Aliyeuza ubunge chadema kutumika kuandaa ugaidi.

Aliyeuza ubunge chadema kutumika kuandaa ugaidi.

Joined
Dec 11, 2010
Posts
3,321
Reaction score
6,331
Aliyekuwa mwanachama na mgombea wa Chadema na kuuza ubunge mkoani Mbeya jimbo la Mbeya vijijini mara mbili na baadae kuhamia ccm ameendelea kutumika na kujifanya kuwa wakati yuko Chadema amesha wahi kuwa mjumbe wa ulinzi na usalama kwenye kurugenzi ya ulinzi na usalama chini ya Rwekatare.

Bwana huyo ambaye sasa amejiunga rasmi na timu ya Monduli kwa ajili ya mbio za uraisi 2015 anatumiwa kwa pamoja na yule Mhariri aliye vuliwa uhariri na wenzake kutoka na mwenendo wake wa kiuandishi na gazeti linalo milikiwa na mmoja wa watu wenye kashfa ya ufisadi mkubwa hapa nchini.

Zilizo vuja zinasema mchuuzi huyo wa ubunge kutoka Mbeya hivi karibuni atatumika kupitia gazeti la m--tanzania na watakuja na mpango mchafu wa kukichafua Chadema kwa kashfa za ugaidi ambao yeye atajifanya kuwa amesha wahi kufanya kazi kama mjumbe wa kurugenzi ya ulinzi na usalama na wamekuwa wana panga mipango ya kuteka na kuuwa. Nia hapa ni muendelezo wa kukipaka Chadema matope mbele ya umma.

Sambamba na hilo, mipango michafu ya kutaka kuihusisha Chadema na fujo za Mtwara ikiwa ni pamoja na kutaka kumpa kiongozi wa chadema mkoani Mtwara kesi ya ugaidi na uchochezi zinaelekea kugonga mwamba, kiongozi huyo amepewa dhamana baada ya kuwekewa mwanasheria na chama, mkumbuke kuwa alishikiliwa muda mrefu bila kupewa dhamana na bila kufikishwa mahakamani kwa zaidi ya masaa 48 kinyume na sheria.

Pamoja na hayo, Japo la wahariri wawili walio nunuliwa na mtuhumiwa wa ufisadi walikutana juzi ili kujipanga upya namna ya kutoa stori kwenye gazeti lao baada ya kunaswa kwa mpango wao wa awali, watatumia kadhia ya Mtwara kujipa uhalali wa kupotosha na kudai kuwa viongozi wa chadema wanapanga na wanajihusisha na fujo na mauwaji.

Tutaendelea kuona na kushuhudia mengi...

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums.
 
Mungu yu pamoja nasi...hakika tutashinda hila zote...
 
Kweli ccm imeshikwa pabaya badala kufanya maendeleo kwa wananchi they are using alot of our money just to do stupid things. Hawa maccm wanatakiwa waondoke madarakani. Wataondokaje ni mimi na wewe na yule kutoa elimu mahali npopote ulipo.
 
Sambwee Shitambala... Hafiki popote na huo mradi wao wa ''ugaidi'' kwakuwa wameshindwa kabla hawajaanza kuutekeleza.
 
Watashindana sana lakini watashindwa,hawa maccm na mbinu yao ya kutumia watu ambao ni makubwa jinga yenye njaa,hakika watashindwa kwa jina la Allah!/Yesu
 
Hizi ni tawile za mganga wala hamna lolote hapa mnatengeneza defence mechanism kwakuwa chama chenu kimekaa kimagumashi magumashi. Viongozi wa juu wana engeneer mipango miovu dhidi ya binadamu kisha mnaituhumu Ccm si mnaona mbowe alivyotengeneza utesaji wa Kibanda?
 
Watashindana sana lakini watashindwa,hawa maccm na mbinu yao ya kutumia watu ambao ni makubwa jinga yenye njaa,hakika watashindwa kwa jina la Allah!/Yesu

Samahani mkuu Allah sio yesu wala yesu hawezi kuwa Allah, Allah kamuumba yesu kwa maana yesu ni kiumbe Allah sio kiumbe tafadhali usimfananishe mungu na mwanadamu.
Nimekukumbusha tu.
 
hilo gazeti litaje ni la nani? unaogopa, mi nimtaje kwasababu nimewai kufika mwabepande na najua viunga vyake vizuri basi namtaja =ROSTAM AZIZ.
 
Hivi Sambwee Shitambala kule kwao MBeya akisema chochote kuhusu chadema huwa anashushwa kutoka kwenye stage, kila mtu anaamini shitambala kauuza ubunge mara mbili sasa akisema watu wote ndio tutathibitisha kwa asilimia mia kuwa yuko kwenye mission ashindwe na alegee
Kwa swala la mtwara wanafanya vizuri kuwakuwadia chadema kwamba ni chama imara kuliko chama chochote mtwara manake wananchi wanajua walivyokuwa wanajiumba na kutengeneza madai yao si mtu mmoja wala kikundi kimoja bali wanamtwara vinginevyo wakubali kulinda mtwara dumu daima na vifaru
 
Yaani Shitambala pamoja na njaa aliyonayo anataka kuongeza matatizo mengine ! Hana uwezo huo na huo ndiyo utakuwa Mwisho wake kwa Siasa za Mbeya ! Mbeya siyo NDAGO !
 
Bado, moyo wa Farao lazima uwe mgumu ili ukuu wa Mungu ushuhudiwe. Hivi punde CCM wataanza kupigwa mapigo kumi ya Musa, ili 2015 wawaache watanzania waende zao Kaanani...
 
