Amepiteza ramani ya maisha, je tunamsaidiaje?

Amepiteza ramani ya maisha, je tunamsaidiaje?

Hapo cha kumsaidia ni yeye kama yeye kutafuta namna ya kuyamudu maisha mwambie ajishughulishe hata kubeba zege kwa muda huku akiwa na malengo yake maalum sababu ndio alishakosea tayari kuchagua aina ya marafiki pamoja na mke aliyekuwa naye.

Siku zote matatizo ndio kipimo cha kujua mioyo ya watu wakaribu wanaokuzungua nje ya hapo ni ngumu sana aiseee. Pole kwake.
Exactly
 
Sitaki kuamini hyo kijana akili yake ilikua kwenye vyeti tu..hivi unaanzaje poteza dira ya maisha kisa tu kukosa kazi!..aache masihara mbona kuna vibarua vingi tu atafute vibarua afanye kupoteza dira ni marufuku kwa binadamu mwenye mikono na akili
 
Mwambie asikate tamaa amshukuru Mungu ana Nyumba, wewe ukiwa kama mtu wake wa karibu unatakiwa uwe wa kwanza kumfariji na kama una jinsi yoyote ya kumsaidia unaweza kumsaidia, amtangulize Mungu kwa maombi maana Mungu hufungua njia pasipo na njia.
 
Alikuwa anafanya kazi serikalini, akakumbwa Na ishu ya vyeti feki akaondolewa kazini.
Alikuwa amebahatika kujenga nyumba Boko, Ila ndio hivyo tena mke kamkimbia Na kwenda kuanza maisha yake baada ya maisha kuwa magumu.
Hana dira Wala mwelekeo, marafiki zake wote wamemkimbia, wanamcheka na kumsema vibaya.
Je mtu huyu tumsaidie vipi?
aliwahi kusema Haris Kapinga "kitu chochote ambacho hakijatoa uhai wako ni changamoto, kudaiwa ni changamoto, kuachwa ni changamoto,kufukuzwa kazi ni changamoto so pamabana na vita kuimarisha."
 
Mwambie apangishe vyumba viwili ili apate pesa ya kujikimu, halafu aendelee kutafuta Mishe atapata tu asikate tamaa.
 

Unapokuwa kwenye nafasi/kitengo kumbuka kuna siku zinakuja hautakua kwenye hiyo nafasi, utawahitaji watu. Ndio maana huyo karani muuza duka akaona awapunguzie madeni wadaiwa wawe msaada huko mtaani.
 
Mwambie aniuzie nyumba ya huko boko Ili apate mtaji afanye biashara.
 
Mkuu huyo jamaa hakua na akiba yoyote benki.?

Kama mke kamkimbia si ashukuru walau mzigo umepungua wa kulisha familia. Cha msingi ni ajipange upya ajue kinachofuata. Kama marafiki wamemuacha ashukuru pia ameweza kutambua ni aina gani ya watu alikua amezungukwa nao. Tunawaacha wangapi.? Tutawaliliwa na wangapi.? Na sisi pia tunaachwa na wangapi.? Tutawalilia wangapi.? Aanze tu kutengeneza marafiki wengine. Ndivyo maisha yalivyo.

"Do not pain for those left you, use pain to earn success that define you"
unajua maisha halisi ya asilimia kubwa ya wafanyakazi serikalini huwezi kuwa na akiba ya kutumia miezi mbele...
 
Bado hiyo haijanishawishi niseme amepoteza raman ya maisha.

Nina amini Elimu haipo kwenye Vyeti ,Kua naelimu ni kutumia ulichonacho kichwan nakukionyesha waziwazi.

Analalama na wakati mahali fulan kuna mtu kafukuzwa kazi ,nahana nyumba nambaya zaid ana ngoma ,lkn bado kaamua kuikubali hali.?.

Mdau mmoja humu JF aliwah toa uzi wa kusimamishwa kazi ..na jamaa alionyesha kabisa kukubaliana naiyo changamoto sasa nikusonga mbele.

Sasa jamaa wako sindo akigundua anakisukari sindo ataamua nakujiua??

Aache masiala.
Huyo jamaa wa jf namkumbuka, ila yeye nilivyoona ni kama alikua amesha sense hilo jambo lingetokea, inshot alikua amejiandaa na hali halisi!!

Ila hata huyu si ana nyumba? Na yeye ana pa kuanzia... Akomae tu!!
 
Pole zake. Maisha lazima yaende mbele. Kama anaweza achukue hatua zifuatazo.
1. Ahame kwenye nyumba yake (akapange chumba kimoja cha elfu 30-50, auze baadhi ya fanicha ili aweze kufit kwenye chumba kimoja. Mambo sijui ya makochi, makabati nk apige bei) aweke mpangaji. Kama nyumba ina ubora anaweza akawa anapata kati ya laki mbili hadi tatu kwa mwezi. Hazimtoshi kula hizo?
2. Kiasi kidogo cha pesa atakachopata kwa kuuza fanicha, afungue kibanda cha M pesa. Akiwa na mtaji wa laki tano, kwa kuuzungusha zungusha sehemu busy kama kwenye stendi za dala dala, masoko nk hawezi kukosa laki moja na nusu nyingine.
Akijumlisha na ile kodi ya nyumba angalau kwa mwezi anaweza akajikuta anakusanya laki nne mpaka tano NET, na huenda akakusanya zaidi. Hali ikiendelea hivi anaweza akajikuta ameshakuwa mfanya biashara mkubwa tu siku za usoni na akajuta kuwa kwa nini alikuwa anapoteza muda kwenye kuajiriwa!
 
kama ameweza kuja kukwambia hayo....bado hajapoteza ramani....msaidie huyo.....
 
Duuuuu.....members wengi wanachangia kirahisi rahisi sana, I believe they just don't understand the situation labda sababu wengi wapo kwenye nyakati zao bora za maisha.

Mimi cha kumshauri ni hiki hapa. Afanye afanyavyo by hooks and crooks apate pahala pa kujishikiza walau kujitibu kisaikolojia. Pahala anakoweza kupata visenti kidogo.

Acheki kwa washkaji, ndugu ama jamaa. La, kwa hapa mjini afanye dei waka za hapa na pale, la hata popote pa kujitolea ili mradi awe involved na shughuli za kiuchumi.

Soon, atakuwa sawa na kuanza kuchora ramani yake kwa utulivu mzuri zaidi. Kipindi hiki 'KUJITUMA' kwa chochote ndio msaada wake mkubwa.

Mpe pole sana.
 
Atulie achore nyingine, ukianguka unasimama tena unajipanga unaendelea na safari
 
Back
Top Bottom