Aliyonambia baba padri kuhusiana na ndoa leo

watu mbona mna mawazo potofu hivi jamani....aliongelea mambo ya ndoa za ulaya hasa ufaransa zinavyofail na hivyo kanisa liko katika mkakati wa kujaribu kuangalia upya taratibu za kufungisha ndoa huko wakishirikiana na serikali pia alinishauri kuhusiana na carrier yangu na maisha kwa ujumla wala sivyo unavyowaza....
Mmmh, hiyo statement ina ujumbe uliojificha ndani yake. Ndiyo maana hujataka kuyaandika mengine. Bila shaka anataka uzae na yeye. Na kwa kuwa ushasema vijana wa siku hizi hawaeleweki, basi baba paroko anaweza kuwa ni chaguo zuri kwako au vipi? Si hana mke?
 
Lukolo,Nadhani wewe ni mtu unayeheshimika.
Siamini kama hujui maisha ya mapadri, au ni kejeli za kutafutia usingizi.
 
Last edited by a moderator:
Umejua mizambi yako ndo maana hujaniita kwenye kithread chako! Mother Teresa!!!!!!!!!!
 
hahahahahahah zimeshasamehewa zote....usinielewe vibaya shosti lara 1
Umejua mizambi yako ndo maana hujaniita kwenye kithread chako! Mother Teresa!!!!!!!!!!
 
Last edited by a moderator:
hahahahahahah hilo sikulisema lol situngekesha nikipewa semina!!! usiharibu bana..nami ni mwanadamu tu lol
JE ULIMWAMBIA PADRI YOU ARE IN FAVOUR OF CHEATTING HUSBANDS????????????????? Or you hid your dirty little secret!!

I know you better!
 
Kweli kabisa alicho sema baba padri ni muhimu sana, kwani wengi wamekuwa wakiziogopa ndoa kwa kuangalia matukio ya kila leo, pengine yamewatokea au yanayo tokea! Na wengine wa nahapa kuto oa ua kuolewa baada ya kuona matukio hasa wanawake kwani wao wanaogopa kuumizwa na sababu kubwa wanasema wanaume sikuhizi waongo na kusahau kuwa uongo hauna jinsia!

Ni vyema watu wakakubali kuyakabili matatizo na kumuomba mungu awape wa kufanana nao na bila kusahau mungu hatoi malaika bali ana kupa binadamu mwenzio pengine anaweza kubadilika muda wowote, cha msingi ni kuomba na kujipanga kuyakabili yote!

Ni vigumu kuzuia cheating kwa kukwepa ndoa, watu wana sahau hata tunao waona wana nyuso za furaha na wao wana matatizo kama ya binadamu wengine!

Kuolewa au kuoa si lazima lakini hatuwezi kuzuia maumivu kwa kukwepa ndoa!

Siku ya leo niliamka nikiwa najifeel so down kwakweli, ni kutokana na ishu moja iliyonikuta hivi karibuni.Basi hata kibaruani nilikwenda shingo upande tu kwani walinipigia simu kuniita.siku ilienda kichovuchovu na niliondoka mapema, basi wakati nimefika kwenye kituo cha daladala nikaamua niende chachi nikaonane na baba padri nimweleze yalonisibu.kanisa liko maeneo ya karibu na kibaruani na mwendo wa nusu saa kutoka kituo cha daladala.Nilifika nikaeleza hitaji langu nikaelekezwa shambani alimokuwepo baba padri akishughulika.Nikamsalimu then akanikaribisha bustanini, tukaketi na nikamweleza shida yangu.lilikuwa ni swala la kiroho ambalo kwakweli lilikuwa limenikosesha raha, basi alinipa msaada mkubwa kweli na kwa kiasi kikubwa alinitua mzigo ulokuwa umenielemea.

