Amimi .... Usiamini

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,864
155,821
4951106.jpg

Katika hali ambayo hata wanasayansi wameshindwa kuielezea, mwanamke mmoja wa nchini Indonesia mwili wake unaota vipande vya nyaya za chuma badala ya vinyweleo.

Mwanamke huyo anayejulikana kwa jina la Noorsyaidah amekuwa akisumbuliwa na hali hii inayomtesa sana kwa miaka 17 sasa.

Utafiti wa madaktari umeonyesha kuwa nyaya hizo mbali ya kujitokeza kwa nje zipo pia ndani ya mwili wake.

Noorsyaidah mwenye umri wa miaka 42 ni mwalimu wa shule ya chekechea katika kitongoji cha Sangatta katika mji wa Kutai nchini Indonesia.

Hadi sasa hakuna sababu yoyote iuliyotolewa na wanasayansi kuhusiana na hali hiyo zaidi ya kusemekena kuwa ni vijimambo vya UCHAWI.

Ugonjwa wake huo ulianza mwaka 1991 wakati nyaya za chuma zilipojitokeza kwenye kifua chake na tumboni mwake.

Katika wiki yake ya kwanza vipande hivyo vya waya vilinyofoka venyewe toka kwenye mwili wake.

Lakini mwezi mmoja baadae vipande vingine vya nyaya vilijitokeza tena lakini safari hii havikunyofoka na badala yake vilianza kuongezeka urefu. Alipovikata vilijitokeza katika sehemu nyingine ya mwili wake.

Madaktari wataalamu wapatao wanne wameishamfanyia uchunguzi Noorsyaidah kwa njia wanazozijua wao lakini hakuna hata mmoja aliyegundua sababu ya nyaya hizo kujitokeza kwenye mwili wake.

Madaktari walimpiga picha za X-Ray kwenye tumbo lake na waligundua kuwa Noorsyaidah ana jumla ya vipande 40 vya nyaya ndani ya mwili wake ambapo baadhi ya vipande hivyo vimeongezeka urefu na kujitokeza nje ya tumbo lake.

Cha ajabu zaidi ni kwamba vipande hivyo vya nyaya havisambabishii Noorsyaidah ugonjwa wa tetenus.

Noorsyaidah anasema kwamba vipande hivyo vya nyaya vinamsababishia maumivu makali sawa na mtu anayechomwachomwa na sindano.
 
hayo yatakuw mambo ya majini kwa hiyo aulizwe sheikh yahaya wa waislamu atakuwa na majibu mwafaka kabisa au ni lazima atatabiri kitu hapo..........tusubiri

Da.. Hii kiboko, kwa hiyo uchawi wa shehe yahaya wavuka bahari?
hayo yatakuw mambo ya majini kwa hiyo aulizwe sheikh yahaya wa waislamu atakuwa na majibu mwafaka kabisa au ni lazima atatabiri kitu hapo..........tusubiri
 
Kuna medical journal yeyote iliyoverify reports hizi ? Isije kuwa hoax tu.
 
hayo yatakuw mambo ya majini kwa hiyo aulizwe sheikh yahaya wa waislamu atakuwa na majibu mwafaka kabisa au ni lazima atatabiri kitu hapo..........tusubiri

Ingependeza hayo mekundu yasingekuwepo.
 
Back
Top Bottom