Ambao hatukuzaliwa Dar: Tukumbushane jinsi tulivyokuwa tunapotea pale mjini Kariakoo

Dec 31, 2017
88
77
Habarini za Jioni,

Mwaka 2008 nilikuja hapa Mjini Dar es Salaam, baada ya kumaliza Form four na nilibahatika nilikuwa na vi akili kidogo mjomba wangu alinitaka nije nikae nikiwa nasubiri matokeo yangu.

Kwa sababu mjomba alikuwa ananipenda sana, basi alipenda kuwa ananichukua tunaenda wote pale Ilala boma alipokuwa akifanyia kazi.

Enzi hizo Jiji lilikuwa la Kandoro, basi tulikuwa tukipata muda tunatembea kwa miguu kwenda Mjini Kariakoo.

Siku moja nikiwa home niliona na mimi niende Kariakoo, nikipanda magari pendwa yale ya msitari mwekundu.. Kimara-Kkoo.

Basi safari mdogo mdogo bila kujua nashukia wapi, maana sikuwahi kwenda kwa Daladala. Nikastuka tumefika pale Bigbon sheli watu wote wakashuka, nikaona ni vema na mimi nishuke itakuwa ni mwisho basi nilizunguka mule ndani ya Kariakoo kama unavyojua ukiwa umezoewa ground building za kule Mkoani yaani shingo na kichwa vinakuwa Juu juu kushangaa maghorofa.

Nilikuja kustuka imeshafika saa kumi na mbili basi nikasema nipatafute pale Bigbon.Nakumbuka nilitembea takribani lisaa limoja nikipatafuta bila mafanikio.

Wazo lilinijia hivi pale boma si karibu tu, ngoja nipatafute mpaka nipapate then nikaanzie hapo. Nikaitafuta ile round about ya kipindi kile pale Uhuru. Nakumbuka nilitumia nusu saa nikaiona.

Nilipoiona nikaanza mdogo mdogo mpaka Boma, nilipofika pale nikajiuliza nifanye nini ili nikipate hicho kituo likaniijia wazo nipige simu nyumbani basi nikapiga wakaniambia panda tu piki piki umwambie akulete Kimara vinane. Basi nikaitafuta pikipiki huku moyoni nikiwa nasema aisee hii ndiyo Dar.

Ila sasa hivi ukinikuta foleni napambana na foleni ukichomeka nakutukana mshamba nini wewe umekuja mjini lini hahaahahaa!

Kama kuna mwingine alishawahi kupatia kitu kama hiki kiweke tukumbushane.
 
Hahahaa mimi yangu sio kariakoo ilikua ni ubungo - mwenge nilipokuwa napita kwa gari nilikua napaona karibu kinoma basi siku moja nipo ubungo nataka kuwahi zangu pindi la tution mwenge nikaona nikanyage mguu fasta kama dk 10 tu..

Mdogo mdogo nikaanza kutembea ile nafika usawa wa udsm ndo najua bado kidogo nifike mwenge kumbe wapi..
Nimetembea na jua la saa 8 kali kinoma wakati mimi nimezoea baridi ya mafinga..
Ile kufika mlimani city nimechoka kinoma na jasho linanitoka nikasema ngoja nikazane kidogo ..
Nilotembea tena ki umbali flani nikaona sasa ntapata dehydration bure kwa jinsi jasho lilivyokuwa linanitoka..
Nikaamua kupanda bajaji..

Ile napanda bajaji hata dk 2 hazijapita nimeshafika mwenge...
Ikabidi nitoe hela ya bure
 
Dar kubwa sana mkuu wangu, nimezaliwa Dar lakini bado kuna sehemu nikitaka kwenda lazima nipige simu kuulizia chochoro.
 
Kuzaliwa dar na kutopotea kariakoo havihusiani. Dar ni jiji kubwa kupotea ni kawaida hata kwa wazawa.
 
Mimi siku ya kwanza nimeingia mikadi beach Kigamboni bana, nikapotea mule ndani, ikabidi nizame ndani ya maji baharini.
Humo namo nikapotea weee.

