Amekuwa akifuatilia malipo yake PSPF kwa miezi miwili bila mafanikio

Nambarione

Member
Sep 3, 2013
63
60
Rafiki yangu mmoja kaja analia akilalamika kuwa amekuwa akifuatilia malipo yake huko PSFP kwa miezi miwili sasa bila mafanikio. Anasema process zote zilikamilika Machi mwaka huu lakini malipo hayatoki. Kila akienda anaambiwa hela hakuna, waliomtangulia bado wengi hawajalipwa!

Hivi inawezekanaje mfuko kama huo ukose hela za kulipa wanachama wake kwa wakati au kuna jipu? Wanachama wanalipa michango, miradi waliyowekeza inalipa, inakuwaje wakose hela za kulipa wanachama? Inasikitisha kwa kweli.
 
Kumbe ulikuwa hujui. PSPF fake kabisa. Nadhani hata rushwa bado inatembea pale. Magu wamulike hao hawaendi na kasi yako katika kuhudumia wananchi.
 
Mifuko ya kijamii ya bongo yote fake tu. ubabaishaji mwingi sana. Kwanza unaombwa barua nyingi na unajaza fomu nyingi tu, na ukimaliza unaambiwa hela hamna usubiri. Khaaa, hawajifunzi wenzao huko nje wanavyohudumia wanachama wao? Unakuta mtu anasimamia mirathi anachukua miaka miwili anazunguka tu. haikubaliki kwa kweli. Mhe Rais wamulike hao.
 
hiyo mifuko ndio inahudumia ccm,na ilichangia kampen za ccm unategemea zitakua na hela?
 
INAKUWAJE NAKUPA HELA YANGU CASH KILA MWEZI HALAFU NIKIIHITAJI UNANAMBIA HUNA???...Hiyo miradi hainihusu wala sio makubaliano yetu, kwanza unaitumia hela yangu kujitafutia other income halaf nikiihitaji unanizingua, JIPU HILI, TENA LIKO UTOSINI.
 
nssf ni wazuri sana... kama mwajiri wako amepeleka michango yako kwa wakati

ila shida ni pale mwajiri wako akiwa hapeleki michango nssf kwa wakati... mbona utaisoma namba
 
Kwa sababu akili zetu tumezipeleka kuangalia ni Muislam gani anaongoza haya mashirika, na kwa kuwa Hilo shirika anaongoza asiye Muislam hivyo kukosa kwetu Huduma stahiki wala sio tatizo
 
labda na wao wakijenga daraja la mto wami pale wachangishe changishe kama wenzao kigamboni watakua na chenji za kutosumbua watu..
 
Mpe pole sana,pesa zake anaambiwa hazipo. Mbona wanalipana mishahara kama pesa hakuna. Hii mifuko haimnufaishi mchangiaji kabisa.
 
Rafiki yangu mmoja kaja analia akilalamika kuwa amekuwa akifuatilia malipo yake huko PSFP kwa miezi miwili sasa bila mafanikio. Anasema process zote zilikamilika Machi mwaka huu lakini malipo hayatoki. Kila akienda anaambiwa hela hakuna, waliomtangulia bado wengi hawajalipwa!

Hivi inawezekanaje mfuko kama huo ukose hela za kulipa wanachama wake kwa wakati au kuna jipu? Wanachama wanalipa michango, miradi waliyowekeza inalipa, inakuwaje wakose hela za kulipa wanachama? Inasikitisha kwa kweli.
Nachojua hawa PSPF hua wanalipa pale wanapopata pesa kutoka serikalini, yaani hawana Reserve ya hela ambazo zipo zinasubiri kulipa. Hii ni kwa sababu hawa PSPF hua wanapokea kutoka serikalini na infact serikali haipeleki hela ipasavyo kwenye huu mfuko (refer hotuba ya Rais May Mosi). Kawaida serikali kwa mwezi inatakiwa kupeleka kwenye huu mfuko takribani Tshs 40Billion, hela zinazotokana na Wafanyakazi kukatwa kutoka kwenye mishahara yao, lakini hilo limekua halifanyiki. Hii inapelekea hawa PSPF kutolipa kwa wakati muafaka, na kwa sasa wameshalipa mpaka wastaafu wa December 2015 na January 2016. Katika deni hili la serikali kuchelewesha makato wanadaiwa zaidi ya 250Billion na huu mfuko

Pili inawezekana kabisa huyo rafiki yako alikua muajiriwa wa serikali hata kabla ya mwaka 1999. kama jibu ni ndio basi huu mwaka wa 1999 serikali iliwahamishia wafanyakazi wake akiwemo huyo rafiki yako kutoka Hazina na kuwaleta kwenye huu mfuko. Sasa basi hapo kabla ya 1999 huyo rafiki yako makato yake yalikua yanaenda hazina lakini kuanzia huu mwaka yalikoma kwenda kwenye hazina na kuanza kwenda kwenye huu mfuko. Uhuni uliofanyika ni kua majina tu ndio yaliyohamishwa kwenda PSPF, lakini zile hela walizokua wakichukua hazina za makato hawakuwapa PSPF, na hapohapo serikali wanataka PSPF wakilipa mafao walipe hata na makato ya kabla ya 1999 ambayo hela hao PSPF hawakuzichukua. Kwa taarifa zilizoko ni kua deni hili ambalo serikali inadaiwa kutokana na hao wastaafu wa nyuma ya 1999 (Pre-99) ni zaidi ya 1Trillion.

Tatu ni kua Serikali iliwaahidi wananchi wa Dodoma kua itawaajengea Chuo Kikuu Kikubwa kuliko vyote East Africa kama ahsante kwa wnanchi hao kwa kuendelea kuichagua CCM (Political reason??!!). Sasa basi kama ujuavyo ahadi nyingi za kisiasa hua zinakuaga haziangalii uwezo wa kifedha wa serikali hivyo iliyaamuru mashirika ya mfuko wa hifadhi ya jamii PSPF, NSSF, LAPF etc kushirikiana na kukijenga hiki chuo (UDOM). Chuo hiki kilijengwa kitambo tu na hadi leo serikali haijalipa huu mkopo kutoka haya mashirika. Kwa hili sina uhakika wa kiasi cha deni linalodaiwa ila nikilipata nitakuja ku-edit hapa

Hivyo namalizia tu kua mchawi wa malipo yako ni serikali na sio huu mfuko. Na kwa taarifa yako tu ni kua pamoja na wastaafu wengi sana kulalamika juu ya huu mfuko kuwacheleweshea malipo yako, lakini hutoona Mtumbua Majipu JPM kuwatumbua viongozi wa huu mfuko sababu hata yeye mwenyewe anajua jinsi serikali yake inavyodaiwa na huu mfuko.

Nimemaliza
 
mmmh mpaka ninatetemeka kwa hasira
 
INAKUWAJE NAKUPA HELA YANGU CASH KILA MWEZI HALAFU NIKIIHITAJI UNANAMBIA HUNA???...Hiyo miradi hainihusu wala sio makubaliano yetu, kwanza unaitumia hela yangu kujitafutia other income halaf nikiihitaji unanizingua, JIPU HILI, TENA LIKO UTOSINI.
Ukiwa unafanya kazi Shirika binafsi unaweza kusema hela yako unapeleka NSSF,
But kwa wewe wa Serikalini unajuaje kama mwajiri wako ambae ni Serikali/hazina anapeleka hela PSPF kwa wakati??
 
Nimeona jamaa humu akilia kuwa PPF wamesitisha mafao ya kujitoa, kweli nampa pole.Sasa kuhusu PSPF nako ni mauzi. Mimi ni mtumishi wa umma kwa miaka kumi sasa lakini kutokana na kamshahara kadogo sijaona maendeleo ya maana zaidi ya kununua viwanja viwili vilivyopimwa, kujenga nimeshindwa mpaka sasa. Ok, basi nikafikiria niache kazi ili nijiajiri na nilitegemea fao la kujitoa liwe ndio capital.

Kwenda PSPF niliishiwa nguvu baada ya kuambiwa nitakachopewa ni kile tu kilichokatwa toka mshahara wangu, kile kilichochangwa na mwajiri kitarudi kwa mwajiri. Nilichukia kuanzia ikulu mpaka serikali za mitaa. Yani ni tofauti na NSSF ambako nimewahi fanya kazi hapo kabla, nilipoacha kazi nilipewa mafao yangu yote na yalinisaidia kweli kuinua kiwango changu cha elimu.

Hivi nyie SSRA mbona mmeacha mifuko hii ya jamii kila mmoja ukijiamulia kivyake!? Yani nina hasira na PSPF wa acha tu.
 
Na hakuna pa kuongelea maana na wabunge wa upinzani wanaelekezwa cha kuongea, ccm ndiyo usitegemee kabisa kama itatetea wanyonge
Mimi nadhani wamezuia bunge live ili wananchi tusi sikie hoja zetu tunazowapa wabunge watuongelee. Inauma sana mtu unataka ujiajiri halafu hivi vitaasisi vya mafao vinazuia mitaji yetu.
 
Back
Top Bottom