BABA TUPAC
JF-Expert Member
- Sep 30, 2015
- 1,526
- 3,802
Hili swala nimekuwa nikilisikia, sijawahi kulishuhudia hata siku moja lakini leo nimeliona.
Mwezi kama mmoja uliopita kuna jamaa yetu alifariki, huyu jamaa tulisoma nae shule sekondari mkoani Mbeya. Inaitwa Meta Sekondari
Sisi tukaona tuchange rambirambi kumfariji mke wa marehemu. Kwa uwezo wetu tulionao na idadi ndogo iliyopo kilipatikana kiasi cha sh 81,000 tu (Yaani elfu themanini na moja tu).
Tukamuomba mmoja wetu awasilishe kwa mke wa marehemu. Huyu jamaa ni mtu ambaye alikuwa karibu sana na marehemu, amewahi kuishi pamoja na marehemu. Tunaweza kusema walikuwa kama ndugu kabisa, huyu tapeli tumuite Gabriel Amos
Wiki kadhaa baada ya kumpa kiasi hicho cha fedha bwana Gabriel, aliulizwa kwenye group kama aliwasilisha mchango. Jibu lake lilikuwa, mchango nilishampa mke wake na amewashukuru sana. Basi tukafurahi, hilo likapita
Sasa hii leo kuna mdau kampigia simu mke wa marehemu (walikuwa wanafahamiana). Akampa pole kisha akamshauri awe added kwenye group ashukuru kisha atoelewe. Shemeji, akasema ashukuru kivipi? Akaambiwa kuhusu michango akasema, mbona hajapokea mchango wowote.
Basi ikawa taflani kwenye group, aliyekula mchango wa msiba anasemwa hatari. Akasema labda alikosea namba wakati anatuma, alipoulizwa mbona ulisema mke wa marehemu alishukuru sana inakuaje sasahivi umeseme ulikosea namba. Akawa hana majibu, ikabidi arudishe ile pesa kwa aibu kubwa sana.
Napenda kuwaambia, kuna watu hawana aibu hata michango ya msiba wanakula. Kuweni makini, ndugu Gabriel Amos uliyemaliza Meta Sekondari huko Mbeya mwaka 2007 aibu iwe juu yako. Huwezi kula pesa ya msiba wa rafiki yako, rafiki yako wa karibu mno.
Sent using Jamii Forums mobile app