Amelaaniwa na mke wake, ameanza kuwa chizi

Ciprofloxacin.

JF-Expert Member
Apr 15, 2015
1,583
2,697
Wakuu, ninawaletea taarifa hii nikiwa ni mwingi wa huzuni na majonzi ya hali ya juu.

Hii si hadithi bali ni tukio la kweli kabisa lililomkuta mkuta rafiki yangu na sasa majuto ni mjukuu na sijui tufanyeje,habari yenyewe ipo hivi :
Rafiki yangu Ben (si jina lake halisi) alikuwa akiishi maisha magumu Sana, hana elimu yoyote, alikuwa akiishi Kwa kufanya kazi za ujenzi na vibarua jijini Mwanza, na mimi na wenzangu tulikuwa tukimsaidia matumizi ya hapa na pale Kwa kipato chetu kidogo.

Mungu hamtupi mja wake, Siku moja wakati akiwa anafanya kibarua cha ujenzi maeneo ya nyakato kwenye Nyumba ya mzee mmoja mwenyewe uwezo kimaisha, Ben akawa amebahatika kupendwa na binti Wa Yule mzee, ambaye alikuwa amemaliza kusoma Makerere university Uganda, binti Yule mrembo mwenyewe rangi ya chocolate alimpenda Sana Ben, Naomba nikiri kuwa japokuwa nilikuwa na mke wangu, nilianza kumwonea wivu Sana Ben, nikatamani yule mrembo angenipenda mimi, wakawa wameanza uhusiano wa kimapenzi, yule mzee alipogundua kuwa binti yake kampenda fukara, alimwonyesha haraka Sana avunje hayo mahusiano, binti hakusikia ndo kwanza akazidisha mapenzi Kwa Ben.

Wakuu, ktk hali iliyomshangaza kila mtu na asiamini kilichotendeka, yule mzee alichanachana vyeti vyote vya bintiye kuanzia O level hadi university.
Yule binti alilia Sana, hadi akataka kujiua, Kwa busara ya mama yake mzazi na sisi shemeji zake akawa ametulia na mama yake akawa amempatia pesa za kufuatilia vyeti vingine, badala yake Kwa hasira akawa kamwibia baba yake zaidi ya milioni 20,alizokuwa kaziweka ndani ili akanunue dhahabu porini, alikuwa ni mfanya biashara wa dhahabu.

Binti na mpenzie Ben wakawa wametoroka Mwanza na kwenda kisiwani ambako walianza kufanya biashara ya samaki huku wakiishi Kama mume na mke.

Mafanikio ya kimaisha yakaanza kuwapata, Ben akawa bonge la handsome na pesa kibao, mara akaanza kumbadilikia mkewe, kufumba na kufumbua akamwacha na kuoa mwanamke mwingine huku akimkashfu mkewe, walikuwa na miaka 3 ya kuishi wote na walipata mtoto mmoja Wa kiume.
binti Yule alilia Sana, nakumbuka kauli yake Kwa Ben, ilikuwa "Ukimaliza miaka miwili hapa duniani ukiwa salama, basi hakuna Mungu".

Tulimshauri Sana rafiki yetu hakusikia, baada ya miezi Kama 9 hivi Ben akaanza kufilisika na yule mwanamke mwingine akamkimbia .taratibu akaanza simu, mara viatu, mara nguo, Napoandika hapa sasa hivi analala kwenye mabaraza ya watu na ameanza kuwa chizi, mkewe hata sijui alipo, Ukimwona Ben Kwa wanaomjua inasikitisha japokuwa alijitakia, anatembea huku akiongea peke yake, nimejaribu kumsaidia nimeshindwa, mama yake kashindwa, watu wanasema hadi mkewe aonekane ndo pekee wa kumfungua.

Nimejifunza jambo zito Sana.
 
Everything that you do, you are doing it for yourself. Ime backfire. Wengi sana ambao waliwatendea ndivyo sivyo wake zao iliwarudia. Kuna jamaa alimtelekeza mkewe wakati anaumwa akaoa mwanamke mwingine, mkewe alikufa huku akiwa hana support ya mume. Zamu ya mume ilikuja katika nyakati zake za mwisho nayeye alitelekezwa na mke yule aliyemwoa. Mambo haya Yamewatokea wengi, nadhani wengi watakuwa mashuhuda humu. Tusiwatendee wenzetu yale tusiyopenda kutendewa maana yataturudia.
 
Duuuuuuuu kweli pata pesa tujue tabia yako,,,,hapo laana ziko mbil ya baba wa bint kwa bint yake kwakuwa hakumsikiliza na ya bint kwa Ben aisee maisha bhana
 
Kiukweli mambo haya kwa ambae hajawahi kuona anaweza kusema ni CHAI. Ila kiukweli, mzazi analaani, girlfriend analaani, mchumba analaani, mchumba analaani hata mimba inalaani. Usiombe yakukute.
 
mshana huu uwanja wako wa nyumbani, hebu msaidie kimawazo amtoa ktk uchizi Jamaa yake
Binti alikuwa na upendo wa kweli kwa jamaa upendo usiohoji kwanini...halafu akatendwa pamoja na ku sacrifice na ku risk it all ikiwa ni pamoja na kumwibia mzazi , roho ya maumivu na ile laana ndio vinamtesa jamaa
Hapa kuna mambo mengi sana na kila moja limepata malipo yake sawia
1. Wote Tunaelewa umuhimu wa cheti..baba mtu alifanya vibaya sana kuharibu vyeti vyote vya mtoto
2. Wote tunaijua nguvu ya mapenzi, baba mtu alipinga kwa kila hali hayo mahusiano (malipo ikawa ni kuibiwa pesa)
3. Binti pamoja na kufanyiwa mambo yanayoumiza na mzazi wake lakini hakupaswa kuchukua hatua alizochukua...mzazi ni mzazi tuu (malipo yake ni kukimbiwa na mtu aliyempenda sana)
4. Kijana maskini kapendwa na mtoto wa kishua, akasaidiwa akasaidika halafu akaja kumtenda mkombozi wake (malipo yake ndio hayo)
Ili kuvunja hizi roho za laana visasi na maumivu ni watatu hawa kukutanishwa na kufanya reconciliation.....! Ikitokea mmoja mmoja akatangulia mbele ya haki yajayo mbeleni hayatakuwa na afya sana na ni afadhali atangulie Ben kuliko mojawapo wa hao wawili
 
At u'r best level
 
Back
Top Bottom