ladyfurahia
JF-Expert Member
- May 10, 2011
- 14,758
- 9,589
Hakupendi,
Anataka aendelee kukumega kirahisi rahisi tu,
Piga chini jipange upya.
Unamlilia mtu ambaye hakupendi?
Wana mmu habari,
Yamenikuta mie. Boyfrend wangu anatakiwa kuoa mchaga mwenzake na mie sio mchaga yaani ni sheeeeda!!!
Mchumba kapatikana uchagani na proces zote ananijulisha. Ingawa anaoa hataki tuachane. Duh! Mazito ndugu zangu. Nipen ushauri au ata pole yatosha
Fanya mpango wa kubadilisha kabila chap chap...
Watu siku hizi wanabadili hadi jinsia, nini kabila...
^^
Pole
^^
Karibu sana kwenye ulimwengu wa Dilemma.
Tafuta wako mapema kabla hujagonga 30's.
achana nae la sivyo utaendelea kuuumia sana
Pole, lakini haitoshi. Huyo jamaa yako hana akili nzuri, keshakupotezea muda sasa anataka kukufanya kasmall hse! Aisee hada adabu kabisa.
Hebu komaza akili achana naye, wanaume tupo wengi; ni wewe utulie tu.
mnafki huyo,anataka akufariji ukubali matokeo halafu aendelee kukutafuna,kashakuambia kata mawasiliano mazima,angejua umuhimu wako asingelazimishwa kuoa mchaga mwenzake,hicho kisingizio tu katafuta.Kama unajielewa achana naye tu.
Katafuta njia ya kidplomasia kukumwaga.
Kwa kifupi, kwake wewe ulikuwa wa kuuzia sura kitaa, ila si wa kuoa. Keshapata wife material wake, kwako anataka abaki na copyright za kuchemsha kiporo.
Stuka!
Yeye anaoa afu hataki muachane. Is he serious? Limeshatokea, kubali kuwa huyo si wako tena, utampata wa kwako ambaye Mungu amekuchagulia. U don't deserve to be mchepuko wa mtu. Pole sana
Kwa wachaga mke ni "family property".....kwa vyovyote wewe usingekubalika kwao.....achana nae...fastaaaa
Ndio!
mwanamke akishafika 30 ujue ni majanga! ni bora muambiwe mapema kabla maji hayajamwagika!
Kama hana cha kufanya, basi ni bora afanye moja la kueleweka!
queenlishas hebu funguka dada wababa wa humu nao tuone kama tunaweza kujibeba! lol
pole mdada hata mimi imenitokea sahv nimeamua nitulize akili tu mungu atatenda yake
We dada kaza moyo fanya maamuzi magumu huyo jamaa achana nae no matter moyo wako bado unamtaka ila onyesha ukomavu wako kimsimamo muache ufanye yako baada ya muda utasahau na utapata mchumba mwingine.
Pole weeh...unatia huruma..kiukweli hilo lilikua ni jaribu na hakuwa wako plz let it go..huezi jua mungu amekuandalia nini mbeleni..pole sana
NIKIWA KAMA MUATHIRIKA WA MOJA KWA MOJA KAULI YAKO HII...
TAFADHALI NAOMBA UTUTAKE RADHI "WACHAGA WOTE" KUANZIA TULIOKUWA HAPA JF MPAKA WALE WALIOKO MOSHI WAKIANDAA KINYWAJI CHETU MAARUFU, WALIOKO PEMBA NA UNGUJA WAKIUZA BIA NA K,MOTO...WALIOKO NJE YA NCHI NA HASA USA SHIRIKA LA NASA WAKIRUSHA SATELITES NA WENGINEO WENGI WALIO-OLEWA NA KUOA WACHAGA....
SITANII..TAFADHALI NJOO UFUTE KAULI HII MAANA IMEJAA "MITUSI MIZITOMIZITO"...KWA TAFSIRI YA HARAKA NAWEZA KULIA.....NJOO BANA ...WAHI AISEEEE.....UJUWE UNACHELEWA....
ACHA UBAGUZI NA GENERALIZATION PRINCIPLE.....MKUBWA SASA WEWE YAKUPASA KUTAFAKARI KABLA HUJAANDIKA.
ni hayo tuu..atleast for now i do care.