Ameandika William Shao: Kanisa Katoliki si populism

Ameandika William Shao: Kanisa Katoliki si populism

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,286
Reaction score
10,831
Tangu jana hadi leo nimesoma humu hoja mbalimbali kuhusu wale "Wakatoliki" walioandamana kwenda Ubalozi wa Vatican. Nikajifunza, nikaacha niliyojifunza, halafu nikajifunza tena. Natangaza maslahi: Mimi si Mkatoliki, na sifikiri kama nitakuwa Mkatoliki baada ya leo. Nafanya tu analysis ya kawaida kwa tukio lile.

Hili si tukio la kawaida, wala si mjadala wa hisia. Ni tukio linalogusa kiini cha taasisi ya kidini yenye historia ya zaidi ya miaka 2,000, taasisi iliyojengwa juu ya teolojia, sakramenti, mamlaka ya kihistoria na nidhamu kali ya kikanuni.

Ni tukio linalogusa hisia za waumini, lakini pia linagusa uhusiano nyeti kati ya dini na siasa, uhuru wa kikatiba, mipaka ya uhuru wenyewe, na hatimaye hatari ya kugeuza imani ya watu kuwa chombo cha ajenda zisizo wazi.

Kwa sababu hiyo, uchambuzi wowote makini lazima ujengwe juu ya nguzo tano zisizotenganishwa:

1. Ukweli wa kihistoria

2. Mantiki ya kikanisa

3. Msingi wa kisheria wa Kanisa Katoliki

4. Busara ya kijamii, na

5. Hekima ya kifalsafa ya dini.

Bila nguzo hizi, mjadala huu utabaki kuwa kelele. Lakini tukiwa na nguzo hizo, mjadala utageuka kuwa maarifa.

Swali la kwanza, na ambalo haliwezi kurukwa, ni hili: Je, waliojitambulisha kama Wakatoliki na kwenda Ubalozi wa Vatican walitaka kufanikisha nini hasa?

Tukichukulia—kwa hoja ya juu kabisa ya kimantiki—kwamba walioandamana ni Wakatoliki halisi, basi lengo lao lingeweza kuwa mojawapo au mchanganyiko wa yafuatayo:

1. Kutoa malalamiko dhidi ya uongozi wa Padre Charles Kitima;

2. Kushawishi mamlaka ya juu ya Kanisa ichukue hatua dhidi yake; au

3. Kujenga simulizi kwamba amekiuka wajibu wa kikanisa kwa kuhusika na masuala ya kijamii na/au ya kisiasa.

Kwa kuchambua kauli zao, mienendo yao, lugha waliyotumia, na muktadha mzima wa tukio, jambo moja linajitokeza kwa uwazi wa kutosha:

1. Hakukuwa na lengo lililofafanuliwa kwa lugha ya kikanisa au ya kitaasisi.

2. Hakukuwa na malalamiko yaliyowasilishwa kwa mfumo unaotambuliwa na Kanisa Katoliki

3. Hakukuwa na hoja zilizojengwa juu ya Canon Law; wala

4. Hakukuwa na msimamo uliotangazwa kwa namna ambayo Kanisa lingeweza kuushughulikia kisheria—hata kiimani.

Hili linazalisha tatizo kubwa la kimantiki ambalo wang'eng'e wanaliita mismatch between intent and lawful capacity.

Hata tukitoa nafasi ya kudhani kuwa walikuwa na nia njema, njia waliyotumia haiwezi kabisa kuzaa matokeo yoyote halali ndani ya mfumo wa Kanisa Katoliki.

Iwapo lengo lilikuwa kumuondoa Padre Charles Kitima katika wadhifa wake kama Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), basi kikanisa na kisheria hilo haliwezekani hata kwa nadharia, hata kwa ndoto.

Padre Kitima hawajibiki kwa Ubalozi wa Vatican, wala kwa waumini binafsi, bali kwa Mkutano wa Maaskofu wa Tanzania, chini ya taratibu rasmi za Kanisa.

Kwa lugha ya Canon Law, waumini wa kawaida hawana locus standi ya kumwondoa kiongozi wa ngazi hiyo kwa hatua ya hadhara, wala maandamano hayaundi forum halali ya kikanisa.

