Am psychologically affected, nifanyeje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Am psychologically affected, nifanyeje?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by TINGA TINGA, Jun 14, 2011.

 1. T

  TINGA TINGA New Member

  #1
  Jun 14, 2011
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari wana JF,
  Siku hizi, japo kuna imani za kidini kuna wanaoamini kuwa ni vigumu kufunga pingu za maisha bila kuonja tamu ya asali. Siku zote Mimi nimekuwa miongoni mwa wanaopingana na huu mtazamo. Nimeishi maisha yangu yote kwa misingi ya malezi bora ya wazazi wangu na imani yangu kuwa ni marufuku kufanya hivyo mpaka siku hiyo maalum kwa baraka zote za mwenyezi Mungu. Nikatenda yote na nikafanya kweli, nikampata nimpendaye naye akawa na msimamo kuwa hakuna kuonja mpaka siku yenyewe. Nilivyompenda sikuwa na jinsi nikajikaza kiume mpaka siku hiyo.

  Siku ikafika, na kila mmoja akafurahi. Muda ukafika wa kupata mtoto. Kadiri siku zilivyoenda nikagundua mapenzi yanahama slow but surely kutoka kwangu kwenda kwa mtoto. Nikajaribu kukaa na mwenzangu na kujaribu kumweleza hisia zangu, nikamweleza pia kuwa huwa ninafurahi tuwapo uwanjani ningependa A, B, C, ............ Nikajikuta napigwa maswali kibao, oooh, umepata kujua wapi hayo, hizo style umepata wapi, umejifunza wapi. Duh jamani nikajaribu kumweleza ukweli lakini hanielewi. Hataki hata kuona nikiwa na CD ya mambo yale, tukiangalia TV hata tukiwa wawili tuu, akiona picha/movie inayomwonyesha msichana nusu uchi, au mashindano ya miss, anasema nibadili channel, tukiwa uwanjani hawezi kwenda zaidi ya mara moja, tena hunitangulia dk chache tuu kashamaliza, then ananiambia nimalize tuu kashachoka (tena kabla yangu mimi mwanaume, wakati mimi namfanyia kila kitu) na hataki manjonjo, kulamba koni hawezi. I can stay even a month hata hatujakutana na yeye hajali anamaind kazi zake na majukumu tuu.

  Ukweli baada ya muda nikajikuta nimeruka ukuta, na nilichokuta huko sina hamu tena ya kurudi ndani. Ukweli ninajikuta mtu wa mawazo tuu niko dillema niendelee kutoka nje (pia naogopa) na nisipotoka najiona highly stressed.
   
 2. Konakali

  Konakali JF-Expert Member

  #2
  Jun 14, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Hapo red, ufafanue vema...! Maana huenda hujajua unachosema....!
   
 3. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #3
  Jun 14, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Unless unataka ukaribu na mke wako uendelee kupotea mpaka uishe kabisa endelea kutoka nje.Kutoka nje hakutombadilisha mkeo...kadri utakavyoonyesha humhitaji tena ndivyo na yeye atazidi kusogoea mbali na wewe.Mwisho mtaishia kuwa wanandoa kwa jina tu na sio vitendo!!Umesema mwanzoni wote mlikua mnafurahia kwahiyo anavyofanya sasa hivi sivyo alivyo.Kwanza tambua kwamba kwa baadhi ya wanawake kufocus kwa mtoto tu pindi anapompata ni jambo la kawaida.Sijui wenyewe mnaishije ila kibongo bongo naweza hisi malezi yote umemwachia yeye tu au yeye na dada wa kazi kama mnae.Hata usiku ye akiamka we unaendelea kuuchapa usingizi wakati mwenzako anahangaika kumlisha/nyonyesha/bembeleza mtoto arudi kulala.Hii inaongeza yeye kutokukujali wewe kwasababu we humjali yeye anavyohangaika na kumsaidia wala humjali mtoto kwa kujitolea kumwangalia every now and then kwahiyo yeyeanamjali kwaajili yenu wote.Sasa badala ya kumlalamikia kwamba sijui kabadilika na kumtaka katika hali uliyozoea na kuipenda msaidie kuirudisha kwa matendo.Anza kwa kumsaidia na mtoto...hata kama mna dada wa kazi badala ya wewe kuangalia mtoto anavyolishwa huku akili iko kwenye tv anza kusaidia kumlisha...kumbembeleza akiwa analia...kumlaza...kumwangalia usiku akishtuka.Ukisikia mwenzako anaamka akamwangalie mwambie “pumzika mama mi ntamwangalia“.Jitahidi kuwa karibu na mtoto ili uwe karibu na mama.Mwenyewe atakapoona nguvu zake zote hazihitaji kwenda kwa mtoto kwasababu na wewe una‘chip in‘ ataanza kurudisha focus kwako taratibu!Usimlazimishe...usimwambie abadilike wala usilalamike.Kua bega lake akihitaji kuegemea sehemu...kua msaada wake anapouhitaji utashangaa mwenyewe kama hata mapenzi hayataongezeka!!Kila la kheri na acha kabisa kutoka nje ya ndoa yako kabla hujamletea mkeo UKIMWI ndani mkaacha mtoto yatima!!
   
