Aliyewahi kupata kazi kupitia JF adhibitishe maana Duuuuu!!!

MAGAMBA MATATU

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
646
1,174
Ndugu qwenzangu wa Jamvini, naomba wale wote waliowahi pata kazi kupitia kuziona humu Jamvini wadhibitishe kwa maneno yao na ni wapi huko ili watu tusiwe tunasumbuka kusambaza CV zetu bila mafanikio.
 
We yaelekea ni mgeni humu!

1) Usiwe unaingia jamvini mara moja kwa mwezi!
2)Kama hata vp uwe unapitia angalau mara tatu kwa week!

3)Hautachangiwa tena na member yeyote hapa zaidi ya Mimi hapa!

4) Kuna wengi wamepata kazi kupitia Jf!
 
Ndugu qwenzangu wa Jamvini, naomba wale wote waliowahi pata kazi kupitia kuziona humu Jamvini wadhibitishe kwa maneno yao na ni wapi huko ili watu tusiwe tunasumbuka kusambaza CV zetu bila mafanikio.

mi nilipata na nikaacha...niliona hapa hapa jamvin
 
Nitumie cv yako, nimepata Tender za kuchimba mitaro Dar. Natafuta wafanyakazi wa kuchimba mitaro kama ume qualify ninaweza kukuita kwenye Interview.
 
Mimi binafsi nilishinda lile shindano la kudesign logo na poster ya miaka hamsini ya chuo kikuu cha Dar es salaam,..mwaka juzi mwishoni,.tangazo la issue ile nilipata link yake humu JF kwenyeforum ya tenders na jobs,..so huu ni mtandao unaoamnika!
 
Ndugu mtoa mada haimaanishi kwamba kila kazi utakayo iomba utaipata, ni kazi ngapi umeziona kwenye magazeti na ukatuma CV ukazipata, suala si JF suala ni CV yako ina nini, na pia nchi yetu kwa sasa who knows who. Anyway usikate tamaa hizo ni frustration za kawaida mtu unapokaa mtaani kwa muda mrefu ilhali una elimu yako Mwombe Mungu wakati ukifika utapata.
 
Atafutaye hachoki, akichoka keshapata. Kama unaona ni usumbufu kutuma CV, acha upumzike baba!
 
Kaka JF sio recruitment agency. Kama umeiona kazi humu ujue ipo pia kwenye sources zingine. Kama hujapata nenda tu kwa mganga lkn kazi zinazoandikwa humu hazimaanishi mwajiri ni JF
Mkuu , mie nishafanyiwa interview kwa kazi kama tatu nilizoziona huku JF na pia kuajiriwa na international org. kwenye post niliyoiona humu ndani.JF is real unless proven otherwise. Good luck ila usisahau kusali maana JF peke yake haiwezi kukupatia kazi ndugu.:amen:
 
Mimi niliona summary ya kazi humu nikafuatilia ktk gazeti husika na nikafanikiwa kupata kazi hiyo. Pia kwenye mtandao huu hapa kuana kazi nyingi za kimataifa na scholarships pia: wavuti.com  - Kilingeni
 
Back
Top Bottom