All about ALPHA BLONDY

All about ALPHA BLONDY

Analyse

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2014
Posts
17,641
Reaction score
47,660
Jina la Kamili: Seydou Koné
Jina la kisanii: Alpha Blondy
Nchi: Ivory Coast

Alizaliwa :1 Januari 1953 ( miaka 62 kwasasa) Dimbokoro, Ivory Coast
Aina ya muziki : Raggae
Kazi yake : Muimbaji, Mtungaji
Miaka ya kazi:1982 - Mpaka leo


Alpha Blondy mara nyingi huimba kwa lugha ya KIDIOULA ambayo ndio lugha yake ya taifa huku akichanganya Kifaransa na Kiingereza , Lakini pia wakati mwingine huimba kwa Kiarabu au Kiyahudi. Mashairi yake yanamaanisha siasa kali yenye mwelekeo na uchangamfu.

MAISHA YA MWANZO:

Alpha ni mtoto wa kwanza katika familia ya watoto tisa. Alilelewa na bibi yake mzaa mama.

Mnamo mwaka 1962, Alpha Blondy alikwenda kukaa na baba yake aliyekuwa anaishi mjini Odienne, Ambapo alikaa kwa muda wa miaka kumi, Baadae akijiunga na shule ya Sainte Elisabeth high school, na kujishughulisha na makundi ya wanafunzi ya Ivory Coast. Hapo ndipo alipo unda bendi. Ingawaje, Upenzi huu uliathiri masomo yake na baadae Blondy alikufukuzwa shule kutokana na maudhulio mabovu shuleni.

Wazazi wake Alpha wakampleka mtoto wao aAplha kusomea lugha ya Kiingereza mjini Monrovia, mji mkuu wa nchi jirani ya Liberia mnamo mwaka 1973. Huko Alikaa kwa muda wa mwaka mmoja na mwezi mmoja kisha akahamia nchini Marekani kwa kuongozea taaluma yake zaidi.

MAISHA YAKE MAREKANI:

Mnamo mwaka 1973 Alpha amehamia mjini New York (Pia aliishi kidogo Texas), ni mahali alipomalizia chuo na aliegemea sana kwenye Kiingereza, Kwasabu toka mwanzo alikuwa anataka kuwa mwalimu wa lugha ya Kiingereza.

Alifanya kazi kwa juhudi zote,wakati mwingine hadi usiku,hadi kuna kipindi anakuwa mgonjwa. Akiwa New York alikutana na Marastafari kwa mara ya kwanza, Pia alikuwa na uwezo wa kuangalia matamasha ya wanamuziki wa kijamaica kama kina Burning Spear n.k. Wakati huo yeye alikuwa akirekodi nyimbo za kikristo lakini hakuthubutu kuacha kuandika nyimbo zake mwenyewe.

Kwa bahati alikuwa akidodosa sehemu mabalimbali za mjini New York na baade kurudi kidogo nchini Ivory Coast, Ambako alipata matatizo saana mpaka alivyokuja kukutana rafiki yake waliokuwa wote toka utoto, Fulgence Kassi, Ambaye baadae alikuja kuwa mtayarishaji maarufu wa vipindi vya televisheni. Hapo ndipo alipoanza kuonekana kama kazi yake kweli ni uimbaji, na kutumia jina la 'Alpha Blondy'.

IMANI YAKE:

Alpha Blondy alizaliwa na Mama Mkristu pamoja na Baba Muislam,ila alilelewa na Bibi yake ambaye alimfundisha kumpenda kila mtu.Alpha Blondy aliheshimu dini zote,na kiimani alikuwa na mafunzo ya dini zote mbili,na hata ukiskiliza wimbo wake wa "God iz One" au pia "Jerusalem" ambao alikuwa anazungumzia umoja kati ya dini zote mnamo mwaka 1986.

NYIMBO MAARUFU:

Nyimbo ya kwanza kumpa mafanikio ilikuwa Brigadier Sabare. ni moja kati ya nyimbo zenye ujumbe:

*Jah Glory - Hii aliimba juu ya upigaji vita umaskini.

*Apartheid is Nazism

*Brigadier Sabare - Nyimbo ilihusu ukatili wa maaskari.

*Cocody Rock - Hii ilikuja kuwa ndio kama nyimbo yake ya taifa kila mtu anajua kuiimba.

*Guerre Civile - Hii ilihusu masuala ya vita ya wenyewe kwa wenyewe.

*Jerusalem- Hii ilataka amani nchini israel. Nyimbo inaanza na maneno yanatumiwa katika sara za kiyahudi, Hivyo aliaza kiyahudi.

*Journalistes en danger - Hii ilihusu mauaji ya Norbert Zongo aliyekuwa mchapishaji na mhriri wa gazeti la Independent la nchini Burkina Faso.