 4. T

  TINGA TINGA New Member

  #4
  Jun 14, 2011
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wee Lizzy, nisaidie mpaka wapi? nafua, napika alipokuwa mjamzito nadeki, usiku nambadilisha mtoto akijichafua sasa nisaidieje? Ok. otherwise good advise, ila hapo bado haijakaa sawa mpaka nifanyaje ndo aelewe.
   
 5. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #5
  Jun 14, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kumbe unasaidia?!Nwy niambie wakati unasaidia yeye anafanya nini?!Hua anashukuru au hata ku-acknowedge kwamba umefanya kitu ndani ya nyumba?!Ana furaha?!
   
 6. T

  Tall JF-Expert Member

  #6
  Jun 14, 2011
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  pole sana,maisha ndivyo yalivyo.
   
 7. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #7
  Jun 14, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,280
  Likes Received: 1,720
  Trophy Points: 280
  Pole sana kaka yangu. Nashukuru kuwa dhambi ya kutoka nje ya ndoa imeanza kukusumbua na hiyo ni dalili kuwa unataka kusitisha hiyo tabia mbaya. I wish I could help. Mtoto wenu ana umri gani? Jitahidi kumrudisha wife kwenye hali yake ya zamani, mimi mwanamke najua mabadiliko ya kuwa mama yana wapa shork wanawake wengi na wanaume wanashindwa kutoa ushirikiano ili mama aweze ku adjust. Jaribu kutafuta watu mnaowaamini (watu wazima) wamuweke chini wamsomeshe. Ila sidhani kama itakuwa ok ku confess kuwa unacheat. Cha kueleza waambie hao watu wazima hata matron wa ndoa yenu au wazee wa kanisa kuwa unahisi uzalendo unakaribia kukushinda kwa sababu wife amechange. Wao watamueleza na kumkanya kuwa tabia yake inahatarisha ndoa, nadhani atawaelewa. Kaka vimada si watu unahatarisha maisha yako, ya mke wako na wanao kwani watabaki yatima na kuongeza mizigo kwa ndugu zako kukulelea wanao siku za usoni pale wewe na mkeo mtakapokufa na HIV. Nakusihi sana jaribu kila uwezalo kusolve hili tatizo.

  Nasikia uchungu kwani nimeshaona yatima wengi sana wanateseka sababu ya ubinafsi wa wazazi wao.
   
 8. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #8
  Jun 14, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,025
  Likes Received: 743
  Trophy Points: 280
  Pole mkuu,acha ka mchezo hako ka kuruka ukuta,kama ni kweli,muweke sawa bibie atatulia tu.
   
 9. Tulizo

  Tulizo JF-Expert Member

  #9
  Jun 14, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 849
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Nadhani unasumbuliwa na guilty conscience ambayo inakula moyo wako kwa kuruka ukuta.. kwa haraka nahisi ume exaggerate issue ya mke wako ili uhalalishe tabia yako chafu...soma vizuri ujumbe wa Lizzy hapo juu..utakufa na kuwaacha watoto wako yatima kwa tamaa zako za mwili...
   
 10. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #10
  Jun 14, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Pole sana lakini jirekebishe na usirudie kuruka ukuta tena
  mara nyingi ni kawaida ya akina mama kuwa karibu na mtoto hasa anapokuwa katika umri mdogo
  unahitaji kuchukuliana naye na ujenge ukaribu zaidi katika yote
  ukiwa mbali naye unamuweka katika mazingira maguma zaidi na ataathirika kisaikolojia kuliko wewe
   
 11. TECHMAN

  TECHMAN JF-Expert Member

  #11
  Jun 14, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 2,677
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 160
  kutokana na maelezo uliyotoa, tatizo kwa mwanamke huyo linatokana na malezi, hilo linagusa upande wako pia.
  1. Umesema kuwa mkeo hajawahi kushiriki na mwanaume yeyote kabla yako, hilo ni jema, lakini je? Alijengewa mtanzamo gani kuhusu mwanaume na tendo la ndoa? Inawezekana kuna upotoshaji aliofundishwa wakati akikuwa ambao umemuathiri kiufahamu. Jambo hili hotokea sana kwa jamii nyingi (sio zote) ambazo zimeshika dini sana, kiasi msichana anaona tendo la ndoa nikama uchafu nahii inamuathiri mpaka akiwa ndani ya ndoa( kuna wanawake hawawezi hata kushika kwa mkono sehemu za siri za waume zao).

  2. Wewe mwazo uliona kila kitu ni sawa kwa kuwa hukuwaunajua tofauti, Hii ni kutokana na malezi na makuzi uliyopitia, baada ya muda ukaanza kuzoea na kufanya utafiti pamoja na mazungumzo ya marafiki jinsi wanavyofanyiwa na wapenzi wao pamoja na kuangalia picha za X kama maelezo yako yalivyo, kilichofuata ukaona tofauti kati ya mke wako na hayo uliyasikia na kuyaona.

  SULUHISHO.

  Tatizo mlilo nalo ni tatizo la kiufahamu. kaa chini na mwezio jaribu kuongea nae ( hakikisha yuko katika mood nzuri ikiwezekana mtoe out sehemu ya kutuliza akili kisha ongea.
  AU mnaweza kutafuta mtaalamu wa ushauri mwende wote pamoja kisha kila mtu aeleze shida yake.
   
 12. LD

  LD JF-Expert Member

  #12
  Jun 14, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Dah, hii taasisi ya ndoa ngumu. Zingatia ushauri unaopewa humu ukichanganya na zako. Maisha yataendelea. Nyumba ndogo ni hatari kwa afya yako.
   
 13. SaidAlly

  SaidAlly JF-Expert Member

  #13
  Jun 14, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 1,806
  Likes Received: 648
  Trophy Points: 280
  Ahaaaaa.....umeona sasa umuhimu wa kutest ZALI mapema?? Ndio hapo ujue dunia sasa imebadirika, ukitaka kuishi kama uko kwenye karne ya 11 wakati sasa tunazungumzia sayansi, teknolojia na utandawazi huwezi kwepa hizo changamoto za kileo na ndio maana umegundua mambo ya kulamba koni, kuruka ukuta na usipoangalia utaruka mpaka PAA la nyumba kisha watu wakushangae na utu uzima wako kufanya mambo hayo, kwa kizazi cha sasa MAUJANJA yote wenzio humaliza katika foolish age kwahiyo anapokuja kwenye commitment ya ndoa anakua amefanya selection sahihi na hategemei kukwazika ktk MIUNDO MBINU labda tu awe KICHECHE hajaridhika. Ushauri wangu Brother ni kujitahidi kumuelimisha taratibu akuelewe na mambo mengine umzoeshe kiaina taratibu na utani mwingi ili kuzuia hasira na kichapo kisha atazoea na kuona TAMU ya ASALI.Ikishindikana Bro basi vumilia ndio shida na raha hizo ulizo ahidi kuzivumilia siku ile ulipo utangazia Umma mbele ya Ushahidi wa Kiongozi wa Dini kwamba uko tayali kuya vumilia. Tena hata kama ni Muislam, usithubutu kuoa mwingine wa pili kwa sababu hizo maana lengo la ndoa ya pili si kwa matatizo ya ndoa ya kwanza. Ndoa Haita Swihi!Pole Mkuu ndio Kidunia.
   
 14. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #14
  Jun 14, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  Piga goti mbele ya Mungu wako ili aokoe ndoa yako!
   
 15. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #15
  Jun 15, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Mpeleke kwa bi fatma apewe somo la ndoa.... pole kwa masahibu, hiyo huwatokea sana wanaume tupatapo watoto na kuona kuwa kama tumewatenga sababu kabla kulikuwa hakuna mtoto it was just the two of you guys, alipokuja mtoto katika hali yoyote ile mama lazima mawazo yahame kule, kuhusu mkeo kukuboa kunako sita kwa sita hiyo ni kawaida kwa baadhi ya wadada hasa wale waliolelewa kwa maadili ya kidini, kwao kila kitu ni dhambi

  Hivo unatakiwa uwe muwazi kwake, mwambie una mazungumzo nae, mtoe out kabisa na mtoto mumuwache home, mwambie unakumbuka jinsi mapenzi yenu yalivoanza na mpaka sasa unahisi kuna kitu kimepungua sana kiasi unapata msongo wa mawazo, kuwa muwazi kabisa na umaanishe unachomwambia kwa kumwangalia usoni bila aibu, mwisho mwambie unapenda abadilike na wewe pia ubadilike ili ingalau mkutane katikati na kuridhishana kwa namna yoyote

  Mwisho kabisa nahisi huyo mkeo kwa vile hakuwa anafanya mapenzi before, bado hujamfikisha kabisa kwenye mahaba yenyewe, kwa hiyo tendo zima analiona kero tu, sidhani kama anakuwa amemaliza kama unavosema maana kwa hali halisi kabisa mwanamke kuwahihivo kabla yako mara kwa mara si jambo la kawaida, anafanya hivo sababu anaona kero, nakushauri nunua vitabu soma, google pia ili upate hints za mambo ya kuridhishana nahisi haya yanatosha
   
 16. dadam

  dadam Member

  #16
  Jun 15, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole asana kwa yaliyo kusibu..jitahidi uonane na psychologist wa mambo ya mahusiano mapenzi na ndoa. siku huzi wapo wengi na wanasaidia sana.
   
Loading...