Walipoingia bungeni mara baada ya uchaguzi mkuu, walipojiona wamepata wabunge wa kuridhisha kidogo, walikataa kuunda baraza la upinzani la mawaziri pamoja na CUF na vyama vingine vyote. Sasa wameona kwamba wameporomoka ki siasa baada ya kuleta ubaguzi wa kufukuza wale wenye mawazo tofauti na Mbowe, wameona wajiunge na UKAWA si kwa lengo la kupata katiba ya wananchi kama walivyodai, bali sasa wamekuja ni huu utapeli mpya wa kujifanya kwamba Mbowe atavunja baraza lake na kuliunda upya, akishirikisha UKAWA na eti atawaacha MREMA, CHEYO na wale ambao hawajawasapoti! Hivi huyu Mbowe anatufanya wa TZ hatuna akili? Huu si ni utapeli mpya! Mods msiunganishe na pls msiufute uzi hii watu wachangie bila matusi.