Ama kweli watanzania tumelogwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ama kweli watanzania tumelogwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mayoscissors, Mar 4, 2012.

 1. mayoscissors

  mayoscissors JF-Expert Member

  #1
  Mar 4, 2012
  Joined: Nov 24, 2009
  Messages: 762
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Watanzania wenzangu mgomo wa madaktari kama ukija kutokea kwa mara ya pili kwani mimi siamini,lazima tujilaumu wote kwani wewe na mimi tuna nafasi ya kutetea lile ambalo ni la maslahi ya watanzania na nchi yetu.
  Ugonjwa hamna mtu anayeomba augue na hamna mtu anayeweza kujihakikishia hataweza kupata ajali hivyo mgomo unakuhusu na unanihusu kwani kwa namna moja au nyigine unaweza ukajikuta unapoteza maisha wakati leo watanzania tuna nafasi ya kuiambia serikali iwaweke pembeni Waziri wa afya na naibu wake ili mchakato wa meza ya makubaliano kati ya madaktari na serikali uendelee
  Watanzania wenzangu tuwe na ujasiri wa kuisemea serilkali pale inapokosea,swala la mgomo likitokea tena kwa serilaki kulindana nitajilaumu sana na nitakulaumu kama serikali hatutaisemea kama Waziri wa afaya na naibu wake watakuwa ofisini watanzania tukipoteza maisha jumatano ijayo
  MUNGU IBARIKI TANZANIA
   
 2. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #2
  Mar 4, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Ndugu zangu madaktari chonde chonde safari hii kuweni wastahimilivu kidogo kuokoa maisha ya watanzania. JK ame prove kuwa ni rais asiye msikivu, sana sana utasikia jumatatu au jumanne ameenda zake Uingereza kwa best yake David Cameron na yote yatakayotokea hatakuwepo nchini.

  SULUHISHO: Mtuamuru sisi waTanzania tuandamane kwenda kuwatoa kwa NGUVU OFISINI Mponda na Naibu wake ili mambo yaishe. Hakuna aliyetegemea baada ya mateso yale waliyopata watanzania serikali ingechelea kutekeleza madai yao na hata madaktari kuamua kugoma tena, hasa dai rahisi kabisa la waziri kujiuzuru.
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Mar 4, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Umeongea vizuri sana mkuu. Nadhani mwangwi wa sauti yako itakua imefika mpaka pale dirishani kwake Mkuu wetu, wa sasa kwa mujibu na matakwa ya sheria, pale Magogoni.

  Kuna mabadiliko yako njiani kwa kuitikia hiyo sauti yako ya upole na unyenyekevu.
   
 4. Ndokeji

  Ndokeji JF-Expert Member

  #4
  Mar 4, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 525
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  mkuu umetoa ushauri mzuri sana wenye mantiki. Maana madactari wanapogoma watu tunashangili wale tuliowazima bila kuchukua hatua yoyote huku wagonjwa tunaumia .
   
 5. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #5
  Mar 4, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Yuko wapi Ananilea Nkya na Deus Kibamba? mnaotaka kuandamana andamaneni mimi nabaki nyumbani, lakini kwa upande wangu nawaomba madaktari wawe na uvumilivu maana si wao tu wenye madai serikalini. Watambue kuwa watumishi wa serikali wako wengi na wote wana umuhimu katika nafasi zao je nao wakigoma itakuwaje? inawezekana wao hawana ndugu wanaohitaji tiba au wataweza kuwatibu katika zahanati zao binafsi au wanazofanya kazi part time lakini naye mwalimu akigoma wajue kuwa watoto wao hawatafundishwa, Polisi wakigoma pia watavamiwa na hata hayo madai yao hawatanufaika nayo. Ni takribani watumishi wote nchini wana madai sawa na madaktari iweje wao ambao tena serikali imeshaahidi kuyashughulikia wanaendelea kutishia tu? wafanyeje wale ambao hata kukutana na Pinda hawajawahi?
   
 6. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #6
  Mar 4, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Haiingii akilini kumtaka Mwalimu akaandamane ili Daktari atimiziwe madai yake wakati na yeye ana madai pia.
   
 7. Dr. Wansegamila

  Dr. Wansegamila JF-Expert Member

  #7
  Mar 4, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 1,233
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  jamani hii logic mnayoitumia mimi siielewi kabisa, eti mbona walimu nao wana madai hawagomi...... Ooh mbona mapolisi nao wana maslahi duni hawagomi............ So whaaat???kama wao wanaridhika au ni waoga haijustify kwamba madokta nao wawe waoga. Au unataka tuongeze na madai ya walimu,mapolisi,etc kwenye madai yetu? Msitulazimishe madokta na sisi tuwe waoga waoga. Aluta continua
   
 8. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #8
  Mar 4, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Wewe si mmoja wa mafisadi wa nchi hii, unadhani hatukujui? Wacha watu wadai haki zao. Sasa ni madaktari na siku nyingine watagoma wengine.

  Endelea kulala na wala hatukuhitaji!
   
 9. K-killer

  K-killer Senior Member

  #9
  Mar 4, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 143
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wacha kuongea utumbo wewe! Kwani kukutana na pinda ndo ku solve tatizo,issue ni kwamba matakwa yao yAtekelezwe,hatA kama huyo pinda Angebaki ofisini kwake au nyumbAni lakini idimrAdi etekeleze mAtakwa yote yA madaktari,hamna mtu anayehitaji kuonana nae,itasaidia nini?

  UmepAtia kusemA karibu kila sector kunA matatizo,sAsa unAwAsihi madaktari wasigome kwasababu hao wengine hawAgomi,MAdAktari wamefunguka macho.HAtA wote wakigoma ni sAwa tuu,hii inAdhihirisha serikali imeshindwA mAjukumu yake.

  Nawakilisha
   
 10. kichwat

  kichwat JF-Expert Member

  #10
  Mar 4, 2012
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 1,824
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  kuna Mtanzania alisema 'nchi haiendeshwi kwa mitandao ya kijamii' ...time to prove otherwise? Time will tell.
   
 11. kichwat

  kichwat JF-Expert Member

  #11
  Mar 4, 2012
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 1,824
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  ndugu K-killer yaani unamaanisha kama kuna nyani wamevamia shamba lako la mahindi usichukue hatua sababu eti mashamba ya jirani zako nayo yameliwa. Nadhani ni mtazamo wa kijuha.
   
Loading...