mi nahisi ameamua kufanya kama yule tajiri yesu akamwambia kauze malizako zote ugaie maskini sema atuji tu anaegaiawa ni nani hapaKweli pesa maua...ndo tuseme jamaa kafulia au?
Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
Zamu yake nae kufulia maana alikwiba sasa fedha zinarudi alikozitoa plus laana za madada aliokuwa anawalala ofcourse kwa kiherehere chao cha kudrive na mkwanja faster
Zamu yake nae kufulia maana alikwiba sasa fedha zinarudi alikozitoa plus laana za madada aliokuwa anawalala ofcourse kwa kiherehere chao cha kudrive na mkwanja faster
hao wadada hata kilio chao hakisikiki kwa Mungu maana ni uasherati walifanya. Ukipewa nafasi ukichezea bora unyang'anywe hiyo nafasi. Yanayompata sasa ni haki yake.
Bora marehemu Daudi Balali aliyeko 'peponi' USA!LIYUMBA ANATIA HURUMA SANA ! maisha yake yako kwenye fadhaa kubwa, ana kila kitu maishani bali furaha iliondoka ndani ya moyo wake.
Ha ha ha na wewe ulikuwa jela? haujui kwamba mr red car alishatoka kitambo.
Mkewe na Watoto wanadai Amatus anaishi Mafichoni na kimada yaani Nyumba ndogo hawajui anaishi wapi na Hatumii Mawasiliano ya simu wala e-mail anaishi kama Mullar Omary hivyo kuhofia Anauza Mali zake kwa shinikizo la Vimada huku wakihofia Pia mgao kupotelea kusikojulikana kwani Mkewe anazani mme wake si mwanachama wa TCRA hivyo akisepa na Mkwanja itakuwa issuekama picha fulani vile
namkumbuka mh huyu sikuwahi kumjua kwa sura mpaka kesi ya epa lakini nikkiwa form two alivuma sana sana na magari mekundu kwa mabinti huku kadi za gari akibaki nazo mkononi....na si hili tu kuna baadhi waliumia sana kwa kulazimishwa kushuka kwenye gari na kuliachia walipofika kwenye mataa kisa kutokuelewana na mh huyu
sasa hili ni lingine linahusu familia
pengine wengi wamepitia kwenye shida hii ya kuuza mali za familia;
familia ya amatus lyumba imefungua kesi ikiongozwa na mkewe lyumba kusimamisha uuzwaji wa mali za familia...kesi hiyo imefunguliwa wilaya ya ilala na mkewe aliefunga nae ndoa 1978 mkoani kilimanjaro
kesi hiyo ilitajwa mahakamani hapo jana na ilihairishwa mpaka kesho ambapo mahakama itatoa uamuzi kulingana na kipingamizi kilichowasilishwa na bw amatus liyumba
mlalamikaji anaitaka mahakama itoe amri ya kumzuia bw liyumba kuuza mali za familia na yeye aendelee kuishi na watoto wake kwenye moja ya nyumba za familia ambazo mh lyumba alileta madalali wa kuiuza huku mama na watoto wakiwa ndani ya nyumba awajaui kinachoendelea...
Kesi hiyo iko mbele ya hakimu jackline rugemalila mlalamikaji anatetewa na margareth ringo
hata hivyo mlalamikaji aliwasilisha kiapo mahakamani cha ndoa yao 1978 na kufanikiwa kupata watoto wa nne lyinda,jennifer,priscus, na yulia na wanaishi kwenye nyumba africasana mbezi beach...kiapo kinasema bw liyumba baada ya kutoka mahakamani alirudi nyumban na kuanza kuuza rangerover 2, landcruiser 2,trekta moja na benzi mbili pamoja na hekari 50 akuishia hapo akataka kuuanza kuza na mali ya nyumba wanamoisihi
mlalamikaji ameomba mahakama kusimamisha swala hili la uuzwaji wa mali za familia
Huyu jamaa kumbe ameshatoka lupango, na ile kesi yake ya kukutwa na simu gerezani aliyoitumia kumpigia mkulu wa inji hii imeishaje?yule anajua hana miaka mingi ya kuwa hai, bado ana hela ya kula , kulala, kustarehe na kuhonga, anachofanya Liyumba ni kama wazimu na kutaka kumkomoa mkewe.
maana inadaiwa tangu atoke jela anaishi kwa kimada, sasa hawa vimada hawanaga uchungu na mali za familia......