Ile naibuka kama masaa matatu hivi najikuta niko Chadibwa beach.

Yaani hatari tupu.

Ikabidi nitembee masaa matatu kuelekea Hunters beach, then masaa manne kuingia mikadi.
 
Mimi na ujanja wote pamoja na kuwa chalii wa gheto na PhD yangu ya mtaa ila Career Core napaheshimu sana.

Huwa naenda kufanya manunuzi, unakuta umepata huduma duka fulani nzuri basi nasema nikija tena nakuja kwenye duka hili hili.

Kinachotokea siku nikienda tena naishia kuzunguka masaa kulitafuta hilo duka mpaka naamua kununua kwa wengine tu..

Huwa nahisi hawa wafanyabiashara wa career core ni wachawi sana kiasi majengo huhama yenyewe na kujatega upande wenye entrance ya watu wengi
 
Nilikuwa naenda Tandika ghafla nikapitishwa nimekuja kushushwa Gongo La Mboto weee wacha nimtukane konda na dereva wake
 
Mimi na ujanja wote pamoja na kuwa chalii wa gheto na PhD yangu ya mtaa ila Career Core napaheshimu sana.

Huwa naenda kufanya manunuzi, unakuta umepata huduma duka fulani nzuri basi nasema nikija tena najuja kwenye duka hili hili.

Kinachotokea siku nikienda tena naishia kuzunguka masaa kulitafuta hilo duka mpaka naamua kununua kwa wengine tu..

Huwa nahisi hawa wafanyabiashara wa career core ni wachawi sana kiasi majengo huhama yenyewe na kujatega upande wenye entrance ya watu wengi
Hata mimikuna siku nilinunua chaji duka fulani nikasema nitakuja siku nyingine ila siku iliyofika naenda pale sipaoni nimezunguuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuukaaaaaaaaaaa weeeeeeeeee mpaka basi
 
kariakoo hapo nilipotea sana...
kuna maeneo huko mikoani ukiishi muda mrefu unadhani ndiyo standard ya miji yote duniani.
pia ramani yangu iilikuwa ni jua, kujua kaskazini ili nijue naelekea wapi ili nipate kupotelea kwenye chimbo langu nje ya jiji. Cha ajabu hapo kkoo au dsm jua lilinichanganya sikulielewa kabisa muelekeo wake ni wapi kila kona naona linaelekea tu.
Siku niliyochemka zaidi nilifika mida ya saa moja jioni, alafu nimeaminishwa kuwa jamaa wote wa jijini hapo hasa kariakoo ni weziwezi. nilipambana kimyakimya na mizigo yangu hadi nikajikuta nimetokea kituo cha daladala pale mnazi mmoja opposite na wanapouza khanga na vitenge. huo mzunguko wa kutafuta kituo bila kuuliza mtu tena ilikuwa mara ya pili kutua kkoo na nilishukia pale daladala za tmk/mbagala zilipokuwa zinaishia(kkoo). nilizunguka zaidi ya saa moja.
googlemap kwa sasa haiwezi kudanganya, unaingia hata prongyang bila kuzubaazubaa.
 
Hahahaa mimi yangu sio kariakoo ilikua ni ubungo - mwenge nilipokuwa napita kwa gari nilikua napaona karibu kinoma basi siku moja nipo ubungo nataka kuwahi zangu pindi la tution mwenge nikaona nikanyage mguu fasta kama dk 10 tu..

Mdogo mdogo nikaanza kutembea ile nafika usawa wa udsm ndo najua bado kidogo nifike mwenge kumbe wapi..
Nimetembea na jua la saa 8 kali kinoma wakati mimi nimezoea baridi ya mafinga..
Ile kufika mlimani city nimechoka kinoma na jasho linanitoka nikasema ngoja nikazane kidogo ..
Nilotembea tena ki umbali flani nikaona sasa ntapata dehydration bure kwa jinsi jasho lilivyokuwa linanitoka..
Nikaamua kupanda bajaji..

