Kisa cha Alpha Blondy kuandika ngoma ya 'Sweet Fanta Diallo'

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
5,721
10,220
KISA CHA 'ALPHA BLONDY' KUANDIKA NGOMA YA "SWEET FANTA DIALLO."
--------------------------------------------------

Katika kitabu chenye list ya wanamuziki bora wa muda wote wa rege barani Africa. Sio simulizi ya kutisha kama jina lake litawekwa katika 3 bora. Alizaliwa Ivory coast mwaka mpya 1953. Akapewa jina la "Seydou Kone."

Alipoanza mchakato wa kujitafutia riziki kupitia mziki wa rege. Akajipa jina la "Alpha Blondy." 'Yerusalemu' ni ngoma ambayo ililiweka jina lake kwenye ramani ya dunia."

Kuna wakati fulani Alpha Blondy alipata tatizo la msongo wa mawazo. Akalazwa katika hospital ya taifa ya Ivory coast. Kitengo kinacho deal na watu wenye changamoto ya afya ya akili. (Psychiatrist hospital.)

Akiwa hospital alikuwa akihudumiwa na manesi wazuri sana. Lakini kuna nesi mmoja alikuwa akimuhudumia katika kiwango cha imani ya ajabu.

Na mara zote huyo nesi alipokuwa akienda kumuhudumia. Alikuwa akihakikisha hakuna mtu yoyote ndani ya chumba alicholazwa Alpha Blondy. Alpha Blondy akawa anajiuliza?! Kwanini watu wote wanapoondoka wodini ndipo yule nesi anakuja kumuhudumia?!

Akawa amepanga siku moja amuulize yule nesi. Anaishi wapi? na kwanini huwa anakuja kumuhudumia?!

Lakini kila alipokuwa akimuona. Ucheshi na tabasamu la yule nesi vilikuwa vinafanya asikumbuke swali lake. Na kila yule nesi alipokuwa akianza kumuhudumia. Alpha Blondy alikuwa akipitiwa na usingizi.

Alpha Blondy alitakiwa kukaa hospital kwa week chache. Lakini baadaye akajikuta ametimiza miezi minne.

Akawa anamfikiria sana yule nesi huku akijiuliza?! Kama atakuwa kaolewa?! au bado yupo single kwa hofu ya kuuza uhuru wake?! Kwa kifupi moyo wa Alpha ulianza kutumbukia ndani ya shimo la huba kwa yule nesi.

Siku moja yule nesi akiwa anamuhudumia Alpha Blondy. Alimuuliza Alpha, "Alpha Blondy unanipenda?!

Alpha Blondy akashituka! sababu ilikuwa mara ya kwanza. Yule nesi kulitaja jina lake tangu alipoanza kumtibu. Alpha Blondy akajibu, "ndio nakupenda." Wewe je unanipenda pia?!

Yule nesi hakujibu chochote. Ila alimwambia Alpha. Yeye anaitwa "FANTA DIALLO." Wakati anatoka wodini nesi aliliachia tabasamu zito. Ambalo lilimchanganya na kuuvuruga mfumo wa akili ya rasta Alpha Blondy.

Alpha akawa anaamini. Hospital inayotibu wendawazimu imemtunuku zawadi ya kumkutanisha na mwanamke wa ndoto zake.

Bahati mbaya baada ya siku ile. Mboni za macho ya Alpha Blondy hazikuwahi kukiona tena kiumbe kile.

Afya yake Alpha ilipoimarika. madaktari walimruhusu aivunje ndoa na kitanda cha hospital. Siku moja Alpha Blondy alirudi katika hospital ile kwenda kumshukuru nesi "FANTA DIALLO."

Safari yake haikubeba kheri na baraka. Ilikuwa ni moja kati ya siku zilizomkabidhi kitabu cha historia ya maumivu. Pale hospital wakamwambia. Hawajawahi kuwa na record ya kumuajiri nesi au muuguzi yoyote anayeitwa "FANTA DIALLO."

Alpha Blondy alimtafuta kila sehemu nesi Fanta Diallo. Lakini hakuwahi kumuona. Ndipo alipozama booth na ku release ngoma ya "SWEET FANTA DIALLO."

Akielezea yule hakuwa nesi. Bali ni malaika aliyemtokea kumpa utabibu katika taswira ya umbo la ubinadamu.

Baadhi ya mistari ya wimbo ule Alpha Blondy anaimba hivi.

Fanta Diallo kwa sasa unapita katikati ya upinde wa mvua. Unatetema katika mawimbi ya mwanga wa mwezi. Unanikumbatia katikati ya kilele cha mlima. Unanibusu tukiwa kwenye miamba inayowaka moto."

Imeandikwa kutoka mtandaoni
 
Back
Top Bottom