Aliyoyasema Mtela Mwampamba siku 2 kabla ya bomu kulipuka Arusha

HAMY-D

JF-Expert Member
Sep 18, 2011
7,149
3,818
Haya ni maneno ya kada wa CCM bwana Mtela Mwampamba kuhusiana na mchakato wa uchaguzi jijini Arusha;

"Tutaona, tuko Arusha kwa kazi maalumu kuhakikisha CCM ina shinda hata kama wananchi hawata tuchagua, na tutahakikisha wanaingia gharama kubwa ya kuishabikia CHADEMA."

Nadhani kama wewe ni mtu mwenye akili timamu unaweza kuona ni kwa kiasi gani chama tawala CCM kina husika na mpango, utekelezaji na ufanikishaji wa mlipuko wa bomu jana katika mkutano wa kufunga kampeni wa CHADEMA, Soweto Arusha.
 
Watatoa kauli nyingii sana wakijua kuwa kuna nguvu ya polisi na watawala madhalimu wakiwalinda kwa gharama zozote..lakini mwisho wa yote hawataishi kwenye mgongo huu wa ardhi milele ipo aiku yatawafika tu yqnqyowastahili kwa maovu wayatendayo.
 
Haya ni maneno ya kada wa CCM bwana Mtela Mwampamba kuhusiana na mchakato wa uchaguzi jijini Arusha;

"Tutaona, tuko Arusha kwa kazi maalumu kuhakikisha CCM ina shinda hata kama wananchi hawata tuchagua, na tutahakikisha wanaingia gharama kubwa ya kuishabikia CHADEMA."

Nadhani kama wewe ni mtu mwenye akili timamu unaweza kuona ni kwa kiasi gani chama tawala CCM kina husika na mpango, utekelezaji na ufanikishaji wa mlipuko wa bomu jana katika mkutano wa kufunga kampeni wa CHADEMA, Soweto Arusha.

Kweli gharama imekuwa kubwa sana:

Hali siyo shwari polisi wanalipua mabomu watu wamejeruhiwa

Bomu lililolipuka limejeruhi watu sana. Inaonekana bomu lilitegwa karibu na gari la matangazo.

Mtoto aliyelipukiwa na bomu amefariki uwanjani.

===========================
Updates toka kwa Washiriki
===========================

attachment.php

attachment.php

PICHA ZAIDI TEMBELEA HII POST -> https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-wahofiwa-kupoteza-maisha-25.html#post6590788
 
Haya ni maneno ya kada wa CCM bwana Mtela Mwampamba kuhusiana na mchakato wa uchaguzi jijini Arusha;

"Tutaona, tuko Arusha kwa kazi maalumu kuhakikisha CCM ina shinda hata kama wananchi hawata tuchagua, na tutahakikisha wanaingia gharama kubwa ya kuishabikia CHADEMA."

Nadhani kama wewe ni mtu mwenye akili timamu unaweza kuona ni kwa kiasi gani chama tawala CCM kina husika na mpango, utekelezaji na ufanikishaji wa mlipuko wa bomu jana katika mkutano wa kufunga kampeni wa CHADEMA, Soweto Arusha.

Jee tumesahau wale waliosema nchi haitatawalika, nao walikuwa na maana hii ya mambo yanvyo tokea Arusha au vipi?
 
CCM wanaamini wataishi kama mawe.....zetu dua.....tulianza na Mungu na tutamaliza na Mungu,safari ya wana wa israel ilikuwa ngumu na vikwazo vya kila aina lkn walifika,hata cc tutafika tena siku si nyingi japo muovu ccm amedhamiria kutupunguza speed ila si neno,nia tunayo na sababu tunayo......Tanzania ni yetu sote.
 
Ni kweli ccm na polisi wana usika baada ya bomu kulipuka tulipokuwa tunasaidia majerui polisi wakawa wanaturushia mabomu ya machozi na risasi za moto na maganda ya risasi tunayo.Walizidisha mabomu na risasi za moto pale alipokamatwa mtu aliyeshukiwa ndie alirusha hilo bomu watu wakatawanyika wakamuachia.mashuuda wanasema alipakiwa kwenye gari la polisi.
 
