Good Father
JF-Expert Member
- Feb 28, 2014
- 10,275
- 18,352
Naandika uzi huu kwa masikitiko makubwa.
Mhe. Amos Makala ukiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es salaam.
Huu Mkoa ni kitovu cha biashara kwenye nchi hii, huu mkoa ndio una image kubwa ya nchi kibiashara, wageni zaidi ya 90% wako Dar es salaam.
Pamoja na mambo yote hayo mkoa huu ghafla umegeuka kuwa sio salama kabisa watu wanakatwa mapanga kila siku, hawa vijana wa Panyaroad wanavamia maeneo mbalimbali ya mkoa huu na kuua, kujeruhi, kuiba na kuharibu mali ambazo wananchi wamezitafuta kwa tabu.
Juzi kati kulikuwa na tukio Kinyerezi, jana kulikuwa na tukio Kawe na mtu mmoja aliuwawa, leo usiku huko Dovya Temeke watu wamekatwa mapanga mengi sana.
Mhe. Makala una sababu gani ya msingi kuendelea kuwa RC na Mkuu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa mkoa wa Dar es Salaam?
Unaamka asubuhi unaenda ofisini kwa gari la watanzania, unawekewa mafuta, unalipwa vizuri, unapewa dereva, una PS una jeshi la Polisi, una JWTZ, una TISS, Fire, Magereza, immigration n.k ivi kweli umefeli Mheshimiwa?
Hawa vijana ni mpaka wamuue mwanao wa kumzaa ndio utajua kuna tatizo?
Mpaka wamuu mkeo ndio utajua kuna tatizo mkoani kwako?
Mheshimiwa Makala acha kuongea maneno marahisi, ingia kazini, tumia vyombo ulivyokabidhiwa watu katika mkoa huu hawana amani na wewe upo.
Kama unaona umefeli resign Mzee aje mtu mwingine hapa.
Nadhani huu mkoa upewe RC sawa na wale wenye sifa za ziada waliopo mikoa ya mipakani kama Mtwara, Kigoma n.k
Nawasilisha.