Ally Bananga: Mdude Nyagali anatakiwa kupumzika kwanza, kumpatia kipaza sauti mapema sioni tukimpenda na kumsaidia

Linguistic

JF-Expert Member
Mar 16, 2021
3,671
8,237
Am speechless
Tulilia wengi alipoteseka gerezani
Tulihuzunika sana alipolazimishiwa makosa ya uongo ili apotezwe.
Tumepigana wengi Mdude chadema kuwa huru.
Alipotoka jela alistahili yafuatayo;

1-Akaione familia yake akae nayo kwa muda
2-Apata physician amfanyie check up ya afya yake kwa kina (muda aliokaa gerezani ni mwingi sana).
3-Apatikane psychologist akae nae kumjenga kisaikolojia ili akitoka kuingia kwenye harakati aingie akiwa imara kimwili, kiakili na kimaono.

Kuendelea kumpatia kipaza sauti mapema haya SIONI TUNACHOJENGA, SIONI TUKIMSAIDIA, SIONI TUKIMPENDA MDUDE!

Sio lazima mnielewe na sio lazima mfanye hili ila TUFIKIRIE MAUMIVU TULIYOPITIA KAMA TUNA UTAYARI WA KUYAPOKEA TENA.

Alitufunza Mkiti freeman mbowetz kwamba tuyakatae mauti, tuivuke mitego inayotegwa kwetu kuturudisha nyuma maana hakuna faida kufa ama kusota jela. Tutapoteza muda wa kujenga chama kwa ajili ya kupigania walio jela, tutapoteza rasilimali watu kama tutakufa, tazama leo hakuna Alphonce Mawazo tena. Tutampata wapi Mawazo? Familia yake itampata wapi mwingine?

Ni muda wa kufikiri aina ya harakati zetu towards...... Bora kuwa mkimbizi uanzishie mashambilizi ukiwa mahali ambapo hata mbu hakung'ati kuliko kujitoa muhanga hivi ukiwa huna uhakika wa KUSOMA ULICHOANDIKA!

Msimamo huu ni wangu, usipoupenda uheshimu wa kwako.
 
Yuko sahihi! Mdude anastahili muda wa kupumzika kabla ya kuendelea na harakati zake. Lakini pia ni wakati wake sasa kuwa makini.

Masuala ya kukubali hela za malaya uliyekutana naye kwenye mitandao, halafu anakuja kukuwekea madawa ya kulevya ndani ya geto lako, ni uzembe wa kujitakia.
 
..hicho anachopendekeza ali bananga labda kinawezekana ktk awamu hii ya rais samia suluhu.

..wakati wa rais magufuli walikuwepo wakina joseph selasini, james mbatia, prof.lipumba,...ambao walikuwa na mtizamo kama wa ali bananga lakini bado hila na ukatili wa ccm dhidi yao zilikuwa palepale.
 
Bananga anataka kusema Mdude alikuwa mgonjwa wa akili kabla hajapelekwa jela? au amekuwa mgonjwa wa akili baada ya kutoka jela?

Mdude jana hakumtukana Rais, ni kauli aliyoitoa ndio imeonekana kuwashangaza/shtua wengi, japo nina hakika wengi wenu mkiambiwa muoneshe tusi kwenye ile kauli hamtaweza, mnatumia hisia zaidi kuhukumu.

Mmekuwa mkifikiria hili jambo kwa upande mmoja tu, kwanini hamfikirii na mateso aliyopitia Mdude akiwa gerezani muda wote huo kwa makosa ya kubambikiwa?

Nae ni binadamu, ana hisia, muacheni atoe frustrations zake, badala ya kusema akajifungie ndani huku sheria za nchi zikiendelea kuvunjwa, na mvunjaji ndio mnamlinda kama malaika, mnamvimbisha kichwa azidi kujisahau aendelee kufanya apendavyo.

Ikulu ni ofisi ya umma, na yeyote anaekaa pale ana jukumu la kuwatumikia wananchi bila kujali itikadi zao, usawa na haki viwepo kwa wote, akijisahau kwa hilo ni lazima akumbushwe, mahaba yenu kwa "mama" yatazidi kumuharibu, amkeni.
 
Back
Top Bottom