Ile napanda bajaji hata dk 2 hazijapita nimeahafika mwenge...
Ikabidi nitoe hela ya bure
Hahaha.. Ile sehemu mkuu ni pafupi mno ukiwa kwenye gari, sasa jiloge useme unatembea utahisi wamekuloga.. Ni sawa na ubungo mataa kwenda rombo/kibo.. Hapo napo kwa gari pafupi hata dakika haiishi, tembea kama hujataka kulia..
 
Halafu tatizo kubwa ni kwamba tukienda dar huwa tunaaminishwa kila mtu ni kibaka na tapeli kwahio ukijichanganya kuuliza kwa mtu unaibiwa kila kitu
 
Halafu tatizo kubwa ni kwamba tukienda dar huwa tunaaminishwa kila mtu ni kibaka na tapeli kwahio ukijichanganya kuuliza kwa mtu unaibiwa kila kitu
hii hatari sana, tena ukiona tuvijana temenyoa kiduku alafu kamevaa mlegezo unajua kibaka mzoefu kumbe mwema tu, anapambana na stress za maisha au anaongeza confidensi mtaani.
hahahaha
 
Hahaha.. Ile sehemu mkuu ni pafupi mno ukiwa kwenye gari, sasa jiloge useme unatembea utahisi wamekuloga.. Ni sawa na ubungo mataa kwenda rombo/kibo.. Hapo napo kwa gari pafupi hata dakika haiishi, tembea kama hujataka kulia..
Mkuu umesahau na Tabata Matumbi kwenda Buguruni, kwa gari ni dakika 2 tembea sasa... yaani unapaona pale ila kufika sasa lazima ushike kiuno...
 
Hahahaa mimi yangu sio kariakoo ilikua ni ubungo - mwenge nilipokuwa napita kwa gari nilikua napaona karibu kinoma basi siku moja nipo ubungo nataka kuwahi zangu pindi la tution mwenge nikaona nikanyage mguu fasta kama dk 10 tu..

Mdogo mdogo nikaanza kutembea ile nafika usawa wa udsm ndo najua bado kidogo nifike mwenge kumbe wapi..
Nimetembea na jua la saa 8 kali kinoma wakati mimi nimezoea baridi ya mafinga..
Ile kufika mlimani city nimechoka kinoma na jasho linanitoka nikasema ngoja nikazane kidogo ..
Nilotembea tena ki umbali flani nikaona sasa ntapata dehydration bure kwa jinsi jasho lilivyokuwa linanitoka..
Nikaamua kupanda bajaji..

Ile napanda bajaji hata dk 2 hazijapita nimeshafika mwenge...
Ikabidi nitoe hela ya bure
Nyie si wanaume wa mkoani?vipi tena kutembea kipande kidogo namna hiyo kikutoe nishai?
 
Kuzaliwa Dar haimaanishi hupotei kariakoo......
Kuna mwaka niliingia hapo na mama. Ile kuingia chini kurudi juu mara gorofani mara umezama chini tena doh baada ya masaa mawili tushapotea maboya kitambo sema tukabahatika kupaona pale polisi ndo ikawa pona yetu
 
Hahahaa mimi yangu sio kariakoo ilikua ni ubungo - mwenge nilipokuwa napita kwa gari nilikua napaona karibu kinoma basi siku moja nipo ubungo nataka kuwahi zangu pindi la tution mwenge nikaona nikanyage mguu fasta kama dk 10 tu..

Mdogo mdogo nikaanza kutembea ile nafika usawa wa udsm ndo najua bado kidogo nifike mwenge kumbe wapi..
Nimetembea na jua la saa 8 kali kinoma wakati mimi nimezoea baridi ya mafinga..
Ile kufika mlimani city nimechoka kinoma na jasho linanitoka nikasema ngoja nikazane kidogo ..
Nilotembea tena ki umbali flani nikaona sasa ntapata dehydration bure kwa jinsi jasho lilivyokuwa linanitoka..
Nikaamua kupanda bajaji..

Ile napanda bajaji hata dk 2 hazijapita nimeshafika mwenge...
Ikabidi nitoe hela ya bure
nimecheka sana....ungekomaa kwa mguu mkuu hadi ufike mana kuna distance tayari ulkua ushaicover
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom