Amatus Liyumba na Mkewe wagombea mali

Amatus Liyumba na Mkewe wagombea mali

King Kong III

Platinum Member
Joined
Oct 15, 2010
Posts
62,920
Reaction score
95,281
Aliyekuwa Mr.ofisa wa BOT Amatus Liyumba yupo katika timbwili zito na mkewe kwa kugombania hekalu,Liyumba anataka kuiuza lakini mkewe hataki kwhyo sakata limetimba mahakamani.
=======
Source:NIPASHE

Kama picha fulani vilenamkumbuka mh huyu sikuwahi kumjua kwa sura mpaka kesi ya epa lakini nikkiwa form two alivuma sana sana na magari mekundu kwa mabinti huku kadi za gari akibaki nazo mkononi....na si hili tu kuna baadhi waliumia sana kwa kulazimishwa kushuka kwenye gari na kuliachia walipofika kwenye mataa kisa kutokuelewana na mh huyu.

Sasa hili ni lingine linahusu familia pengine wengi wamepitia kwenye shida hii ya kuuza mali za familia; familia ya Amatus Liyumba imefungua kesi ikiongozwa na mkewe Liyumba kusimamisha uuzwaji wa mali za familia...kesi hiyo imefunguliwa wilaya ya Ilala na mkewe aliefunga nae ndoa 1978 mkoani Kilimanjaro.

Kesi hiyo ilitajwa mahakamani hapo jana na ilihairishwa mpaka kesho ambapo mahakama itatoa uamuzi kulingana na kipingamizi kilichowasilishwa na bw Amatus Liyumba.

Mlalamikaji anaitaka mahakama itoe amri ya kumzuia bwn. Liyumba kuuza mali za familia na yeye aendelee kuishi na watoto wake kwenye moja ya nyumba za familia ambazo mh liyumba alileta madalali wa kuiuza huku mama na watoto wakiwa ndani ya nyumba awajui kinachoendelea.

Kesi hiyo iko mbele ya hakimu Jackline Rugemalila mlalamikaji anatetewa na Margareth Ringo.

Hata hivyo mlalamikaji aliwasilisha kiapo mahakamani cha ndoa yao 1978 na kufanikiwa kupata watoto wa nne Lyinda,Jennifer,Priscus na Yulia na wanaishi kwenye nyumba Africa sana Mbezi Beach.

Kiapo kinasema bwn. Liyumba baada ya kutoka mahakamani alirudi nyumbani na kuanza kuuza rangerover 2, landcruiser 2,trekta moja na benzi mbili pamoja na hekari 50, hakuishia hapo akataka kuuanza kuza na mali ya nyumba wanamoisihi.

Mlalamikaji ameomba mahakama kusimamisha swala hili la uuzwaji wa mali za familia.

heee hana kitu tena mpaka anataka kuuza nyumba?
 
Aliyekuwa Mr.ofisa wa BOT Amatus Liyumba yupo katika timbwili zito na mkewe kwa kugombania hekalu,Liyumbaa anataka kuiuza lakini mkewe hataki kwhyo sakata limetimba mahakamani.
=======
Source:NIPASHE

Yasemekana tatizo Amatus hataki kuwaonyesha mafichoni anakoishi na nyumba ndogo kwani alihama Nyumbani kwake pindi alipotoka jela na Hana mawasiliano na mtu hatumii simu ya mkononi wala landline phone .sasa wanafamilia wako wanahofia Nyumba ikiuzwa hawatapata kitu alisikika mkeo akilalamika kituo cha polisi wazo hivyo huenda sakata likachukua sura mpya na kuibua Vioja vingi
 
Waswahili bwana! Labda waganga wamemueleza mke ndio mkosi kwa yaliyompata.
 
Aloo jamaa kiboko, yaani hatumii simu? Ndio kusema hataki tcra wakate kodi yao ya bukubuku kila mwezi?
 
Nilibahatika kukutana na aliyekuwa Deputy Real Estate Manager wa BOT,by then,ambaye alifukuzwa kazi kionevu(kwa mujibu wa mahakama,kwani Mahakama ilimrudisha kazini)na bwana Liyumba na wenzake,anasema kuna siku alikutana uso kwa uso na bwana Amatus,cha kushangaza, ghafla jamaa aligeuza njia na kutokomea..Kweli mwisho wa ubaya ni AIBU!
 
Aisee mwisho wa ubaya aibu
 
Nadhani hili funzo kwa wale wote wanakwapua/fisidi mali ya umma!!
 
Back
Top Bottom