Alshabaab finally admits

Sammuel999

JF-Expert Member
Jun 1, 2016
3,481
2,347
Screenshot_2016-06-17-22-10-34.png
Screenshot_2016-06-17-22-10-41.png
 

Sura yenyewe inakaa kama sokwe fulani hivi, hata akitabasamu watoto wanamtoroka. Jamaa kamwaga damu sana huyu kisa eti anapigania dini.
Kuna wakati huwa nakaa nakuwaza hivi hii dunia tatizo nini, tunauana miaka baada ya miaka, tangu jadi watu wanauana hata leo hii binadamu wanasakana na kuchinjana. Kila mtu anatoa vijisababu bila mashiko, mara dini, ukabila, ushirikina, rangi ya ngozi n.k. Kuchinjana tu, kukatana vichwa, risasi, mabomu jameni ifike wote tusitishe na kujiuliza nani hatorudi kwenye ardhi na kuwa mavumbi.

Huwa inaniuma sana nikiona jinsi wakimbizi wanahangaika wakiitoroka nchi yao ya Syria, watu walioishi kama ndugu, tena dini moja.
Akina Hitler waliuwa mamilioni lakini hawapo leo.

Sasa huyu hapa na bunduki yake hiyo kaiacha dunia, aliikuta na ameiacha hata baada ya kuchinja watu. Hakuna mbabe asiyeonja kifo, utakwenda tu. Mamako atapanua miguu uzaliwe, unyonyeshwe, ukue na kubadilika na kuwa zombi na kuanza kuwaua watu, hatimaye utaenda na kuacha mother earth jinsi uliikuta.
 
Back
Top Bottom