Ally Pugi Hatunaye tena | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ally Pugi Hatunaye tena

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tiba, Jun 12, 2010.

 1. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #1
  Jun 12, 2010
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Wana JF,

  Taarifa nilizozipata muda si mrefu zinasema kwamba mwanamuziki mwimbaji maarufu wa muziki wa dansi Ally Pugi amefariki dunia usiku wa kuamkia jana (12/6/2010) huko Morogoro alikokuwa amekwenda kusalimia ndugu zake. Marehemu Ally ambaye mpaka wakati kifo kinamkuta alikuwa mwimbaji wa bendi ya BRC (Bendi ambayo uwa inatumbuiza pale Port View siku ya Ijumaa) alikuwa akifanya shughuli za Muziki huko nchini Botswana kabla ya kujiunga na BRC January 2009. Marehemu Ally tayari amezikwa huko huko Morogoro.

  RIP Ally.

  Tiba
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Jun 13, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Poleni kwa msiba.. Mungu ailaze roho yake pema peponi amen.
   
 3. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #3
  Jun 13, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  RIP Ally Pugi, almaarufu Ally Baba kwa huku Botswana, tutakumiss sana, memeory zako haziwezi kufutika hasa ulipokuwaga jukwaani ndani ya ZEBRAS,
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  Jun 13, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,578
  Likes Received: 18,524
  Trophy Points: 280
  RIP. Aliy Pugi
   
 5. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #5
  Jun 13, 2010
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mkuu Kituko,

  Kwa sisi tuliopata nafasi ya kuwa naye karibu, kwa kweli alikuwa ni muimbaji mahiri. Mimi nilimpenda sana na hasa alipokuwa anaimba wimbo wa "Kinyonga". Ilikuwa ni lazima nikamtuze. Anyway yeye katangulia na wengine tunafuata!!!!

  Tiba
   
 6. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #6
  Jun 13, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  pole na wewe pia Bw Tiba kwa kuondokewa na mtu wako wa karibu
  na mimi huyo jamaa alikuwa wa karibu sana, nilianza kumfahamu alipokuwa pale Knondoni Mkoko alipokuwa anapiga na Bantu group, niliishi nae pia pale Gaborone akiwa na Marehemu Abdalah "Dogodogo", Shaban "Wanted", Gregory, Maliki Star na baadae Kupaza na nilikuwa nae mwezi wa tatu this yr hapo Dar Pale maeneo ya MAwenzi Tabata walikuwa wanapiga pale,
   
Loading...