*Politiqui - Hii ilihusu uraia.

*Yitzhak Rabin -Hii iliandikwa mwaka 1995 kutokana na mauaji ya Waziri Mkuu wa Israel Yitzhak Rabin.Huu wimbo ilikuwa ni kama dedication

*Sweet Fanta Diallo

*Téré

*Blesser

*Rasta Poué

*Rendez vous

*Mystic Night Move


ALBUM ALIZOTOA:

1982: Jah Glory

1984: Cocody Rock!!!

1985: Apartheid Is Nazism

1986: Jerusalem (Alpha Blondy album)|Jerusalem (Akiwa na Wailers Band|The Wailers)

1987: Revolution (Alpha Blondy album)|Revolution

1989: The Prophets (album)|The Prophets

1992: Masada (album)|Masada

1993: SOS Guerres Tribales

1993: Live Au Zénith (Paris)

1994: Dieu

1996: Grand Bassam Zion Rock

1997: Best Of (Alpha Blondy album)|Best Of

1998: Yitzhak Rabin (album)|Yitzhak Rabin

1999: Elohim (Alpha Blondy album)|Elohim

2001: Blondy Live Paris Bercy

2002: Merci

2005: "Akwaba"


Hii ni historia kwa ufupi ya Seydou Kone a.k.a Alpha Blondy.Kwa wale wapenzi wa Reggae kama mimi nadhani mtakuwa mmemjua japo kwa ufupi.Next time ntaleta kuhusu malegendary wengine wa aina hii ya mziki.

Analyse.
 

Attachments

  • 1433977536029.jpg
    1433977536029.jpg
    25.8 KB · Views: 476
Karibuni wadau wapenzi na mashabiki wa Reggae
 
Bloodshed in africa,mystic night move,masada,peace in liberia na comeback jesus hzi nazkubali sana japokua kiumjumla namkubali sana jamaa
 
Bloodshed in africa,mystic night move,masada,peace in liberia na comeback jesus hzi nazkubali sana japokua kiumjumla namkubali sana jamaa

Tuko pamoja sana mkuu kwa hilo.Kwa ufupi ukisikiliza nyimbo za jamaa kuna vitu utajifunza tu
 
Tuko pamoja sana mkuu kwa hilo.Kwa ufupi ukisikiliza nyimbo za jamaa kuna vitu utajifunza tu

Yaa mkuu,jamaa alikua na ushairi flan hvi kama wa BOB,nakumbuka nlishawah soma stori yake akiwa balozi wa amani wa UN kwa nchi za africa ya magharibi aliandika BOB MARLEY kwenye plat namba za gari kwakua anasema ni mmoja wa mtu aliyemuinspire kufanya mziki wa hvyo na hadi leo anaamini yeye kwake BOB ndio bora
 
"Babylon shall not rise Again.........."-Alpha Blondy. Naukubali huo wimbo balaa
 
pia huyo ni mwanamuziki pekee afrika kufanya kazi na the wailers.

Jamaa ni mtu wa kujituma sana na anajua anachokifanya,most of Reggae artist they r aware of their doings
 
Yaa mkuu,jamaa alikua na ushairi flan hvi kama wa BOB,nakumbuka nlishawah soma stori yake akiwa balozi wa amani wa UN kwa nchi za africa ya magharibi aliandika BOB MARLEY kwenye plat namba za gari kwakua anasema ni mmoja wa mtu aliyemuinspire kufanya mziki wa hvyo na hadi leo anaamini yeye kwake BOB ndio bora

Hata ukisikiliza ule wimbo wa Mystic Night Move utaskia kuna seheme anamtaja Bob...anaposema "i receaved terrible news yesterday night,when i heard that Bob Marley died".

Mystic Night Move ni wimbo mzuri sana,ni moja kati ya nyimbo alizoimba kwa uchungu akizungumzia Black Heroes
 
"Babylon shall not rise Again.........."-Alpha Blondy. Naukubali huo wimbo balaa

Jamaa ni motivator sana kama ilivyo kwa wanamuziki wengi wa Reggae.Ukisikiliza wimbo wake flan unaitwa "Afrique Antilles" utazidi kumkubali zaidi,napenda mstari mmoja anaposema "Piece of wood in a river will never be a crocodile" nadhani kwa mpambanaji yeyote atakuwa kamuelewa alichomaanisha
 
Hata ukisikiliza ule wimbo wa Mystic Night Move utaskia kuna seheme anamtaja Bob...anaposema "i receaved terrible news yesterday night,when i heard that Bob Marley died".

Mystic Night Move ni wimbo mzuri sana,ni moja kati ya nyimbo alizoimba kwa uchungu akizungumzia Black Heroes

Yaa man,kwenye hiyo ngoma anajiuliza why heroes n luck people they die so soon
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom