Amekuwa akifuatilia malipo yake PSPF kwa miezi miwili bila mafanikio

Kwani muajiri kawaambia anataka hiyo asilimia aliyokuchangia?

na vipi kama mtu akifukuzwa kazi au akaaga dunia kabla ya umri wa kustaafu fao la muajiri linarudi kwa muajiri pia?
Mimi niliambiwa ukiacha kazi kabla ya muda wa kustaafu ndio unapoteza ile portion aliyochangia mwajiri, kuhusu kufariki kwa kweli sikuulizia hilo.
 
wao wana hela za kujenga magorofa na si kuwalipa waliowakata mpaka kujenga hayo magorofa ambayo hayana faida kwa wanachama wa huo mfuko bongo tunaendeshana kama kijiji vile...ujinga huo ufanye South Africa wafanyakazi wanakojitambua uone litalotokea...
 
mimi mwaka jana nilienda hapo hapo PSPF, jamaa wa reception akaniambia kama unavyosema, nilikuwa nimefanya kazi miaka 8, nikataka kuondoka lakini baadaye nikarudi nikamwambia nipe nipe fomu, jamaa akanijibu kwa ukali utadhani fedha ni zake, akanielekeza documents za kuambatanisha, nilifanya hivyo ndania ya miezi miwili nikapata zote michango yangu na ya mwajiri. Sijui kama wamebadilika ila wale wazee wa reception sio wakweli
 
Maofisi ya Serikali Kuna watu Wanajifanya kama ni yao na family zao. Wanafanya wanachokijua sheria wamekuwa wakiweka za kukandamiza watu wengi
 
Hawajakosea wapo sawa kisheria, labda tudai sheria ibadilishwe
Mbona NSSF wao ukiacha kazi any time wanakupa hela yako yooote. Kwa hiyo SSRA wameacha kila mfuko ujiamulie utakavyo, kama ni hivyo basi hamna haja ya kuwa na monitor useless kama huyo.
 
mimi mwaka jana nilienda hapo hapo PSPF, jamaa wa reception akaniambia kama unavyosema, nilikuwa nimefanya kazi miaka 8, nikataka kuondoka lakini baadaye nikarudi nikamwambia nipe nipe fomu, jamaa akanijibu kwa ukali utadhani fedha ni zake, akanielekeza documents za kuambatanisha, nilifanya hivyo ndania ya miezi miwili nikapata zote michango yangu na ya mwajiri. Sijui kama wamebadilika ila wale wazee wa reception sio wakweli
Kwa hiyo hao reception wameelekezwa kudanganya sio, ngoja niwarudie kwa hasira ya mbogo
 
Sifa za kulipwa mafao lazima uwe umefanya kazi miaka 15 na kuendelea au nimekosea?

Sifa ya kuwa pensionable ni kufanya kazi walau miaka 15 sawa na miezi 180, ndiyo una-qualify. Utapewa malipo ya mkupuo na monthly pension. Malipo haya yanategemea parameters mbili muhimu.... 1) idadi ya michango yako meaning kwamba wale waliochangia miezi mingi wanabebwa kwenye kukokotoa mafao yao 2. Wastani wa mishahara yako 5 mizuri ya mwisho kabla hujaacha kazi. Vyote hivi vnaingizwa kwenye tool ambayo wanaiita benefit calculator ambayo itakupa mafao yako
 
Nimeona jamaa humu akilia kuwa PPF wamesitisha mafao ya kujitoa, kweli nampa pole.Sasa kuhusu PSPF nako ni mauzi. Mimi ni mtumishi wa umma kwa miaka kumi sasa lakini kutokana na kamshahara kadogo sijaona maendeleo ya maana zaidi ya kununua viwanja viwili vilivyopimwa, kujenga nimeshindwa mpaka sasa. Ok, basi nikafikiria niache kazi ili nijiajiri na nilitegemea fao la kujitoa liwe ndio capital.

Kwenda PSPF niliishiwa nguvu baada ya kuambiwa nitakachopewa ni kile tu kilichokatwa toka mshahara wangu, kile kilichochangwa na mwajiri kitarudi kwa mwajiri. Nilichukia kuanzia ikulu mpaka serikali za mitaa. Yani ni tofauti na NSSF ambako nimewahi fanya kazi hapo kabla, nilipoacha kazi nilipewa mafao yangu yote na yalinisaidia kweli kuinua kiwango changu cha elimu.

Hivi nyie SSRA mbona mmeacha mifuko hii ya jamii kila mmoja ukijiamulia kivyake!? Yani nina hasira na PSPF wa acha tu.

Pitia hapa: Withdrawal Benefits
 
Haya sasa, ukisikia 'hapa kazi tu' ndiyo hii. Kuanzia sasa, kama upo kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii sahau kuhusu kuchukua pesa zako pale unapoacha kazi. Mifuko yote imepewa maelekezo yakusitisha fao hilo. Kwa hiyo, utasubiri mpaka ufikishe miaka 55.

Nionavyo.
1. Mifuko ina hali mbaya, kwa hiyo wanabana ili wa-survive. Madai ya fao la kujitoa yalikithiri sana (70% ya malipo yote) na kupelekea mifuko kushindwa kupumua (haswa PSPF)
2. Serikali haina pesa, inataka ipate mahali pa kukopa!

Wafanyakazi poleni, Pigeni kazi!
 
Kama ni kweli basi naanza kuamini kuwa #hapakazitu inatekelezwa kwa remote control!
 
Sio kweli huu ni uongo, weka source

serikali haijataka kutangaza ili kuepuka mgogoro. nimezipata taarifa kutoka ndani ya mifuko. maofisa wenyewe hawajapewa maelekezo zaidi ya kuambiwa wasitishe. wanaojua undani zaidi ni wakurugenzi!
 
Nasubiri taarifa kamili ili nijitoe mapema...!

Wasilete ushenzi.

Hela tunawapa, wanazijengea MAKARAVATI, na MAJENGO YA GHARAMA halafu nikiitaka pesa yangu wanisumbue?!

Kudadeki ... Hii ngoma tutapelakana mahakamani kwa wao kukiuka masharti ya mkataba. Dadeki.!
 
Hii ni habari mbaya sana kwangu!! Lakini kwa nini Niiamini? Naomba sababu za kunifanya niamini habari hii!
 
Back
Top Bottom