Samahani mkuu Allah sio yesu wala yesu hawezi kuwa Allah, Allah kamuumba yesu kwa maana yesu ni kiumbe Allah sio kiumbe tafadhali usimfananishe mungu na mwanadamu.
Nimekukumbusha tu.

Asante kuu kwa kunikumbusha hata hivyo nilichokuwa nimekusudia ni kwa wale wanaoamini kwa Allah ni sawa na kwa wale wanaoamini katika jina la Yesu ni sawa.kwa hivyo basi nilichokuwa nimekikusudia hapo ni waumini wa dini mbili tofauti.wala sikuwa nimemanisha Allaha ndo Yesu wala Yesu ndo Allah
 
sawa sawa mbn humu siku hzi imekuja hali ya kuwa tunaficha majina ya watuhumiwa? kama una uhakika sema kma alivyofanya huyu bana, aisee nimekukubali inatakiwa namna hyo kama una uhakika na unachokisema wala usifiche jina lamtuhumiwa humu ndo tunapapenda coz tunapata habari kwa uhakika sio yale ya gazeti la uhuru ETI JINA KAPUNI
 
Samahani mkuu Allah sio yesu wala yesu hawezi kuwa Allah, Allah kamuumba yesu kwa maana yesu ni kiumbe Allah sio kiumbe tafadhali usimfananishe mungu na mwanadamu.Nimekukumbusha tu.
Mfuasi wa Allah uliyeamua kujitoa ufahamu. Unatetea ufisadi, ujangili, uuaji, kung'oa watu meno na kucha? ....au Allah wako ni tofauti na yule aliyehubiriwa na Mtume Mohammad SAW? Acha kuuaibisha uislam wewe!
 
Zilizo vuja zinasema mchuuzi huyo wa ubunge kutoka Mbeya hivi karibuni atatumika kupitia gazeti la m--tanzania na watakuja na mpango mchafu wa kukichafua Chadema kwa kashfa za ugaidi ambao yeye atajifanya kuwa amesha wahi kufanya kazi kama mjumbe wa kurugenzi ya ulinzi na usalama na wamekuwa wana panga mipango ya kuteka na kuuwa. Nia hapa ni muendelezo wa kukipaka Chadema matope mbele ya umma.


Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums.


Nitashangaa wasipo mkamata na kumuambatanisha na Rwakatare au wambinye Kende aseme alihusika wapi na wapi!
 
Hivi hii biashara ya habari za ugaidi inalipa sana ehee?
 
Sambwee Shitambala... Hafiki popote na huo mradi wao wa ''ugaidi'' kwakuwa wameshindwa kabla hawajaanza kuutekeleza.

Huyu jamaa ni mtu wa ajabu sana. Mwisho wake umefika kama vile walioutumainia mwili walivyoishia. CCM mnatakiwa mfahamu kwamba Mungu aishiye milele yupo. Ni Mungu ambaye hali sembe, wala hahitaji meno ya tembo na biashara ya madawa ili aimarishe Ukuu wake. Yeye ni Yeye na habadiliki siku zote na wala hachanganyikiwi. Kweli kwake inabaki kuwa Kweli na wala hahitaji baraza la wazee ama utetezi wa wakuu ili afahamike kuwa ni Mwenye haki. Yeye ni Mungu tu hata kama mtaamua kumchezea na kujifanya ni miungu. Ni upumbavu mkubwa sana kuendelea na mambo yenu ya hila mkidhani kwamba Mungu hayupo, haoni ama hajali.

CCM wamemblackmail shitambala kwa kumpa kazi moja yenye mambo mazito ili awape ushauri wa kisheria. Kwa kutumia u sensitivity wa hiyo biashara na facts alizokuwa tayari kazijua akaambiwa kwa usalama wa biashara, kazi yake na yeye mwenyewe aende ccm. Huko angepewa nafasi nzuri ambayo ingempa international exposure. Pia alitahadharishwa athari za yeye kukataa ushauri (black mailling) huo na akaopt ku surrender. Ajabu tangu aingie mtegoni mkataba wake na mwajiri wake mpya ukawa kama umeishia hapo na badala yake sasa analazimika kukubali kila anachoambiwa.

Shitambala mwogope Mungu anayeweza kuua mwili na roho. Shitambala na hao mafia wenzako tambueni hakuna fishy business ambayo iko free from mistakes. Umejiingiza pasipo penyewe. Weka mambo wazi uishi kwa amani hata kama utaacha siasa.

Unavyoendelea kujizamisha katika dimbwi la uhalifu wa ki demokrasia kwa kutunga na kutangaza uwongo huo mliopanga unamkosea Mungu na katika uwepo wa mwanadamu hakuna kitu chenye malipo mabaya na ya kutisha kama ku "provoke hasira ya Mungu".

CHADEMA mmepewa taarifa. Pelekeni hizi taarifa polisi mapema ili wazifanyie uchunguzi. Ninaamin polisi kama sekta yoyte ya serikali kuna rushwa na upotovu wa haki lakini si mara zote. Ipo siku watafany akazi kwa uadilifu hata kama nia yao ni kujisafisha. CCM wakianza kutekeleza uovu huo, wapelekeni mahakamani na sisi tunaendelea kuwaombea. CCM kwa mafisadi, CDM kwa Watanzania.
 
Shitambala anatumika kama tambala la deki kusafisha sakafu, kisha watamtupa juani akauke kisiasa!
 
Back
Top Bottom