Wacha uongo wewe, Zanzibar unaijua weye?CUF wamtumie ujumbe huyo mshauri wa Obama. Hali Zanzibar ni mbaya kuliko Kenya!
aah! nadhani wasilete Tanzania kitu kama hiki, wasiwasi wangu ni hawa akina Ponda na kundi la waislam wenzake wenye msimamo kama wake. Naomba radhi kwa waislam, hapa sisemi juu ya waislam wote ndo maana nataja jina la Ponda. Ninamaanisha lile kundi lenye msimamo wa boko haram. Kundi hilo linaushawishi mkubwa sana na siku zote linatafuta sababu ya kuifanya Tanzania ikosane na USA au mataifa ya magharibi.
.
hii kitu wailete tu TZ if that's what it takes kuwashikisha adabu mafisadi, udini sio kitu, kama mjaluo live ameweza kuipeleka Kenya kwenye ukabila, hata hapa itafaa tu...kwenye hiyo list ya wakosa visa na wakristu si watakuwapo ndani? kama hiyo hapo juu isivyochagua kabila
Hakuna. Ila ndio "Israel" ya Marekani kwenye ukanda huu.Kenya kuna oil?
Huyu Michuki si yuko kwenye list ya waliopigwa marufuku kukanyaga marekani? vp tena??
Odinga, Michuki and World Bank Director Zoeller
Matatizo yao ni UFISADI au vurugu zilizoambatana na mauaji baada ya uchaguzi mkuu wa KENYA? Mbona kamwacha Raila, kinara wa yote haya?
Huyu Michuki si yuko kwenye list ya waliopigwa marufuku kukanyaga marekani? vp tena??
Hebu fikiria kama angekubali kushindwa mapema kabla ya alivyofanya baadae. Asingekufa mtu. Watu wamekufa, kapewa Uwaziri Mkuu bandia na magari ya ving'ora basi hadi 2012.Hivi kinara wa haya Mauaji ni Raila? au ni Kibaki aliyejitangazia Ushindi mwenyewe!!
Dah! amefariki! yaani huyu mtu tunafahamiana uzuri,Mungu amuweke mahali pema. kama ndio huyo ninayekusudia anaitwa Bw Msaki,ni huyu mkuuau ?Kabla Marekani hawajaileta Tanzania, si na sisi tuanze ili kutekeleza ule msemo Charity begins at home?? Kwa kuwa serikali yetu inawakumbatia mafisadi na haitaki kuwapa ban. Bas sisi tuanze kwa kutoshirki biashara zao. Tususie kununua bidhaa na huduma zote za mafisadi. Ni nani ajitokeze kuelezea hayo?? Ila akubali kuwa maisha yake yatakuwa mafupi, japo si kwa bomu la mhanga but ni kujitoa mhanga???
Hivi mnafahamu yule suspect wa Benki ya NBC aliyetuhumiwa kuwa alitoa zile account za mafisadi na akafukuzwa kazi alifariki tarehe 11/9/2009 na kuzikwa tarehe 15/9/2009?? Alipata maradhi ya kutatanisha?? na umauti ukamfika!!! Pengine nitaanzisha tread yake ili mwenye lolote kuhusu marehemu huyu shujaa achangie (jina nimelihifadhi kwa sasa). Rest in Peace.
Hivi kinara wa haya Mauaji ni Raila? au ni Kibaki aliyejitangazia Ushindi mwenyewe!!
Dah ukabila hatari sana kama udini sasa hawa jamaa dah naona walikosea sana kudharau Kiswahili kuwa lugha ya Taifa lao na wangekipa kipau mbele makabila yote yangeunganika lakini mmh!
Ab- Titchaz,
Hauwezi kumwondoa Raila kwenye sakata hili kwa sababu zifuatazo:
1. Aliyakataa matokeo yale ya Uchaguzi kabla hata hayajatangazwa.
2. Alikuwa na uwezo na ushawishi mkubwa kuwatuliza wafuasi wake.
3.Baada ya watu kuuwawa kakubali usuluhishi, kwa nini sio kabla?