Iwapo lengo lilikuwa kumtia shinikizo la kimaadili au kisaikolojia, basi pia Kanisa Katoliki si taasisi inayofanya umuzi kwa misingi ya presha ya hadhara.

Uamuzi wa Kanisa hutokana na ushahidi, taratibu na busara ya kichungaji. Na iwapo, kwa mtazamo mpana zaidi, tukio hili lilikuwa na ajenda ya kisiasa iliyojificha nyuma ya lugha ya dini, basi hapo ndipo hatari yake inapoongezeka maradufu.

Kanisa si POPULISM


Hapa ndipo mantiki ya kikanisa ilipo. Kanisa Katoliki ni taasisi ya hierarchical authority, si taasisi ya populist democracy. Hili ni jambo la msingi linalopaswa kueleweka kabla ya kutoa hukumu yoyote.

Kwa mujibu wa Code of Canon Law (CIC, 1983), viongozi wa Kanisa huwekwa na kuondolewa kwa taratibu mahsusi, chini ya mamlaka ya Maaskofu na, kwa kiwango cha juu, Vatican kupitia Dicastery husika.

Dicastery ni idara au wizara rasmi ya Kanisa Katoliki, hasa uongozi wa Vatican, inayoshughulikia eneo maalumu la kazi za Kanisa. Hilo linatokana na neno la Kigiriki dikasterion, likimaanisha chombo cha utawala au mahakama ya kanisa.

Hakuna hata kifungu kimoja—nasema hata kimoja—miongoni mwa vifungu vyote 1,752 vya Canon Law kinachotambua maandamano ya barabarani kama chombo cha kinidhamu cha Kanisa.

Malalamiko, hata yakiwa mazito kiasi gani, huandikwa kwa heshima, huwasilishwa kwa Askofu husika, hujadiliwa ndani ya Mabaraza, na pale inapobidi, huwasilishwa Vatican kwa njia rasmi.

Haki ya waumini kutoa maoni yao ipo (Canon 212 §3), lakini haki hiyo huambatana na staha, ukweli, busara na kamwe haiwezi kuwa fedheha ya Kanisa lenyewe. (Nimeambatanisha hiyo Canon).

Hiyo ndiyo mantiki ya Kanisa; nje ya hapo, hakuna uhalali wa kikanisa wa kufanya yale tunayoambiwa yalifanyika. Sasa hawa ni Wakatoliki gani wasiojua taratibu za kikanisa za kanisa lao?

Kwa lugha ya kisheria, tukio hili lazima tu lingeanguka kwa misingi ya lack of locus standi na wrong forum. Hoja zisizoletwa kwa njia sahihi hazisikilizwi, hata kama zingekuwa na msingi.

Padre, masuala ya jamii na ukweli wa mafundisho ya Kanisa

Hoja kwamba Padre Kitima “aache masuala ya kijamii” ni hoja inayopingana moja kwa moja na historia na mafundisho ya Kanisa Katoliki. Tangu ile ambayo Wakatoliki wenyewe wanaita 'Rerum Novarum' ya Papa Leo XIII (1891), kupitia Gaudium et Spes (Katiba ya Kichungaji) ya Mtaguso wa Pili wa Vatican, hadi mafundisho ya Papa John Paul II, Benedict XVI na Papa Francis, Kanisa limekuwa likisisitiza kuwa haliwezi kukaa kimya mbele ya dhuluma, ukiukwaji wa utu wa binadamu na uovu wa kijamii.

Hiyo 'Rerum Novarum' ni waraka (Encyclical) wa Papa Leo XIII unaohusu hali ya wafanyakazi, haki za kazi, umiliki wa mali, wajibu wa waajiri, wajibu wa serikali na haki za binadamu katika jamii ya kisasa ya viwanda kwa wakati huo, na bado inafanya kazi hadi karne hii kama foundational framework.

Kwa hiyo, ushiriki wa Padre Kitima katika mijadala ya haki, amani na masuala ya kijamii si kosa la kikanisa, bali ni utekelezaji wa moja kwa moja wa Social Teaching of the Church. Hoja ya kumtaka Padre ajitenge na jamii si ya kiteolojia, si ya kihistoria na si ya kikanisa.

Kulikuwa na mjadala wa alama, mavazi na lugha. Hii kwangu ni teolojia isiyoandikwa.

Katika taasisi za kale kama Kanisa Katoliki, alama ni teolojia hai. Hili linathibitishwa na wanateolojia na anthropologists wa dini kama Clifford Geertz Literature yake imejaa tele, hapa narejea The Interpretation of Cultures kilichochapishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1973), na humo ndani anaeleza kuwa taasisi huwasiliana kupitia ALAMA kuliko MANENO. Mavazi, nyimbo, lugha na mienendo si mapambo; ni sehemu ya ujumbe.

Kwa hiyo, hoja kwamba “mavazi hayana maana” inapuuza context nzima ya kidini. Kukutana na Balozi wa Papa si tukio la kawaida; ni tukio la kidiplomasia na la kikanisa linalohitaji staha maalumu. Huwezi kwenda na DERA au JEANS. Pale alama zinapokosewa, ujumbe wote huporomoka, hata kama hoja ingekuwa na mashiko.

Biblia, maarifa na uwakilishi.

Ni kweli kwamba Kanisa Katoliki halijajengwa juu ya kukariri mistari ya Biblia kwa kichwa. Lakini ni kweli pia kwamba muumini anayejitokeza hadharani kuwakilisha Kanisa katika tukio zito anapaswa kuwa na maarifa ya msingi ya maandiko na liturujia. Kushindwa kabisa kutofautisha vitabu, sura na mistari, pamoja na kutumia lugha isiyo ya kikanisa, kunazua mashaka halali juu ya uwakilishi na uhalisia wa madai ya utambulisho.

Hapa si suala la dharau, bali ni tathmini ya kitaasisi ya uaminifu wa uwakilishi.

Hatari ya kuchezea imani, somo la historia

Historia ya dunia inatoa mifano ya kutosha ya madhara ya kuchanganya dini na siasa bila busara. Lebanon, Nigeria, Yugoslavia ya zamani, n.k ni mifano hai ya jinsi instrumentalization of religion inavyoweza kuvunja jamii na kuharibu mataifa. Hii kutumia dini kama chombo au kifaa cha kufanikisha malengo mengine yasiyo ya kidini, badala ya kufuata maana halisi ya dini yenyewe.

Mwalimu Julius Nyerere alionya kwa busara isiyozeeka aliposema: “Tusiendekeze udini, wala tusipuuze udini.” Onyo hili linabaki kuwa la msingi katika Tanzania ya leo.

Kwa uchambuzi wa kisheria, kikanisa, kifalsafa, kihistoria na kijamii, hitimisho haliepukiki. Waandamanaji hawakuwa na mamlaka ya kikanisa ya kumuondoa Padre Kitima. Njia waliyochagua haikuwa sahihi wala haiwezi kuzaa matokeo yoyote halali. Dalili nyingi zinaibua mashaka juu ya uhalisia wa uwakilishi wao wa Kikatoliki, na hata kama wangekuwa Wakatoliki halisi, walipaswa kutumia taratibu za ndani za Kanisa.

Njia halali ambayo Mkatoliki yeyote angeitumia iko kwenye ukurasa wa 71, wa Code of Canon Law, kwenye Title I inayoitwa 'The Obligations and Rights of All the Christians Faithful'. Hapo utakutana na 'Canon 212 §3' inayosema hivi:

"...In accord with the knowledge, competence and preeminence which they possess, they have the right and even at times a duty to manifest to the sacred pastors their opinion on matters which pertain to the good of the Church, and they have a right to make their opinion known to the other Christian faithful, with due regard for the integrity of faith and morals and reverence toward their pastors, and with consideration for the common good and the dignity of persons."

Kanisa Katoliki limeishi zaidi ya miaka 2,000, limepitia mapinduzi, vita na migogoro ya kila aina, na bado limesimama likitumia hizi Canon.

William Shao
06.01.2026
 
CCM watakipata wanachokitafuta. Muda utaongea.
Kuna siku ccm siyo tu itafutwa bali itakuwa ni najisi kutamka ccm au kujihusisha nayo, itakuwa kama CCCP na wakati huo huo Kanisa Katoliki litakuwepo kwa miaka mingi ijayo mpaka ukamilifu wa dahari.
 
Screenshot_20260122_173120_Samsung Internet.jpg
 
Back
Top Bottom