Ameniambia tufunge ndoa kabla ya Ramadhani

Mributz

Senior Member
Aug 29, 2022
112
388
Habarini

Nimeishi na uyu bint sasa ni miaka 3 . Amekomalia sana ndoa ramadhani hii kasema lazima tufunge ndo
Wote sisi ni waislam

Mimi mfukoni apa nna laki 3 tu. Wazazi wetu wako mbali na sisi yeye anasema inawezekana bila ya ndugu na ndoa inakuwa safi.

Wataalamu, ma sheikh ushauri wenu
 
We kumbe ni Muislam alafu unaishi na mwanamke (sio mke) kinyumba na bado unashauriwa na mwenzio msiendelee kuzini wewe unashupaza shingo kuja kwenye mitandao ya kijamii kuomba ushauri.

Hebu timiza matakwa ya dini yako, km hutaki muache huyo mtoto wa watu usiendelee kumtia matatizoni siku ya kiama akakosa Cha kujibu.
 
Kikosi cha kataa ndoa ndio wamshauri vizuri kwa unavodhani?
Hawawezi kumshauri vizuri lakini hai-make sense mtu umekaa nae miaka 3 anakushauri mfunge ndoa kihalali unasita unaona ni mtego.

Hapo binti anatimiza majukumu yake kama mke lakini hatambuliki kama mke...hakuna maana ya kuishi pamoja basi.
 
Funga ndoa nae

Muislam unaogopaje ndoa huku umeruhusiwa kuoa mara 4.

Funga ndoa akibadilika kuleta mawenge unapiga talaka na kuoa mwingine.

Ama unampandisha cheo anakuwa mke mkubwa
 
Habarini

Nimeishi na uyu bint sasa ni miaka 3 . Amekomalia sana ndoa ramadhani hii kasema lazima tufunge ndo
Wote sisi ni waislam...
Ushauri wa kwanza wote mnatakiwa mjutie na mtubie kwa muda wote mliokuwa mnaishi kinyumba bila ndoa.

Cha pili ndoa ya waislamu haina mambo mengi hata kuwa laki Moja inaweza kufanikisha shighuli nzima malahi ndogo unaweza usilipe yote kwa kuanzia ,sherehe unawaalika watu wachache muhimu inaiisha chap muhimu ndoa kupita.

Mimi hapa ndugu yangu alipata mchumba Zanzibar ndoa ikafungwa hapa Dar ikatumia elfu hamsini tu hawakuzidi watu 20 waliohudhuria ni simple tu wakaondoka kuendelea na maisha yao ya ndoa .

Nb:Kumbuka kufuata taratibu zote za ndoa.

0b00425b3942452ead3511a50a32865a.jpg
 
We kumbe ni Muislam alafu unaishi na mwanamke (sio mke) kinyumba na bado unashauriwa na mwenzio msiendelee kuzini wewe unashupaza shingo kuja kwenye mitandao ya kijamii kuomba ushauri. Ebu timiza matakwa ya dini yako, km hutaki muache huyo mtoto wa watu usiendelee kumtia matatizoni siku ya kiama akakosa Cha kujibu.
Atakosaje Cha kujibu. Si alikuwa Kwa jamaa Wana pasha viporo Kila uchwao Kwa miaka hiyo.
 
Ulitakiwa umshauri mwenzio amrudishe binti wa watu kwao mpaka pale atakapokuwa tayari kuoa . Binti hataki uzinzi
miaka mitatu ndo leo akomalie ndoa asingekuwa anataka uzinzi ndani ya mwaka mmoja angekomalia ndoa.inaonesha wote wazinzi anaekomalia ndoa na anaekataa ndoa
 
Back
Top Bottom