Ameniacha eti sijui ku-care

kindikwili

JF-Expert Member
Oct 5, 2016
1,862
2,872
Umofia kwenu wana jukwaa!

Wadada badilikeni na jifunzeni kujua hakuna mwanaume aliyekamilika, msijifanye too complex kuliko uhalisia, acheni kuiga uzungu. Kuna binti nikiwa form six yeye alikuwa five shule moja huko Kilimanjaro. Tukiwa kule shule sikuwahi kuongea naye labda salamu kwa nadra, nilipomaliza zangu chuo huko Moro nikarudi zangu mjini wakati huo yeye akiwa DUCE basi tukaingia kwenye mahusiano.

Kiufupi tulikuwa kwenye hali ya juu sana ya mapenzi nilimpenda sana yule binti na mwenyewe niliona napendwa. Bahati mbaya naona alizidisha hulka ya uzungu kwenye kitu kinaitwa CARE. Alitaka kila wakati niwe nafanya mambo ambayo mwenyewe yangempa uhakika kwamba nacare. Sijui yeye alidefine vipi neno kucare maana nilifanya mengi ila hakuridhika. Basi hatimaye tuliachana anatafuta mtu anayejua kucare.

Lakini si mimi tu yuko rafiki yangu wa karibu jamaa wa Kilimanjaro huko naye alikuwa na demu wake hapa mjini , basi demu kila wakati anataka apigiwe simu, akiomba hela apewe immediately, akisema anaumwa anataka jamaa afike haraka iwezekanavyo, kwakweli rafiki yangu huyu naye yalimshinda wakatemana na binti bado anatafuta mwanaume anayejua ku care.

Humu JF kuna nyuzi kibao zinazoanzishwa na wadada au wake za watu kuelezwa jinsi ambavyo wameolewa na wanaishi vizuri, mara wana nyumba na kila moja ana gari ila kavutiwa na jamaa fulani anayejua kucare. Yaani unakaa unasoma maelezo ya mtu unashindwa kujua huyu mwanamke ni kahaba au anatafuta kitu kwa mume wake.

Hivi shida ni nini nyie dada zetu mnataka tuwafanyie nini mridhike?

JE MAMA ZENU WALIKUWA NA HAYA KWELI AU MALEZI NDIYO HAMKUPEWA VIZURI AU NDIYO KUSOMA HUKO?

AU NISAIDIENI WADADA ZANGU, NINI MAANA YA KU-CARE?
 
Utafiti wako umeonyesha kuwa wanawake wanapenda caring. Ndivyo hivyo tulivyo ndugu na hatutabadilika labda iwe dunia nyingine. Ishi na wanawake kwa akili..ndo hivyo mlivyoambiwa!
.
.
.
Care, caring ndo tunachotaka. Hatuwezi kufanana na nyie. Pia mna mambo yenu yanakera kama nini lakini ndio hivyo mlivyo, mmeumbwa hivyo na hatuwezi kuwabadilisha!
 
Sawa dada bora umekuja hivi hii care mnayaotaka ni namna nyingine ya kusema mnapenda pesa au? kama siyo je masikini kabisa yaani kapuku anaweza kucare? kama ndiyo nini maana ya kacare mnayotaka haswa walau na mifano kadhaa nione kama niliyafanya hayo au lah.
 
Hujui kucare wewe bahili kama nini.zawadi hujui, kumpigia simu baada ya mwezi yaan ovyo kabisa! Utachapiwa tuu wacha wanaume wanaojua nn maana ya mwanamke wale vilivyoiva
 
Hii ndio shida sasa. Sasa usipomjali wewe unategemea nani amjali.

Ndio uanaume huo hivyo kubali tu hakuna jinsi la sivyo itakuwa ndio kazi yako kuacha acha. Hakuna mwanamke utakayempata na asitake kujaliwa hata kama ni kwa kiwango kidogo.
 
Sawa dada bora umekuja hivi hii care mnayaotaka ni namna nyingine ya kusema mnapenda pesa au? kama siyo je masikini kabisa yaani kapuku anaweza kucare? kama ndiyo nini maana ya kacare mnayotaka haswa walau na mifano kadhaa nione kama niliyafanya hayo au lah.
Care inategemea mtu na mtu. Care ninayoitaka mimi haiwezi kufanana na hiyo anayoitaka huyo wako. Ukimpenda mtu utamjali kama anavyopenda. Na yeye pia akujali kama unavyopenda.
.
.
Pesa pia ni moja ya caring lakini iangalie kipato. MAPENZI NI PESA (huu ni ukweli lakini ni mchungu mno kwa baadhi ya watu). Toa bila shurti usipende kuombwaombwa kila siku.
.
.
NO ROMANCE WITHOUT FINANCE
.
.
Na kama mpenzi wako kazidi kuomba hata bila sababu ya msingi basi muweke chini mueleze wazi kuwa huwezi kumpa hela hovyo hovyo bali kwa utaratibu unaoeleweka. Kama anakupenda atakuelewa, asipokuelewa basi ndio ujue yupo after money piga chini kabla hajakupiga chini.
 
Achana naye akifikisha miaka 30 nyodo zote nje, atawatafuta wanaume kwa torch.

mkuu mbona toka tutemane kashapita kwa wengine kama watatu, juzi ananiambia eti kama naweza kuzidisha care kidogo turudiane, nikamgomea . Wanafikiri maisha ni marahisi kama mtu anayetoka kijijini kuja dsm akifikiri huku maisha yanaokotwa tu.
 
Hii ndio shida sasa. Sasa usipomjali wewe unategemea nani amjali.

Ndio uanaume huo hivyo kubali tu hakuna jinsi la sivyo itakuwa ndio kazi yako kuacha acha. Hakuna mwanamke utakayempata na asitake kujaliwa hata kama ni kwa kiwango kidogo.

kujali hii mnayotaka ni ipi mrembo? hebu nambie contents za care maana nilikuwa nafanya kama mwanaume kwa mpenzi wake ila sikujua anachotaka au ni kutoa roho ya mwanaume? hebu niokoe plz care yenu hii ni ipi?
 
Back
Top Bottom