Amnesty International Siyo Mahakama ya Tanzania

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
945
Amnesty International Siyo Mahakama ya Tanzania

Siku chache baada ya kukamatwa kwa Wakili Boniface Mwabukusi, Mpaluka Nyagali na Dk Wilbroad Slaa, Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro, ameonya mashirika ya kimataifa likiwemo Amnesty International, akiyataka kuacha kuingilia mambo ya nchi za Afrika na badala yake waachie vyombo vya dola vifanye kazi yake.

Waziri Dkt. Ndumbaro amesema hayo Agosti 17, 2023 akizungumza katika kongamano la huduma ya msaada wa kisheria na upatikanaji haki kwa wananchi linalofanyika mkoani Arusha.“Kama wewe unaamini kwamba mtu wa kawaida hawezi kufanya na kupanga uhaini uje mahakamani utoe ushahidi ili wote tukusikie pale ukiongea chini ya kiapo na ukiulizwa maswali yale ya cross examination (maswali ya dodoso)" alisema Waziri Dkt. Ndumbaro na kuongeza

"Amnesty International siyo mahakama ya Tanzania, sisi tuna mahakama zetu na tutaendelea kuziheshimu, kwenye hili tuviache vyombo vya dola vifanye kazi yake."

amnesty-pic.jpg
 
Back
Top Bottom