Jee tumesahau wale waliosema nchi haitatawalika, nao walikuwa na maana hii ya mambo yanvyo tokea Arusha au vipi?

Mkuu, tusipindishe mada, kitu pekee hapa nchini chenye dhamana ya kulinda raia na mali zao ni polisi kwa niaba ya serikali.

Sasa kama kuna mtu alitoa maneno hayo uliyo yaweka na hawakumchukulia hatua yoyote, udhani kwamba serikali ina udhaifu?

Kauli hii aliyo itoa Mtela sio nyepesi hata kidogo ukiliangalia na tukio la jana, nadhani kuna namna ana husika, na wa kuthibitisha hilo ni vyombo vya ulinzi na usalama.
 
"Siasa za arusha ni za Lema na Lowasa,japo ccm imepeleka watu wengi ukizingatia lowasa ana nguvu za kutosha kabisa pale arusha na monduli ila kwa Jembe hili i do salute him<Lema ebu idhihirishie dunia kuwa wewe ni zaidi yao,kuwa wewe ni kiboko yao,jembe lao> japo najua una maadui wengi na wako ladhi kufanya kila aina ya umafia ili cdm ipoteze majimbo yote,moja wapo ni mkuu wa mkoa,policcm,mwigulu na team yake,nape na team yake,lowasa na team yake,usalama.ikulu as ikulu na bado lile jeshi la GG nasikia nalo limeingia jana usiku hapo,kazi kwako jembe"Ndugu yangu Molemo unakumbuka huu ujumbe wa jana? uko salama lakini? Tumshukuru mungu kwa yote japo wengine sio manabii ila kwa sasa nchi inakoelekea hata mtoto mdogo anaweza tabiri kitu na kweli kikatokea...
 
Jee tumesahau wale waliosema nchi haitatawalika, nao walikuwa na maana hii ya mambo yanvyo tokea Arusha au vipi?
je wewe unafikiri nchi inatawalika? Kama ccm na vibaraka wake wanang'oa watu kucha bila ganzi? Je kama kina dr. Ulimboka wanang'olewa kucha na meno na usalama wa taifa? Je kama wapinzani nchi nzima wanapata vipigo huku polis wakishuhudia? Je nchi itatawalika vip wakati rais wa nchi muda wote yuko angani? Badala ya kuwatumikia watanzania kwa usawa bila kujali itikadi zao? Je nchi itatawalika vip wakati polis wanalinda usalama wa upande mmoja tu badala ya watanzania wote? Ilhali polis wanalipwa na watanzania wote? Binafsi sioni nuru kwenye taifa letu kama ccm itaendelea kuwa na viongozi kama mwigulu! Ccm ni janga kwa taifa letu!
 
Watanzania wenzangu ... Nani kahusika na Nani hakuhusika kwenye kusababisha tukio hili sio muhimu sana. Jambo la msingi na la kweli kabisa ni kuwa tukio limetokea. Na Kuna Serekali na vyombo vyake katika kulinda Usalama na Usatawi wa Wanachi. Wote hawa wajipime kama wametekeleza majukumu na viapo vyao ipasavyo!

Kwani Cheo ni Dhamana!!
 
Mbona jibu unalo mkuu, tukio limetokea jana, sasa siku mbili kabla ya jana itakuwa lini?

jamaa wa magwanda kwa uzushi ndio wenyewe.hata kiongozi mmoja wa magwanda alidiriki kusema kama watanzania wanakufa kwenye mikutano yao sio tatizo kwani wanawake wataendelea kuzaa.mimi wakuhojiwa ni huyohuyo aliohutubia na ndio aliwahi kutoa kauli hiyo.na hii ni wazi.kwani ni mbinu ya kuahirisha uchaguzi kila wanapoona hawajajipanga.kama ni mfuatiliaji durusu chaguzi zote za wenyeviti wa halmashauri,na manispaa na majiji.karibu zote huahirishwa siku iliopangwa na kufanyika siku nyingine na ndipo migogoro huzuka.
 
IGP huu ni muda wa kuwaonyesha watanzania unafanya kazi kamata wote wachochezi hawa
 
Back
Top Bottom