Ametembea naa wanawake watatu akitafuta mtoto wa kiume

Ametembea naa wanawake watatu akitafuta mtoto wa kiume

Tatizo jamaa mchovu, mwambie atulize akili, ale chakula bora pia asiwe na msongo wa mawazo.

Awaone madr watamsaidia
 
at the end of the day mtoto ni mtoto tu huo ubaguzi wa watoto ni mbaya sana
Anasema anatafuta wa kiume wa kurithi mali zake kwani wa kike akirithi mali zake zitaenda kwa mwanaume atakaemuoa, anasema hapo ndo panamchanganya.
 
Sex determinant ni mwanaume asihangaike maana mtoto kuzaliwa wakike au wa kiume inategemea mbegu alizo ingiza baba full stop
 
Yeye mwenyewe anatumbukiza mbegu za kike, anategemea zibadilikie tumboni kwa mwanamke? Kinavunwa kilichopandwa. Eti anatafuta mrithi wa mali zake, kwani lini watoto wa kike wamekataa kurithi mali? Kwanza yeye na wenye mtazamo kama wake wasimkufuru Mungu. Kuna watu wanamlilia Mungu awape mtoto yeyote tu hawajapata. Huyo mkewe naye akiamua kutafuta watoto wa kiume nje atajisikiaje? Atatokea kimada mjanja atadakisha mimba isiyomuhusu na bahati itokee azae mtoto wa kiume atamwandikisha mtoto Mali zake zote kumbe mtoto wa kubambikiziwa. Nilishaiona hii kwa ndugu yangu wa karibu kabisa. Mwisho mnatibuana na kimada anakupa live kuwa huna chako hapa sijui waanzaje kurudi kwa mkeo baada ya kumfanyia visa vyote hivyo. Jamani mtoto ni mtoto.
 
Angejua chanzo ni yeye asingehangaika. Mwananume ana mbeyu XY na mwanamke YY. Ili apatikane mtoto wa kiume, wakati viini vinaunga, inabidi itokee kuwa ile X ya mwanaume ndio iungane na Y ya mwanamke. Kama ikitokea mwanaume kutoa Y, basi mtoto anakuwa wa kike.

..watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa..

Mkuu unapotosha umma...kareviev biology vizuri ndio uandike...mwanaume ni XY mke ni XX so anayedetermine jinsia ya mtoto ni mwanaume...
 
Mwambie aendelee kubadili wanawake labda atapata mwenye XY!!!
Mpaka akija kukubali ukweli tayari ana mabint wa kutosha timu ya netball na ma reserve pia! Asiwatelekeze tu!
Ujinga donda la kichwa.
 
Mkuu unapotosha umma...kareviev biology vizuri ndio uandike...mwanaume ni XY mke ni XX so anayedetermine jinsia ya mtoto ni mwanaume...

Ni kweli mkuu kuna mtu tayari kaliona hilo na limewekwa sawa ni XX
 
Pole Sana! Lakini Ni Rahisi Sana ! Ukitaka Ani Pm Ntampa Maelekezo Ataza Hata 4 Mfululizo
 
Watu wanataka kuendeleza ukoo


Sent from my iPad Air using JamiiForums mobile app
 
duuuuuu mi nina midume mitupu natamani ka kike lakini siwezi toka nje ya ndoa
 
Anasema anatafuta wa kiume wa kurithi mali zake kwani wa kike akirithi mali zake zitaenda kwa mwanaume atakaemuoa, anasema hapo ndo panamchanganya.

waswahili bana mali zenyewe ukiuliza ana shamba chanika na bodaboda hata ukiviuza vyote havitoshi kumsomesha huyo mtoto.
 
Back
Top Bottom