baada ya kumaliza kunitibu kiroho, basi baba padri akanichapa swali, akaniuliza binti una umri gani??? nikamtajia magunia ya chumvi niliyokula, then akanitundika swali lingine, akaniuliza, je una mpango gani na swala la ndoa?? (nikajisemea moyoni loh huu mwaka wa kupewa ujumbe wa ndoa) nikamjibu baba padri wajua vijana wa sikuhizi hawapendi kuingia kwenye ndoa, kwani kwao ni jukumu kubwa na miye sitaki kuuvaa mkenge so bado nasoma mazingira.Basi baba padri akaanza kutiririka ,akanambia unajua kijana wa kiume aweza kutana na binti kwenye daladala na wakifika mwisho wa safari wanaishia gesti...limekuwa jambo la kawaida kwa vijana wa sasa kwani maisha wanayachukulia kiteknolojia zaidi.wasichana wanaangalia nani mwenye qualifications za kumwezesha kufikia malengo yake hivyo ni rahisi kwao kubadili wapenzi mara kwa mara, hivyo swala la mahusiano na ndoa wengi wanayachukulia kama ajira, na mwenye vigezo ndo anapewa nafasi.swala la upendo wa dhati halipewi kipaumbele kwenye mahusiano ya siku hizi na ndo sababu ndoa nyingi hazidumu.Ila hayo(huku akinitazama usoni) yasikufanye uepuke sakramenti ya ndoa, Mungu aliiweka kwa makusudi yake ya kuendeleza kizazi na ni muhimu watoto wazaliwe, wakue na walelewe katika familia ili tuweze kupata jamii iliyo bora.Akahitimisha kwa sala nami nikaaga na kurudi kwangu.Huu ni ujumbe wa baba padri kwa vijana wote so muusome na muufanyie kazi.
 
Jamani usiku mwema kwenu nyote...wacha nilale mapema ili nidamke nijisomee...nimepata bahati ya kuitwa kwenye written interview Jumamosi na maswala ya sheria tena inabidi mtu kurudia vifungu.....Gnite to you wana JF wote
 
Au Ciello na wewe ni wale mnaotaka mume mwenye Vogue ilhali baba yako ana Baiskeli ya Swala! Ridhika kama mama yako...
 
Last edited by a moderator:
Jamani usiku mwema kwenu nyote...wacha nilale mapema ili nidamke nijisomee...nimepata bahati ya kuitwa kwenye written interview Jumamosi na maswala ya sheria tena inabidi mtu kurudia vifungu.....Gnite to you wana JF wote

bora uelewe tuu kuliko kuandika kifungu ambacho ukikosea utakuwa umebadilisha maana yote,japo vifu vina kuongezea marks kama umevishika! Nyc preparation
 
Jamani usiku mwema kwenu nyote...wacha nilale mapema ili nidamke nijisomee...nimepata bahati ya kuitwa kwenye written interview Jumamosi na maswala ya sheria tena inabidi mtu kurudia vifungu.....Gnite to you wana JF wote

Ha kumbe kuna wanasheria humu...bi ciello naomba kesho niku PM kuhusu jambo fulani 'linalonitatiza na kuninyima usingizi kiroho na kiakili ila halihitaji ushauri wa baba padri!!!'!???
 
inasaidia sana kuongea na Padri kama umetatizika kiroho.

Unamuuliza maswali yote hata yale ya kijinga yanayohusu imani, anakusaidia.

Ukitoka hapo, unakuwa na nguvu ya kuendelea na maisha.
 
kama ukienda kwa kitubio, kuficha haisaidii kitu.

Maana hata ukimficha padri, Mungu anaona, bora kumwaga yoote hadharani.

Wale watu wanasikia mambo lakini, hadi inatisha ku-imagine tu.

JE ULIMWAMBIA PADRI YOU ARE IN FAVOUR OF CHEATTING HUSBANDS????????????????? Or you hid your dirty little secret!!

I know you better!
 
Mhmhh! we BornAgainst Tungeoa wote nani Angetibu Roho ya Cielo??

Yeye kama padri anajua kuwa Mungu aliiweka ndoa kwa makusudi yake ya kuendeleza kizazi na ni muhimu watoto wazaliwe, wakue na walelewe katika familia ili tuweze kupata jamii iliyo bora yeye mbona hakuoa ili atii maagizo ya Mungu
 
Jamani usiku mwema kwenu nyote...wacha nilale mapema ili nidamke nijisomee...nimepata bahati ya kuitwa kwenye written interview Jumamosi na maswala ya sheria tena inabidi mtu kurudia vifungu.....Gnite to you wana JF wote

Ulale unono...gd nyte..
 
Halafu nimejifunza kitu kwako Ciello
Hawa watumishi ni muhimu sana kuwaona ngoja nipange siku nitinge kwa parish kabisa...
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom