makonda uone kama kutakuwa na Panyaroad au Panyamwendokasi!
 
Makonda alimudu kuwaondosha Panyaroad na kurekebisha kero kibaaao mkampiga majungu hadi leo yupo benchi, ona leo mambo yako shaghalagabala DSM.
 
Hzo sio kazi TISS. Yaan TISS waache kuhangaika na ishu kubwa za usalama wa nchi wahangaike na panya road. Polis ambao ndio walinzi wa mali na raia wanafanya kazi gani?
Kwahiyo kazi ya RSO kwenye Mkoa ni kumpigia ngoma RC ili acheze sio? Acha ujuaji kijana!
 
Amos tutamsingizia bure, Hawa vijana wanaojiita PanyaRoad wamekosa ajira hasa pale walipowafukuza wanachinga kufanya biashara maeneo ya mjini, walikosa ajira na namna pekee ya kujipatia kipato na kujiajiri ni hicho wanachokifanya, Serikali ilitakiwa kuwaandalia maeneo na mazingira mazuri ili waweze kufanya biashara na kujipatia kipato, kutumia nguvu sizani kama itakuwa suruhu, watapunguza lakini baadae wataendelea!
 
Back
Top Bottom