Hii ilikuwa miaka kama minne iliyopita tangu nilipokutana na huyu Binti niliyempenda kwa moyo wote, Ilikuwa vigumu kumpata kutokana na msimamo wake. Baada ya mda kama miezi mi3 alikuja kunieleza kuwa kuna mwenzangu na yuko tayari kumuoa na mbaya zaidi anatumia ndugu na jamaa wa Binti ili kumpata kitu ambacho kiliniuma sana ila nilijiaminisha kuwa yeye ni wangu tuu maana ananipenda na Kuna kipindi alinipeleka kwao kama rafiki na wazazi wake walinipokea vzr na pia baadhi ya ndugu walinifahamu ikumbukwe hapo nilikuwa chuo na yeye alishamaliza.
Kipindi cha likizo ndipo aliponipigia simu kuwa hataweza kuwa na mimi tena kwa sababu huyo kijana alituma washenga kwao na wazazi wakawapokea na kuwakubali maana pia walikuwa ni family friends. Huku upande wangu niliumia sana kwa kipindi cha miezi kama mitatu mwisho nikaruhusu ipite. Ila nilienda mpaka kwao na kujaribu kuongea na mama yake mdogo maana mama yake alikuwa mbali na alinijibu mwenye maamuzi ni Binti. Baada ya mda tulianza tena kuchat na bnt ila kumbe huyo mchumba aliona na akanipigia ila nilimjibu kuwa huyo Bnt ni mpenzi wangu, siku moja mama wa Bnt akanipigia nikamueleza ukweli akaniambia nipotezee.
Nilimaliza chuo na kupata kazi nzuri ya fani yangu na maisha yamenyooka ndio juzi tukaonana instagram Binti amechoka maana majukumu yote kaachiwa yeye na mshahara wake mdogo ndio kuniomba msaada kodi imeisha na hana hela na hapo alibakiwa na 500 tuu, ukweli nilimpa pesa za kuongezea kodi. Ikawa ni kama tulianza kukumbushia ya nyuma na Bnt akapanga kuja kwangu ila nilimchenga kuwa nasafiri nje nikirudi ntamuambia. Sasa anataka amtoroke mume wake tena wa ndoa na nimemuuliza atawezaje?? Anasema kuwa kwanza hampendi na hata huyo kaka anajua kuwa alimforce kwa kuwalaghai wazazi wake na mpk Bnt kutaka kutengwa kama asingeolewa nae pili ni mtu mzima sana na hafurahii kuwa nae, now wazazi wanajuta kwanini walifanya yale maamuzi.. na nashindwa kuelewa maana anaweza kupiga simu usiku kabisa au kuchat usiku akitumia maneno magumu. Ila ugumu hapa ni ndoa aliyonayo nahisi nikiwa na mahusiano nae ntakuwa na makosa japo ameniomba sana kuwa atafanya awezalo ila nisimuache na mimi moyo unampenda pia.
Ikumbukwe huyu kaka alinichukulia mtu niliyempenda mno na kuniacha na jeraha ila sasa Bnt anataka kurudi.