Amepiteza ramani ya maisha, je tunamsaidiaje?

Amepiteza ramani ya maisha, je tunamsaidiaje?

Heci

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Posts
3,867
Reaction score
6,881
Alikuwa anafanya kazi serikalini, akakumbwa Na ishu ya vyeti feki akaondolewa kazini.
Alikuwa amebahatika kujenga nyumba Boko, Ila ndio hivyo tena mke kamkimbia Na kwenda kuanza maisha yake baada ya maisha kuwa magumu.
Hana dira Wala mwelekeo, marafiki zake wote wamemkimbia, wanamcheka na kumsema vibaya.
Je mtu huyu tumsaidie vipi?
 
Moderator, typing error, naomba
heading isomeke amepoteza ramani ya maisha badala ya amepitiza
 
Aliyepoteza raman ya maisha ni mfu tu na wafu wote wamezikwa.

Mwambie ajifunze kuyaishi maisha na mambo yake vile yanavyokuja mbele yake.
Hata hela ya kula kwake imekuwa shida, hata nauli ya daladala haiwezi tena
 
Mkuu huyo jamaa hakua na akiba yoyote benki.?

Kama mke kamkimbia si ashukuru walau mzigo umepungua wa kulisha familia. Cha msingi ni ajipange upya ajue kinachofuata. Kama marafiki wamemuacha ashukuru pia ameweza kutambua ni aina gani ya watu alikua amezungukwa nao. Tunawaacha wangapi.? Tutawaliliwa na wangapi.? Na sisi pia tunaachwa na wangapi.? Tutawalilia wangapi.? Aanze tu kutengeneza marafiki wengine. Ndivyo maisha yalivyo.

"Do not pain for those left you, use pain to earn success that define you"
 
Amekata tamaa mapema bado ana nafasi ya kuishi apambane ukikata tamaa hata akili inagoma kufikiri zaidi
 
Hapo inabidi kwanza akubali situation, kwamba hali imebadilika, hela zimekata, mke kamkimbia, hakuna namna ni kujipanga tu upya ndo ataweza kufanya hata kazi ya zege, otherwise msongo wa mawazo utammaliza
 
Hyo labda kama alikuwa na anasa kuna watu wamemaliza vyuo hawaja wahi onja hata mshahara hata nyumba yenyewe sidhan kama IMO kwenye fikra zao alafu wewe unasema kapoteza dira hyo aje tuungane tu kubrash viatu vya walio maofisini
 
Hapo cha kumsaidia ni yeye kama yeye kutafuta namna ya kuyamudu maisha mwambie ajishughulishe hata kubeba zege kwa muda huku akiwa na malengo yake maalum sababu ndio alishakosea tayari kuchagua aina ya marafiki pamoja na mke aliyekuwa naye.

Siku zote matatizo ndio kipimo cha kujua mioyo ya watu wakaribu wanaokuzungua nje ya hapo ni ngumu sana aiseee. Pole kwake.
 
Hata hela ya kula kwake imekuwa shida, hata nauli ya daladala haiwezi tena
Bado hiyo haijanishawishi niseme amepoteza raman ya maisha.

Nina amini Elimu haipo kwenye Vyeti ,Kua naelimu ni kutumia ulichonacho kichwan nakukionyesha waziwazi.

Analalama na wakati mahali fulan kuna mtu kafukuzwa kazi ,nahana nyumba nambaya zaid ana ngoma ,lkn bado kaamua kuikubali hali.?.

Mdau mmoja humu JF aliwah toa uzi wa kusimamishwa kazi ..na jamaa alionyesha kabisa kukubaliana naiyo changamoto sasa nikusonga mbele.

Sasa jamaa wako sindo akigundua anakisukari sindo ataamua nakujiua??

Aache masiala.
 
Ashukuru Mungu hata hapo pa kulala anapo,wengine ma dish yameyumba kwelikweli huku kitaa,watoto na familia zinawakodolea,mbaya zaidi maisha chumba sebule cha kupanga.
 
Hapo inabidi kwanza akubali situation, kwamba hali imebadilika, hela zimekata, mke kamkimbia, hakuna namna ni kujipanga tu upya ndo ataweza kufanya hata kazi ya zege, otherwise msongo wa mawazo utammaliza
Kweli kabisa best na mie nilijikuta naiwaza hiyo hiyo afanye tu kwa lengo la kujipanga upya na sio kusikiliza watu watasema nini juu yake.
 
Alikuwa anafanya kazi serikalini, akakumbwa Na ishu ya vyeti feki akaondolewa kazini.
Alikuwa amebahatika kujenga nyumba Boko, Ila ndio hivyo tena mke kamkimbia Na kwenda kuanza maisha yake baada ya maisha kuwa magumu.
Hana dira Wala mwelekeo, marafiki zake wote wamemkimbia, wanamcheka na kumsema vibaya.
Je mtu huyu tumsaidie vipi?
Mchukue nenda nae mkatembelee wagonjwa Muhimbili, katembeleeni wafungwa Segerea na Ukonga,tembeleeni huku kwetu kwa Mtogole muone tunavyoishi,tembeeni barabara nyingi muone omba omba na vilema wanavyopambana na maisha bila kukata tamaa.
 
Kufukuzwa kazi sjui kukimbiwa na mke hayo hayawezi kukufanya maisha yasiendelee.Maisha yako pale pale na akipambana atafanikiwa kuliko hata waliobaki kwenye ajira.
 
Alikuwa anafanya kazi serikalini, akakumbwa Na ishu ya vyeti feki akaondolewa kazini.
Alikuwa amebahatika kujenga nyumba Boko, Ila ndio hivyo tena mke kamkimbia Na kwenda kuanza maisha yake baada ya maisha kuwa magumu.
Hana dira Wala mwelekeo, marafiki zake wote wamemkimbia, wanamcheka na kumsema vibaya.
Je mtu huyu tumsaidie vipi?
Cha maana hapa kwanza ajikubali katika halo aliyonayo kimaisha,halafu angalie jinsi ya kujikimu kimaisha,kuvunjika kwa koleo sio mwisho wa uhunzi,jipange fikiria cha kufanya ambacho kitakusidia kupata msosi wa siku ,vingine taratibu utaviangalia mwelekeo .Usikate tamaaa mapema wakati jalali kakupa pumzi,jitume acha kuna aibu jikubali halo ulipo
 
Kweli anaweza akawa amepata mfadhaiko kidogo wa maisha kubadilika lakini hiyo isimfanye akate tamaa ya maisha.

Mwanaume hujikwaa na kuamka, unaweza kumsaidia kwa kumfariji na aanze kutafuta kibarua chochote cha kumuingizia riziki
Kukata tamaa ni udhaifu mbaya sana
 
Embu mwambie aache utani aisee..mtu unanyumba tayari na unasema umepoteza ramani ya maisha..je angekuwa amepanga je??

Atafute kazi ndogo ya kuweza kupata mahitaji madogo madogo,huku akiendelea kutafuta namna nyingine
 
Back
Top Bottom