Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 58,636
- 220,437
Kuna bwana mmoja alioa mchumba wa kutokea shuleni. Walipendana sana, walifanikiwa kupata mtoto mmoja wa kike kabla maradhi kumfika yule mama na alifariki. Yule bwana aliachwa na binti wa miaka minne. Aliamua kuto kuoa mpaka mwanae akue. Aliajiri housekeeper wa kuja saa mbili na kuondoka saa 10 jioni akiwa amesha wapikia chakula cha jioni.
Maisha yalikwenda mpaka binti alipata usajili wa chuo kikuu. Alimuacha baba nyumbani mwenyewe. Baba aliona huu ndiyo muda wa kutafuta mwenza. Baba alimtaarifu binti mipango yake ya ndoa. Baada ya harusi binti alirudi chuoni na wana ndoa kuendelea na maisha.
Binti amerudi nyumbani alikuta mama wa kambo amebadili meza ya kulia chakula na sofa. Yule binti aliwaka kwa hasira kuwa kumbu kumbu ya mama yake imepotezwa. Ugomvi ulikuwa mkubwa binti aliapa hatarudi tena nyumbani. Ile hali ilimsononesha sana baba yake.
Baada ya muda yule bwana maradhi yalimfika. Binti alitaarifiwa, alisema atakwenda hospitali muda ambao yule mama hatakuwepo. Hapa mke ndiye muuguzaji. Yule bwana alikuwa na masononeko sana. Anampenda sana binti yake na anampenda sana mke wake.
Ndugu waliingilia kati, kikao kiliitishwa na mama na mtoto waliweza kupatana. Siku ile mgonjwa alipata nafuu ya ajabu. Aliweza kula vizuri na hali yake ilianza kuwa nzuri. Alikaa na mke wake na binti yake na kujadili mirathi yake.
Miezi sita baadae alifikwa na mauti lakini alikufa akiwa na amani moyoni.