Ambulance ya Nassari yaharibikia barabara ya Kikwe

mmaranguoriginal.

JF-Expert Member
Jan 1, 2014
4,060
1,500
Wadau nawasalimu sana.

Kama ilivyo ada ya mbunge Nasari kuwadanganya wananchi Wa Meru juzi alipata aibu ya mwaka Mara baada ya ambulance alizozileta kimagumashi (inasemekana kuwa zilipakwa rangi kwa nje kuonyesha mpya) ziliharibikia barabarani akielekea njia ya Kikwe hapa Meru kuwaonyesha matunda ya ubunge wake kwa vipindi viwili.

Mosi mtoa taarifa Wa karibu Wa mbunge huyo kaniambia kuwa Mara baada ya kuharibikia njia ya Kikwe ilibidi kwa aibu awashe gari yake kuelekea mjini kumleta Fundi wake ambaye kimsingi ndiyo anayetengeneza magari yake huku akipandisha vioo vya gari wananchi wasimgundue kuwa ni yeye.

Aghalabu niliwahi kusema huku JF kuwa Nassary kiukweli amekuwa msanii haswaa kuelekea huu uchaguzi kwani hata gari hizi bado hajazikabidhi mamlaka husika lakini zimeanza kumwaribikia njiani na tukisema kuwa anaharibu legacy yake kama kijana kwa kuwa muongo kuna think tank wanakuja huku kunitukana kuwa Nina wivu naye ,kimsingi unaposimimia ombwe la hawa wabunge Wa CHADEMA utatukanwa sana na " wabeba mikoba" Wa BAVICHA.

Nawasilisha
 

Kennedy

JF-Expert Member
Dec 28, 2011
33,112
2,000
Nadhani Gari Kuharibika Siyo Jambo Geni
Lete Hoja Kuhusu Hizo Gari Ikiwa Kama Kweli Zilipakwa Rangi Na Huko Ziliko Nunuliwa
Unajua Lolote
 

simba wa mara

JF-Expert Member
May 21, 2015
377
0
kwanza ht walio mtangulia ht hz mbovu unazo ita hawakuwai kuwaletea au eb jibu!.alafu achen maada za kinafk km hz mtu anawaletea vitu vy maana ambavyo wengne kwa miaka 50 wameshindwa alaf ww unaleta uchawi wa maneno km hy!ama kweli waafrika lik u is zombi.
 

Marire

JF-Expert Member
May 1, 2012
12,255
2,000
Bila picha huaminiwi hapa jf
*Pia mleta mada unakumbuka kampuni ya Toyota ilishawahi kuuza magari mapya yakawa mabovu na kulazimika kugaramia yarudishwe kiwadani?

Kama alivyo binadamu kuumwa hata magari huaribika
 

kuku87

JF-Expert Member
Mar 3, 2013
1,221
1,500
Ya ccm ambayo haijaharibika ni ipi? Kwani kununua gari used ni kitu kigeni mpk boxa yako used huji kuitangaza hapa
 

kapotolo

JF-Expert Member
Sep 19, 2010
3,727
1,225
Weka picha mkuu zinafanya kazi wapi.
Mbona picha ya kuharibika hamjaweka, bora yeye katuletea gari hata kama ni mbovu kuliko JK na CCM yake kuwatukana na kuwadharau wanawake wa Tanzania kwa kuwaletea baiskeli za miguu mitatu. Hebu bebeeni mama zenu na wake zenu hizo pikipiki muone kama mlichofanya sio dhihaka kwa wajawazito.
 

Renegade

JF-Expert Member
Mar 18, 2009
6,396
2,000
mmaranguoriginal

Aibu huna , lakini hata shukurani kidogo tu nayo huna? Hata kama zimeharibika hazijawahi kufanya kazi hata kidogo? Muogopeni mungu saa nyingine.
 
Last edited by a moderator:

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom