Aliyonambia baba padri kuhusiana na ndoa leo

Nicole

JF-Expert Member
Sep 7, 2012
4,274
0
Siku ya leo niliamka nikiwa najifeel so down kwakweli, ni kutokana na ishu moja iliyonikuta hivi karibuni.Basi hata kibaruani nilikwenda shingo upande tu kwani walinipigia simu kuniita.siku ilienda kichovuchovu na niliondoka mapema, basi wakati nimefika kwenye kituo cha daladala nikaamua niende chachi nikaonane na baba padri nimweleze yalonisibu.kanisa liko maeneo ya karibu na kibaruani na mwendo wa nusu saa kutoka kituo cha daladala.Nilifika nikaeleza hitaji langu nikaelekezwa shambani alimokuwepo baba padri akishughulika.Nikamsalimu then akanikaribisha bustanini, tukaketi na nikamweleza shida yangu.lilikuwa ni swala la kiroho ambalo kwakweli lilikuwa limenikosesha raha, basi alinipa msaada mkubwa kweli na kwa kiasi kikubwa alinitua mzigo ulokuwa umenielemea.

baada ya kumaliza kunitibu kiroho, basi baba padri akanichapa swali, akaniuliza binti una umri gani??? nikamtajia magunia ya chumvi niliyokula, then akanitundika swali lingine, akaniuliza, je una mpango gani na swala la ndoa?? (nikajisemea moyoni loh huu mwaka wa kupewa ujumbe wa ndoa) nikamjibu baba padri wajua vijana wa sikuhizi hawapendi kuingia kwenye ndoa, kwani kwao ni jukumu kubwa na miye sitaki kuuvaa mkenge so bado nasoma mazingira.Basi baba padri akaanza kutiririka ,akanambia unajua kijana wa kiume aweza kutana na binti kwenye daladala na wakifika mwisho wa safari wanaishia gesti...limekuwa jambo la kawaida kwa vijana wa sasa kwani maisha wanayachukulia kiteknolojia zaidi.wasichana wanaangalia nani mwenye qualifications za kumwezesha kufikia malengo yake hivyo ni rahisi kwao kubadili wapenzi mara kwa mara, hivyo swala la mahusiano na ndoa wengi wanayachukulia kama ajira, na mwenye vigezo ndo anapewa nafasi.swala la upendo wa dhati halipewi kipaumbele kwenye mahusiano ya siku hizi na ndo sababu ndoa nyingi hazidumu.Ila hayo(huku akinitazama usoni) yasikufanye uepuke sakramenti ya ndoa, Mungu aliiweka kwa makusudi yake ya kuendeleza kizazi na ni muhimu watoto wazaliwe, wakue na walelewe katika familia ili tuweze kupata jamii iliyo bora.Akahitimisha kwa sala nami nikaaga na kurudi kwangu.Huu ni ujumbe wa baba padri kwa vijana wote so muusome na muufanyie kazi.
 
Bandabichi

JF-Expert Member
Jun 3, 2012
230
0
Sasa tujadili usemi wa Baba paroko unaonaje tukachukua hatua mama? Au wewe unazingatia nini katika kuchagua mume?
 
bornagain

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
3,384
2,000
Yeye kama padri anajua kuwa Mungu aliiweka ndoa kwa makusudi yake ya kuendeleza kizazi na ni muhimu watoto wazaliwe, wakue na walelewe katika familia ili tuweze kupata jamii iliyo bora yeye mbona hakuoa ili atii maagizo ya Mungu
 
snowhite

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
15,967
2,000
hili nalo neno !ngoja nianze mambo yangu yalee si wajua mi ndo event organizer humu ndani!
tuyaache hayo mamduchu!
ila umenigusa sna uliposema kuna kitu kimekufanya ukose raha mpka ukaona uende kwa baba padri!
Nimejaribu kujihoji mimi mwenyewe ni lini niliwahi kufikia hatua hii ya kujikana!?
UMENICHALLENGE i see!
 
Bandabichi

JF-Expert Member
Jun 3, 2012
230
0
Acha woga mdadaa maisha ni hayahaya hakuna mengine. Au unataka mpaka ukutane nae Sellena Hotel, Beach au Mlimani City. Muda ni huu. We hata hakuna haraka ya kunijibu. kaa ufikirie then urudi. Kama vp una watu unawaogopa ni PM.
 
Nicole

JF-Expert Member
Sep 7, 2012
4,274
0
yah ni kweli ni muhimu kujikana,mara nyingi likinisibu jambo lakunitatiza basi huenda chachi...either kupray ama kuzungumza na padri kama nikimkuta...
hili nalo neno !ngoja nianze mambo yangu yalee si wajua mi ndo event organizer humu ndani!
tuyaache hayo mamduchu!
ila umenigusa sna uliposema kuna kitu kimekufanya ukose raha mpka ukaona uende kwa baba padri!
Nimejaribu kujihoji mimi mwenyewe ni lini niliwahi kufikia hatua hii ya kujikana!?
UMENICHALLENGE i see!
 
Nicole

JF-Expert Member
Sep 7, 2012
4,274
0
si wote wameitiwa wito wa ndoa...hata paulo alisema hayo..
Yeye kama padri anajua kuwa Mungu aliiweka ndoa kwa makusudi yake ya kuendeleza kizazi na ni muhimu watoto wazaliwe, wakue na walelewe katika familia ili tuweze kupata jamii iliyo bora yeye mbona hakuoa ili atii maagizo ya Mungu
 
Nicole

JF-Expert Member
Sep 7, 2012
4,274
0
hahahahah sina haraka miye ingawa sauti za kunihimiza zinazidi lol....
Acha woga mdadaa maisha ni hayahaya hakuna mengine. Au unataka mpaka ukutane nae Sellena Hotel, Beach au Mlimani City. Muda ni huu. We hata hakuna haraka ya kunijibu. kaa ufikirie then urudi. Kama vp una watu unawaogopa ni PM.
 
Nicole

JF-Expert Member
Sep 7, 2012
4,274
0
hahahahahah kweli asee, baba padri amenigusa sana na maongezi yake..alinambia mengi sana ambayo hata sijayaandika hapa
mh chezeya sister maria salome wa Asizi wewe!ahahahahhahaa kama sio weye vile!kweli leo tunapata upako!LOL
 
Cynic

JF-Expert Member
Jan 5, 2009
5,147
2,000
baada ya kumaliza kunitibu kiroho, basi baba padri akanichapa swali, akaniuliza binti una umri gani??? nikamtajia magunia ya chumvi niliyokula, then akanitundika swali lingine, akaniuliza, je una mpango gani na swala la ndoa?? (nikajisemea moyoni loh huu mwaka wa kupewa ujumbe wa ndoa) nikamjibu baba padri wajua vijana wa sikuhizi hawapendi kuingia kwenye ndoa, kwani kwao ni jukumu kubwa na miye sitaki kuuvaa mkenge so bado nasoma mazingira.Basi baba padri akaanza kutiririka ,akanambia unajua kijana wa kiume aweza kutana na binti kwenye daladala na wakifika mwisho wa safari wanaishia gesti...limekuwa jambo la kawaida kwa vijana wa sasa kwani maisha wanayachukulia kiteknolojia zaidi.wasichana wanaangalia nani mwenye qualifications za kumwezesha kufikia malengo yake hivyo ni rahisi kwao kubadili wapenzi mara kwa mara, hivyo swala la mahusiano na ndoa wengi wanayachukulia kama ajira, na mwenye vigezo ndo anapewa nafasi.swala la upendo wa dhati halipewi kipaumbele kwenye mahusiano ya siku hizi na ndo sababu ndoa nyingi hazidumu.Ila hayo(huku akinitazama usoni) yasikufanye uepuke sakramenti ya ndoa, Mungu aliiweka kwa makusudi yake ya kuendeleza kizazi na ni muhimu watoto wazaliwe, wakue na walelewe katika familia ili tuweze kupata jamii iliyo bora.Akahitimisha kwa sala nami nikaaga na kurudi kwangu.Huu ni ujumbe wa baba padri kwa vijana wote so muusome na muufanyie kazi.
Uwe mwangalifu na huyu baba padri wako. Bottom line ni kwamba wao pia ni binadamu wa kiume kama wanaume wengine. anaweza akageuza somo wakati wowote, na akaishia kumsingizia shetani
 
adolay

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
11,190
2,000
hahahahah sina haraka miye ingawa sauti za kunihimiza zinazidi lol....

Chelewa chelewa utakuta mwana si wako na ngojangoja yaumiza matumbo japokuwa mbio za sakafuni huishia ukingoni na kukosa baraka.

Kazi Kwako Ciello
 
bornagain

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
3,384
2,000
si wote wameitiwa wito wa ndoa...hata paulo alisema hayo..
Asante mama naona upo vizuri kwenye neno, haya Mungu akubariki na vijana pia wabadilike maana sasa wakati ni ukuta watapambana nao lakini yatawashinda
 
Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
3,089
1,225
Ubarikiwe sana binti yangu Ciello wa Cicero. Nami nakushauri kama baba yako upige moyo konde uoleke na kuzaa matunda kama mama yako nami tulivyokuzaa wewe. Ni hilo tu kwa leo. Ubarikiwe sana na wale wanaokukwaza wabanikiwe kama si kubanikwa.
 
PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,216
1,500
Father amekwambia maneno ya msingi sana.
Ndoa zimepoteza maana siku hizi!. Hapa JF penyewe tunaona kila siku kupitia Jukwaa la Love Connect, jinsi watu wanavyotoa vigezo vya wanawake au wanaume wanaowataka, utadhani kuoa au kuolewa ni matter ya CV au sifa za mtu ki'uwezo.
Naamini Ciello utafuata vema maneno ya mtumishi wa Mungu na kuepuka 'harakaharaka'
 
Last edited by a moderator:

Lukolo

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
5,146
1,250
hahahahahah kweli asee, baba padri amenigusa sana na maongezi yake..alinambia mengi sana ambayo hata sijayaandika hapa
Mmmh, hiyo statement ina ujumbe uliojificha ndani yake. Ndiyo maana hujataka kuyaandika mengine. Bila shaka anataka uzae na yeye. Na kwa kuwa ushasema vijana wa siku hizi hawaeleweki, basi baba paroko anaweza kuwa ni chaguo zuri kwako au vipi? Si hana mke?
 
Nicole

JF-Expert Member
Sep 7, 2012
4,274
0
hahahahahahahah we acha kumwazia mabaya mtumishi wa MUNGU ,ingawa yes ni binadamu tena still bado kijana...but i respect him as a man of God nothing else...
Uwe mwangalifu na huyu baba padri wako. Bottom line ni kwamba wao pia ni binadamu wa kiume kama wanaume wengine. anaweza akageuza somo wakati wowote, na akaishia kumsingizia shetani
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom