Wale wa PhD zenu mpaka leo hamjajua kwamba hata 'AMANI ni miongoni mwa haki za RAIA?
🫴 Miongoni mwa haki za kwanza za raia ni; kulindwa au kupewa ulinzi na usalama wa yeye kama raia pili na mali zake
🔹️ Ndio maana kukawa na Jeshi la kulinda nchi na mipaka yake na Jeshi la kulinda usalama wa raia ndani ya nchi [Polisi]
🔹️ Na serikali zote duniani bajeti kubwa iko kwenye usalama wa raia na mali zao.
Hakuna bajeti inafikia bajeti ya Jeshi na Usalama wa nchi.
🔹️ Kipi kinatangulizwa na kipi kinacheleweshwa kwenye hizo haki zote?
Haki ziko nyingi sana za raia ;
🫴 Haki ya usalama[amani]
🫴 Haki ya chakula
🫴 Haki ya matibabu
🫴 Haki ya elimu
🫴 Haki ya kuabudu
🫴 Haki ya kuishi
🫴 Haki ya uraia
🫴 Haki ya kuheshimiwa n.k
Je, msingi wa hizo haki zote ni upi?
Jawabu;
✍️ Ili haki zote hizo zipatikane msingi wake ni 'AMANI au USALAMA' uwepo'
Isipokuwepo hiyo ya msingi(Amani)zote zinapotea;
*Kwenye vita chakula hakipatikani,
*Kwenye vita matibabu hakuna,
*Kwenye vita haki ya kuishi haitakwepo mtakua mnauana tu,
*Kwenye vita shule haziendeki walimu na wanafunzi wako ndani wanaogopa kufa,
*Kwenye vita misikitini na makanisani hakuendeki n.k
Kwahiyo fanya ufanyavyo lazima haki ya msingi ambayo ni usalama[amani] wa mtu na mali zake itakua juu ya zote.
Haki ya usalama haiwezi kukaliwa juu au kutanguliwa na kitu chochote.
Kwakuwa kwenye haki zote hizo huwezi zipata kama hakuna 'AMANI' au 'USALAMA'
🫴 Huwezi kula, huwezi kutibiwa, huwezi kusoma sehemu haina amani kama Sudan na Libya au Congo.
Huwezi kuivunja na kuiondoa haki ya msingi ya amani ambayo ndio inalinda uwepo wa haki zingine kisha utarajie kwamba haki zingine zitatendeka.
🫴 Sasa basi je, kati ya hizo haki zote hapo juu utatanguliza ipi ili zingine zipatikane kwa ufanisi?
Wala huitajii PhD hapo.
Je, hii haki ya amani[ambayo ni usalama wa raia na mali zao] tuiondoe tuache ya mwisho kwanza ili tupate haki ya tume huru na katiba mpya inawezekana?
Kiakili za kawaida tu bila PhD haiwezekani mifano ipo.
🫴 'Sudan na Congo' hakuna chakula, hakuna tume huru, hakuna katiba mpya, hakuna matibabu watu wanajifia kwa kukosa matibabu, hakuna maisha, hakuna shule, hakuna kuabudu kwasababu ile haki ya msingi au kile cha msingi kimekosekana nacho ni 'AMANI'
🔹️ Habari ya kusema msingi wa amani ni haki HAPANA, Ni sawa na mtu kusema msingi wa haki ni haki
Kwasababu hii amani pia ni haki
Zote ni katika haki lakini inatangulizwa yenye msingi wa kuwepo kwa haki zingine.
Kwasababu huwezi kwenda serikalini ukaanza kusema ; nipeni haki yangu, nipeni haki yangu; je ni haki ipi unakusudia upatiwe ⁉
*Je, unakusudia haki ipi ambayo ndio msingi wa àmani?
*Je amani si miongoni mwa haki?
*Je, ni haki ipi ambayo ndio msingi wa haki zote
🔹️Ama ukija na hoja kwamba watu wanatekwa na wengine kuuwawa kwa hiyo haki ya amani na usalama inavunjwa?
Kwanza; Jiulize sababu ya wao kukamtwa na kutekwa au kuuwawa ni nini ⁉ wamefanya nini kwani au kila mtu anatekwa Tanzania?
🫴 Kama usalama wa raia na mali zao Tanzania haupo ...mbona wanatekwa watu fulani tu?
*Mbona sijasikia mwanajeshi au polisi au wanafunzi au masister au walimu katekwa?
Pia kumbuka kwamba; wapo raia ambao wanakusudia kwa dhamira kuiharibu amani ya nchi au usalama wa raia na mali zao
🫴 Sasa hao wakikamatwa au kutekwa au kuwawa kwa ajili ya kulinda raia wengine walio wengi na mali zao huezi sema ni uvunjifu wa amani au usalama
🫴 Mbona wakikamatwa wezi, majambazi au wakauwawa hamlalamiki kwamba haki za raia zinavunjwa na askari wa Tanzania?
🔹️ Kumbukeni kulikuwa na panya road Dar na Tanga kulikuwa na watoto wa ibilisi.
Watu wakawa wanaishi kwa hofu kwa kuhofia usalama wao.
🔹️ Serikali ikawavalia njuga...wakauwawa na wengine kukamatwa na wakafunguliwa mashtaka....mbona hamkulalamika kwamba haki zinavunjwa ⁉
au wale panya road sio raia wa Tanzania au wale walikua Gen z wa Kenya
🫴 Sasa mkiukubali msingi huu wa kulinda amani na usalama wa raia namna hii, lazima pia mkubali utumike kote sio kwa wezi tu na majambazi na panya road.
🫴 Hebu fikiria mtu ni kweli kadhulumiwa ubunge, au kaona ufisadi serikalini, au kaibiwa kura
akifanya jambo la uasi linalopelekea kuvunjika kwa amani aachwe tu asiwajibishwe ⁉
🔹️ Mfano ; Mtu kaibiwa kura kwenye uchaguzi sawa kadhulumiwa; Kisha yeye baada ya kufanyiwa dhulma ile akawa anatamka wazi kwamba askari wauwawe au anashawishi vijana waandamane kufanya uasi dhidi ya serikali je, aachwe?
*Huyu na jambazi au mwizi au panya road wana tofauti gani?
Mbona mnakuwa na nyuso mbili tofauti 🫷🖐👀👀👀✍️