Amenichosha: Nisaidieni software za kuhackle simu yake

Jaman mimi ninampenzi lakini hatakai kabisa niguse simu yake! yaani namtunza kweli na kumpa kila anachotaka lakini yeye inaonekana anamtu mwingine! N

WATAALAMU WA IT, NAOMBA SOFTWARE YA KUHACKLE SIMU YAKE NIZISOME MESSEJI ZAKE KWA MBALI TUMALIZANE NA HUYU

Ya nini yote ndugu yangu utaumiza moyo wako bure kama umuamini muache
 
Lakini naona ipo clear, kama hana dem mwingine ungekuwa huru na simu yake labda jambazi
 
cha muhimu ww nunua simu mbili zinazofanana!afu mshawish atumie simu uliyompa!makusudically badilishaneni simu!haitafika saa 4asbh bila ya upupu kumwagika!very easy
 
Dah, hivi kuna sababu yoyote ya msingi ya kupasuka Moyo/nyoyo nyakati hizi? Ni kujifunza tu na kuamua, nampenda naweza kwenda nae twende, Siwezi kaa pembeni kwa gharama kidogo ya muda wa kumsahau. Maisha yaendelee kwa furaha.
 
Nimeamini JF kuna great thinkers! Kwa sisi FBI tunazidi kuongeza maujuzi! Thanks guys. Hata Mungu anamsaidia anayejisaidia. Kama nyie mme relax amchungi mizigo yenu tuachieni wazoefu wa ku protect.
 
Jaman mimi ninampenzi lakini hatakai kabisa niguse simu yake! yaani namtunza kweli na kumpa kila anachotaka lakini yeye inaonekana anamtu mwingine! N

WATAALAMU WA IT, NAOMBA SOFTWARE YA KUHACKLE SIMU YAKE NIZISOME MESSEJI ZAKE KWA MBALI TUMALIZANE NA HUYU

yaani huu msemo wa akina dada ati NINAMPA KILA ANACHOTAKA yaani mi huwa sielewi elewi unamaanasha mambo yapi hasa, huwa najiuliza maswali yasiyo na majibu, nieleweshe kiduchu tafadhali. Lol
 
kwa unavyoonekana sio tu ku hack simu, bali hata ukimuona live haitasaidia kitu. weye unaonekana umegandishwa ki mtindo. kila mtu anakushauri hakuna umuhimu wa kuhack weye baaaado umeshikilia tuu. ni mbishi mno weye.
hata hivyo uwe pole
 
Yanini malumbano,ya nini maneno,jiweke pembeni kuepusha msongamano!
 
Jaman mimi ninampenzi lakini hatakai kabisa niguse simu yake! yaani namtunza kweli na kumpa kila anachotaka lakini yeye inaonekana anamtu mwingine! N

WATAALAMU WA IT, NAOMBA SOFTWARE YA KUHACKLE SIMU YAKE NIZISOME MESSEJI ZAKE KWA MBALI TUMALIZANE NA HUYU

kuna software inauzwa, inaitwa mobile manager pro, inaweza kufanya hayo unayotaka. Lakini angalia usije ukafanya kitu cha ajabu. Authorized dealers hapa East africa wanaitwa DynaTechAfrica.com.
 
Unampa kila kitu na unaji express au kila kitu kama nini? kama umetoa pole we, mie sioni umuhimu wa kwenda mbali kote huko, upoteze muda wako bure, angekuwa mumeo unataka talaka hapo sawa lakini bwana tu mpaka utafute ma software looooo mbona una thamani zaidi ya hayo?
hahahah kujiexpress sku hz muhimu ww lasivyo unaachwa
 
Dah, hivi kuna sababu yoyote ya msingi ya kupasuka Moyo/nyoyo nyakati hizi? Ni kujifunza tu na kuamua, nampenda naweza kwenda nae twende, Siwezi kaa pembeni kwa gharama kidogo ya muda wa kumsahau. Maisha yaendelee kwa furaha.
:confused2::confused2::confused2::confused2::confused2:
 
Jaman mimi ninampenzi lakini hatakai kabisa niguse simu yake! yaani namtunza kweli na kumpa kila anachotaka lakini yeye inaonekana anamtu mwingine! N

WATAALAMU WA IT, NAOMBA SOFTWARE YA KUHACKLE SIMU YAKE NIZISOME MESSEJI ZAKE KWA MBALI TUMALIZANE NA HUYU

Simu ya mpenzi wako unaitakia nini?

Ile ni mali yake binafsi na ana uhuru wa kuitumia atakavyo!
 
shida yote ya nini kama anacheat mmwage, kama unaona anakupa mateso ya moyo badala ya faraja tupa kule,uki-hack cm yake ukakuta mayb yupo na mahusiano na watu zaidi ya watatu,halafu wewe kakusave 'nyau' kwenye phone book utafanyaje? Maumivu mengine ni ya kuepukika

Anataka ku-make an informed decision based on fact na sio assumptions:)
 
Anataka ku-make an informed decision based on fact na sio assumptions:)
huyu anataka kuumiza moyo wake. Jamb keshaweka password, yaani kusoma hujui hata picha huelewi? Je penzi limechuja? Amebadilika? Hamheshimu? Kama majibu ni hapana aachane na mapaswrd!

Mwenyewe keshasema anataka kujua tu hayupo tayari kumuacha! Thats gud,sasa kama akigundua kuwa wako zaidi ya mmoja atafanya nini? Kama c kutafuta maumivu ambayo yanaepukika.

N what if ameweka paswrd kwa sababu kuna siri labda za ofsn hataki zijulikane,na yy akazichimbua huko? Ukimchunguza sana bata huwezi kumla. Ni vyema angevunja ukimya wakazungumza na mumewe kero zake kumaliza sarakasi za moyo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom