well behaved women never make history.........
Nimekuwekea THANKS siyo kwa vile nakubaliana na mawazo yako yote 100% la hasha! Bold ya blue ni maeneo ambayo nakubaliana nawe kuwa kuna cha kujifunza na kuelewa. Kwenye nyekundu mhh!Umeongea point kabisa. Najua ukweli huu wengi hawataki kuusikia lakini huwezi kushindana na ukweli ukashinda. Mi nadhani wanawake hawakupaswa kupewa majukumu mengi zaidi ya kulea familia. Leo tuna kizazi korofi kwa sababu watoto hawalelewi majumbani kwao. Mama anaondoa saa 11 asubuhi na anrudi saa 4 usiku (almost 6 days a week) na akifika nyumbani anakuwa na ma-stress kibao ya kazini hana muda na watoto wala mme. kama mwanaume unawahi kurudi nyumbani utakoma maana kero zote za home ambazo huna competency ya kuzi-handle itabidi ukukuruke nazo tu.
Lazima ifike mahali tujiulize nini hasa maana ya maisha. Tusikimbilie kusaka pesa kwa kudhani ndo tunatafuta maisha. Mi policy ya nyumbani kwangu ni kuwa sitaki mke wangu awe busy na kazi kuliko familia. Ni heri tuishi kwa mshahara wangu lakini mke wangu awe na muda na familia. Maana usipokuwa makini watoto watakuja kuwa a very big liability kwa kukosa malezi. Mi nikifika home nataka nimkute wife, ameshaweka mambo sawa na anakuwa na nguvu ya chakula ya usiku ya watu wakubwa (i.e. tendo la nanihiiii).
Sasa unakuta mwanamke anarudi saa 4 usiku ana-mastress kibao ya kazi, ataweza kweli kushiriki tendo la ndoa na mmewe vizuri. Let us face it - kuna mambo/kazi ambazo wanawake hawakuumbwa kuzifanya ila ni ukichwa ngumu tu na haya mambo ya gender balance ambayo hayatusaidii kwa lolote.
..hivi wanaume wanavyokunywa pombe mpaka usiku wa manane, 7 days a week, hawaathiri malezi ya familia zao?
..je, jukumu la kutunza watoto ni la mwanamke peke yake?
Nakubaliana na wewe roselyne1, mambo ya kutunza nyumba na familia ni kwa jinsi mwanamke anavyoijali familia yake. kuna wanawake wapo nyumbani tu na hata hawaijali familia kama wale wanaofanya kazi...kuna ukweli fulani ktk usemayo,ila sio kwa wanawake wote...
...I doubt kama nyumba 'zote' ambazo mama ni mama wa nyumbani,ndio zinatoa familia bora...
...unaweza ibua mwanamke hajasoma na hana kazi na akawa 'bogus' nyumbani vile vile .... 😛ainkiller:😛ainkiller:
..mimi nafikiri kids need love, a sense of security, and direction.
Kama mtoto akiharibikiwa then you will have to look at the totality of the circumstances that led to huyo mtoto kuharibikiwa. In some instances you can't just wholly lay the blame on the parents. Parents can only do so much. The child also has a responsibility to listen, make the right choices, and stay away from bad influences. I also believe that some people are genetically predisposed to making the wrong choices in life i.e. kuharibikwa...vilevile mambo ya malezi nadhani ni complex sana na kama mtoto "ataharibikiwa" basi ni lazima lawama zote zielekezwe kwa mzazi.
Yep...that's peer pressure. Nakumbuka mimi wakati niko sekondari baadhi ya watu niliokuwa na hang nao walikuwa wanaona ujanja kutoroka shule. Ukiwa na mahudhurio hafifu, usipojali kujituma darasani, ukiwa mtu wa kujirusha kiwanja, n.k. ndio ulikuwa unaonekana 'shapu' au 'street smart'. I guess fainali ilikuwa ukubwani maana leo hii baadhi yao ukikutana nao yaani ni choka mbaya na utapigwa mizinga hadi utatia akili...unaweza ukawa unalea mwanao vizuri tu, lakini akitoka nyumbani anakutana na influence nyingine za ajabu-ajabu.
Success in raising your kids will come only if your kids cooperate. If they don't, then no matter what you do will be futile. Mimi nimeshaona watoto wa maprofesa kibao hapo UDSM wakiharibikiwa licha ya kuzaliwa na kulelewa kwenye academia. Baba msomi, mama msomi na wote wanatambua umuhimu wa malezi bora kwa mtoto. Wanawapeleka watoto wao kwenye shule nzuri tu lakini mtoto anakuja kuharibikiwa. Why?..pia vipi kuhusu wale single parents ambao wanawalea watoto vizuri mpaka kufikia watoto hao ku-excell. je single-parents wana luxury ya muda wa kukaa naku-monitor watoto kama house wives? how do some single parents succeed in raising their kids, while some married couples fail do to the same?
sina nia mbaya na hili.. Ni mtazamo wangu wangu tu!!
Wengi wa wanawake waliofanikiwa/ wenye njaa ya kufanikiwa kielimu/ kiuchumi wamejikuta wanapoteza wenzi wao au wanaishia kuwa na mahusiano tata.!! Wengi wao au.. Wameachika.. Wanachelewa sana kupata wenza wa maisha... Wanaishia kuwa 'chakula' ya serenget boys.. Wanazeeka wakiwa wapweke.. Na zaidi ya yote watoto wao, licha ya kuwa na maisha bora, wanakosa 'elimu dunia' na kuishia kuharibikiwa..
Binafsi namtazama mwanamke kama nguzo ya familia...aghalabu, nyumba isiyo na mama mambo mengi yahusuyo familia(umoja, maadili n.k.) huenda mrama. Familia nyingi ambazo ziko imara,mwanamke ni kama amejitoa sadaka(kuachana na malengo ya mafanikio makubwa) kwa ajili ya mumewe, wanawe na familia kwa ujumla..!!
the more the ambitious the woman is, chances are, she will lead a lonely and emotionally distressful family life and vice versa!!
Kwa mwanaume kuwa na mahusiano imara na huyu'ambitious' woman(sorry for kiswakinge), akubali kuwa na utwala wa "kura ya turufu" au akubali kuwa ka-"bushoke"!!
Nakubali kukosolewa!!