Amos Makalla ahalalisha "Uchawa", asema ni utamaduni wa kibinadamu wa kushukuru

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
118,605
220,421
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Amos Makalla ametetea machawa wa CCM kwamba ni watu wazuri ambao uchawa wao ni sehemu ya Shukrani.

Zaidi soma hapa

===========

leo Jumanne Mei 7, 2024 akifanya mahojiano maalumu na waandishi na wahariri wa kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) alipotembelea ofisi za kampuni hiyo Tabata Relini jijini Dar es Salaam.

"Utamaduni wa kibinadamu, mtu akifanya vizuri anatakiwa ashukuriwe. Ndicho kinachotokea kwa Rais Samia Suluhu Hassan, kumshukuru, kupongeza ni utamaduni wa kibinadamu, huwezi kuwanyamazisha Watanzania kumshukuru, huwezi kuwaratibu, suala la uchawa huu wa kushukuru hatuwezi kuwafunga midomo wananchi," amesema Makalla.

Hata hivyo, Makalla amesema wanaendelea kuchunguza athari ya suala hilo na atakaa na timu yake kulichunguza kwa kina.

Mwananchi
 
Kuna chawa wengi wa CCM mitaani wanadhulumu ardhi za watu sababu wanamuiga mwenyekiti wao taifa. Mungu atawajibu tu kama Uchawa maana yake ni shukrani au udhalimu.
 
CCM safari hii imepata kiazi kibovu kikweli. Huyu jamaa akidumu hata miezi sita kwenye hiyo nafasi nitashangaa sana. Yaani Akili ya kufikiri na kusema hana.

Uwezo wa kujenga au kujibu hoja hana. Mbinu za kufanya siasa hana. Swaga za kufanya siasa hana.
 
CCM safari hii imepata kiazi kibovu kikweli. Huyu jamaa akidumu hata miezi sita kwenye hiyo nafasi nitashangaa sana. Yaani Akili ya kufikiri na kusema hana.

Uwezo wa kujenga au kujibu hoja hana. Mbinu za kufanya siasa hana. Swaga za kufanya siasa hana.
Anasema kazaliwa Mjini, Babaake alikuwa Polisi Kilwa Road
 
Back
Top Bottom